Watanzania siku mtapokezana madaraka baina ya vyama ndio mje mtutambie

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Watanzania naona mnafungua nyuzi nyingi nyingi za kututambia namna kwenu huko mna desturi ya kupokezana madaraka bila ugomvi, hiyo poa na hongera pia, ila bado sana maana siku mtapokezana uongozi baina ya vyama (kama sisi Kenya) ndio siku mje mtutambie kuhusu demokrasia.

Kwenu huko chama kimoja kile kile tu cha CCM, anayekiwakilisha huchaguliwa pale Dodoma na kundi la wazee, na huyo akishachaguliwa ndiye atakua rais, mengine yote kama vile kampeni na uchaguzi huwa maigizo tu.
Sisi huku tulithubutu kupokeza uongozi baina ya vyama, wapinzani walifika ikulu na kutawala na ndio maana tunatusua kwenye kila idara.

Yote tisa, huku Kenya tunaendelea siku saba za kumuombeleza marehemu Magufuli, pia tunamsklizia mama Suluhu atakuja kivipi, aidha atachezea mle mle au aboreshe. Ifahamike licha ya makelele ya kutia vifaranga kiberiti na ukamataji wa ng'ombe, uhusiano wetu kibiashara ulikua umeboreka, kuna namna timu ya Magufuli ilikua inahakikisha mambo yanaenda vizuri kimya kimya maana takwimu zinaonyesha mauzo yetu kwenda Tanzania yaliongezeka sana kipindi cha Magufuli.
 
Hakujawahi kuwepo chama cha upinzani nchini Kenya kilichowahi kuchukua madaraka ya nchi zaidi ya KANU, marais wote waliopita Kenya ni kutoka KANU ila wanachofanya ni maigizo tu ya kuanzisha kikundi (wanachoita chama) kisha wanachukua madaraka, uchaguzi mwingine ukifuata unamwona huyu anabadili tena jina la kikundi chake halafu inaonekana ni chama kingine kipya.

Hivi sasa kuna maigizo tena ya Jubilee, mara Tangatanga sijui na nini vile, lakini wote ni walewale tu. hakuna jipya, ni sawa na hapa Tanzania mwaka 2015 tulikuwa na wagombea wawili wa CCM na mmoja aligombea kupitia upinzani...
 
Hivi sasa kuna maigizo tena ya Jubilee, mara Tangatanga sijui na nini vile, lakini wote ni walewale tu. hakuna jipya, ni sawa na hapa Tanzania mwaka 2015 tulikuwa na wagombea wawili wa CCM na mmoja aligombea kupitia upinzani.
Kumekuwa na vyama vya kutwaa madaraka anapotoka rais hufa kifo cha asili! where is PNU?
 
Tanzania hakutatokea transition of power baina ya vyama bila mapigano.

Hata katiba mpya haitaweza kuwepo bila mapigano. CCM ni shetani kabisa.

Mfano halisi ni Zanzibar.
Kwa hiyo umekuja kushtakia. Pole sana kijana.

Laiti ungejua hao unakoshtakia kuwa ni wabovu kupitiliza. Ungebakia kimya.

Wewe subiri 2022 ndiyo utajua aina ya watu tunaopakana nao.
 
Sijasema wao ni bora. Ila wametuzidi mbali mnooooo
 
Kijana unahitaji kuwajua zaidi. Kwa ufupi, wenyewe wana ccm mbaya zaidi kuliko ya Tanzania. Wenyewe wana ccm yenye misingi ya damu na vinasaba, siyo kila mtu anaweza kuhamia. Tofauti na sisiem ya tz kila mtu anaweza kuingia na kupata nafasi. Kenya kuna deep state ambayo inaamua nani awe rais, kutoka makabila teule tu.
 
Ninyi mna vyama au makabila?

Ndio athari za demokrasia, kila mtu anapewa uhuru na fursa ya kuchagua kulingana na anavyotaka, akipenda azingatie kabila kama mojawpo wa vigezo, anapewa huo uhuru na katiba. Binafsi huwa najaribu kuhamasisha na kuhubiri watu watumie vigezo zaidi ya kabila, ila huo ni uhuru wao.

Sasa tukija kwa Tanzania, ndio mpo kama wafu au misukule kabisa, hamna uhuru wa chochote, yaani uamuzi hufanywa na wazee pale Dodoma nani awakilishe chama na huyo ndiye rais, utake usitake ndio basi.

Kwetu hapa tumebadlisha uongozi kwa vyama tofauti, chama cha KANU na mawaziri wake wote na makatibu na kila kitu walifagiliwa nje nje, upinzani ukachukua nchi na ndio maana mnaona uchumi wetu umezidi wenu mara mbili, yaani double double.
 
Kwenye upande wa democrasia you should shut up tuko juu yenu.Tanzania hakuna wapinzani wenye sifa ya kutuongoza.hii nchi ni nchi Malini Sana.
 
Watanzania naona mnafungua nyuzi nyingi nyingi za kututambia namna kwenu huko mna desturi ya kupokezana madaraka bila ugomvi, hiyo poa na hongera pia, ila bado sana maana siku mtapokezana uongozi baina ya vyama (kama sisi Kenya) ndio siku mje mtutambie kuhusu demokrasia.

Kwenu huko chama kimoja kile kile tu cha CCM, anayekiwakilisha huchaguliwa pale Dodoma na kundi la wazee, na huyo akishachaguliwa ndiye atakua rais, mengine yote kama vile kampeni na uchaguzi huwa maigizo tu.
Sisi huku tulithubutu kupokeza uongozi baina ya vyama, wapinzani walifika ikulu na kutawala na ndio maana tunatusua kwenye kila idara.

Yote tisa, huku Kenya tunaendelea siku saba za kumuombeleza marehemu Magufuli, pia tunamsklizia mama Suluhu atakuja kivipi, aidha atachezea mle mle au aboreshe. Ifahamike licha ya makelele ya kutia vifaranga kiberiti na ukamataji wa ng'ombe, uhusiano wetu kibiashara ulikua umeboreka, kuna namna timu ya Magufuli ilikua inahakikisha mambo yanaenda vizuri kimya kimya maana takwimu zinaonyesha mauzo yetu kwenda Tanzania yaliongezeka sana kipindi cha Magufuli.
Msaidieni Ruto kupambana na dynasty inayojificha kwenye vyama vya siasa, mkimaliza ndio mje na hoja hizi.
Hi
 
Magufuli ametuletea mambo ambayo tulikuwa tunasikia tu kwa majirani hivyo kuondoka kwake huenda ccm ikarudi kwenye kuheshimu uhai na hali za watu japo sio kwa standards za kimataifa. Kuingia upinzani itachukua muda mrefu sana kwanza upinzani wenyewe una matatizo ambayo ccm ya magufuli ilikuwa nayo.

Magufuli ni kiongozi pekee ambae ameligawa hili taifa kuliko kiongozi mwingine yoyote kwa ukanda,udini, kuibuka watu wasiojulikana waliokuwa wanadeal na upinzani tu, kuibuka kwa musiba, kuibuka kwa wasifiaji tu na kutaka aongezewe muda, wapinzani kuuawa hovyo bila kesi zao kushughulikiwa na mbaya kuliko yote ni kuwabrainwash watu bila yeye mambo hayaendi. Haya yote yalikithiri kwenye uongozi wake.

Ccm ilikuwa na madhaifu ya rushwa lakini haya aliyokuja nayo magufuli ni makubwa kuliko rushwa. Kufanya maendeleo hakuwezi kuoveride haki za binadamu kwa namna yoyote ile na mifano ni mingi ya nchi zilizoendelea huku zikiheshimu haki za binadamu.
 
Hakujawahi kuwepo chama cha upinzani nchini Kenya kilichowahi kuchukua madaraka ya nchi zaidi ya KANU, marais wote waliopita Kenya ni kutoka KANU ila wanachofanya ni maigizo tu ya kuanzisha kikundi (wanachoita chama) kisha wanachukua madaraka, uchaguzi mwingine ukifuata unamwona huyu anabadili tena jina la kikundi chake halafu inaonekana ni chama kingine kipya.

Hivi sasa kuna maigizo tena ya Jubilee, mara Tangatanga sijui na nini vile, lakini wote ni walewale tu. hakuna jipya, ni sawa na hapa Tanzania mwaka 2015 tulikuwa na wagombea wawili wa CCM na mmoja aligombea kupitia upinzani...
Nakazia
 
Kwa hiyo umekuja kushtakia. Pole sana kijana.
Laiti ungejua hao unakoshtakia kuwa ni wabovu kupitiliza. Ungebakia kimya.

Wewe subiri 2022 ndiyo utajua aina ya watu tunaopakana nao.
Kijana unahitaji kuwajua zaidi. Kwa ufupi, wenyewe wana ccm mbaya zaidi kuliko ya Tanzania. Wenyewe wana ccm yenye misingi ya damu na vinasaba, siyo kila mtu anaweza kuhamia. Tofauti na sisiem ya tz kila mtu anaweza kuingia na kupata nafasi. Kenya kuna deep state ambayo inaamua nani awe rais, kutoka makabila teule tu.
msikize vile mwenzako anavyokuambia la sivyo ukikaidi utapigwa2
 
Mimi huwa naona Kenya mnajidanganya sana kwa sababu ukiangalia jinsi Kibaki alichukua uongozi kutoka kwa Moi na kuwageuka wakina Raila na wenzake na akaanza kumpa nafasi Uhuru kwenye serekali yake unaona kabisa KANU ilijivika chama kipya anachoongoza Uhuru sasa. Naweza kusema bado hamjafikia hatua ya kutamba kupokezana nchi vyama tofauti.
 
Watanzania naona mnafungua nyuzi nyingi nyingi za kututambia namna kwenu huko mna desturi ya kupokezana madaraka bila ugomvi, hiyo poa na hongera pia, ila bado sana maana siku mtapokezana uongozi baina ya vyama (kama sisi Kenya) ndio siku mje mtutambie kuhusu demokrasia.

Kwenu huko chama kimoja kile kile tu cha CCM, anayekiwakilisha huchaguliwa pale Dodoma na kundi la wazee, na huyo akishachaguliwa ndiye atakua rais, mengine yote kama vile kampeni na uchaguzi huwa maigizo tu.
Sisi huku tulithubutu kupokeza uongozi baina ya vyama, wapinzani walifika ikulu na kutawala na ndio maana tunatusua kwenye kila idara.

Yote tisa, huku Kenya tunaendelea siku saba za kumuombeleza marehemu Magufuli, pia tunamsklizia mama Suluhu atakuja kivipi, aidha atachezea mle mle au aboreshe. Ifahamike licha ya makelele ya kutia vifaranga kiberiti na ukamataji wa ng'ombe, uhusiano wetu kibiashara ulikua umeboreka, kuna namna timu ya Magufuli ilikua inahakikisha mambo yanaenda vizuri kimya kimya maana takwimu zinaonyesha mauzo yetu kwenda Tanzania yaliongezeka sana kipindi cha Magufuli.
Hivi mbona Kamwana na Ruto wananuniana kama wameshikana ugoni? sioni ni jinsi gani Ruto anaweza kupewa nchi kama TZ ilivyofanya kwa mama Samia ikitokea Kamwana akawaacha.

Tunajua Mungiki wataingia mtaani na kuanza kazi yao iliyowapa umaarufu duniani...
 
Back
Top Bottom