Watanzania siku mtapokezana madaraka baina ya vyama ndio mje mtutambie

Watanzania siku mtapokezana madaraka baina ya vyama ndio mje mtutambie

Watanzania naona mnafungua nyuzi nyingi nyingi za kututambia namna kwenu huko mna desturi ya kupokezana madaraka bila ugomvi, hiyo poa na hongera pia, ila bado sana maana siku mtapokezana uongozi baina ya vyama (kama sisi Kenya) ndio siku mje mtutambie kuhusu demokrasia.

Kwenu huko chama kimoja kile kile tu cha CCM, anayekiwakilisha huchaguliwa pale Dodoma na kundi la wazee, na huyo akishachaguliwa ndiye atakua rais, mengine yote kama vile kampeni na uchaguzi huwa maigizo tu.
Sisi huku tulithubutu kupokeza uongozi baina ya vyama, wapinzani walifika ikulu na kutawala na ndio maana tunatusua kwenye kila idara.

Yote tisa, huku Kenya tunaendelea siku saba za kumuombeleza marehemu Magufuli, pia tunamsklizia mama Suluhu atakuja kivipi, aidha atachezea mle mle au aboreshe. Ifahamike licha ya makelele ya kutia vifaranga kiberiti na ukamataji wa ng'ombe, uhusiano wetu kibiashara ulikua umeboreka, kuna namna timu ya Magufuli ilikua inahakikisha mambo yanaenda vizuri kimya kimya maana takwimu zinaonyesha mauzo yetu kwenda Tanzania yaliongezeka sana kipindi cha Magufuli.
Hahahaha, mnajiandaa kulalamika, ghafla Magufuli amekua mtu mwema. Ninauhakika 120% mtaanza kulalamika kwamba Mama Samia haipendi Kenya ni bora Magufuli, ninyi ni watu wa kulialia na kuhusi dunia nzima haiwapendi.

Mlikua mnasema Kikwete alikua ni rafiki wa Kenya na Magufuli anaichukia Kenya, sasa mtasema Magufuli alikua ni mzuri kwa biashara zaidi za Samia Suluhu. Ninyi ni watu wa kuwapuuza
 
Back
Top Bottom