Sawa Twende Taratibu
Magu amerithi deni la $16.2B toka kwa Kikwete kwa Gdp ya 49.99B
Mpaka mwishoni 2020 deni la Taifa lilikua 25.5B kwa GDP ya 66B so kulikua na ukuaji wa Pato la Taifa Takriban 16B na ukopaji wa 9.3B ndani ya miaka 5.
Deni la Taifa sasa hivi imezidi 33B ila hatuna data za 2024 za Gdp, natumia za 2023.
Mpaka 2023 GDP yetu ilikua ni 79B usd na deni 31B usd, sawa na ongezeko la 13B usd kwenye pato na 5.5B usd kwenye Deni
Ukiangalia ratio hapo
Magu 1.77
Samia 2.36
So kila 1 aliyokopa Magu alizalisha 1.77 na Kila moja aliyokopa Samia alizalisha 2.36.
Pengine ikawa ratio ya Samia imeshuka 2024 maana viashiria vinaonesha kuna ongezeko dogo ila still ni much better kuliko Magu.
Hivyo mtu yoyote yule anayemsema Samia na kumsifia Magu kwenye Suala zima la ukopaji ni mnafiki, tu wote Wawili Samia na Magu utawala wao tumeshuhudia ukopaji mkubwa mno, Wamekopa zaidi kuliko maraisi wote 1961-2014.
Halafu kumbuka Takwimu zako kuhusu SSH zinajumuisha miaka 2-3 tu (2021-2023), na uchumi hauwezi kupimwa kwa muda mfupi namna hiyo, na bado kwenye mahesabu umeboronga.
Kingine Miradi mingi inayochangia ukuaji wa GDP sasa ilianza enzi ya Maguful lakini matokeo yake yanaonekana sasa.
Magufuli alikumbana na changamoto za COVID-19 mwishoni mwa utawala wake
, hali iliyopunguza ukuaji wa uchumi, ingekuwa huyu SSH asingetoboa, hali ingekuwa mbaya vibaya sana.
Serikali ya JPM ilijenga miundombinu mikubwa ambayo inaweza kuwa na athari za muda mrefu.
Hata ongezeko la Pato la Taifa chini ya Rais Samia lina uhusiano mkubwa na juhudi za Magufuli. Miradi aliyoanzisha Magufuli imekuwa msingi wa maendeleo yanayoonekana wakati wa SSH.
Miradi ya Hayati JPM aliyoanzisha wakati wa uongozi wake imechangia katika ongezeko la Pato la Taifa chini ya SSH. matokeo yake yameendelea kuonekana hata baada ya uongozi wake kumalizika. ujenzi wa barabara na madaraja na upanuzi wa barabara mbalimbali umechangia kuboresha biashara na usafirishaji, hivyo kuongeza mzunguko wa fedha katika uchumi chini ya SSH.
Magufuli aliboresha usimamizi wa sekta ya madini kwa kusimamia mikataba na kuhakikisha serikali inanufaika zaidi, chini ya SSH mapato kutoka madini yameongezeka, ikiwa ni matokeo ya mfumo mzuri ulioanzishwa wakati wa JPM.
Na JPM angeendelea kuwepo, uchumi ungekuwa juu zaidi , angalia miradi aliyoacha kama SGR, faida zake mnaziona sasa katika ajira, biashara, na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo, angalia mradi mkubwa wa kuzalisha megawati 2,115 za umeme, kujenga madaraja n.k....