Watanzania tuachaneni na imani zilizopitwa na wakati

Habari zenu Watanzania,

Jamani mfumo wa maisha umebadilika sana tupo ulimwengu wa Technolojia ya hali ya juu.

Sababu ya kuandika uzi huu imetokana na kupokea habari ya msiba ya aliekuwa rafiki yangu ambae alikuwa anafanya kazi shirika la Umeme TANESCO kuwa amefariki.

Story yenyewe ipo hivi mdada alikuwa anaumwa Pumu, asthma kwa muda mrefu kama unavyojua Mbeya ni mji wenye baridi kali badala ya kumpeleka Hospitali Aunt yake akampeleka kwenye Maombi.

Huko kwenye kambi ya maombi wamekaa na mgonjwa week nzima mgonjwa kazidiwa mpaka amefariki.

Tukio lingine nimekutana nalo ni la kijinga sana yaani ukweni kwangu kuna mtu mzima alitoka bafuni kuoga akatereza kwenye ngazi na kuvunjika mfupa wa mguu mmoja eti wamemvundika ndani wanasema eti kachezewa kwa sababu eti pale alipojikwaa panaoneka sio pa kupelekea kuvunjika mfupa hivyo ukoo mzima unasema KARUSHIWA KOMBORA 😭😭😭😭 yaani nimecheka na kulia hapo hapo anyway ngoja nimalizie hicho kisa cha pili sasa.

Mpaka ninavyoandika hapa hawajampeleka mgonjwa hospitali wamemtumia nauli tulizochanga ndugu mzee fulani kutoka Tabora eti anaunga mifupa bila kugusa sehemu iliyovunjika week imeshapita mguu umeanza kuoza wanapeana tahadhari eti akipelekwa hospital watamkata mguu.

Anyway ngoja niseme kitu hapa Jamii ya WATANZANIA tuache kutumia Formular za kizamani haswa kwenye kusolve matatizo ya kileo.

Imani hizo zimeshapitwa na wakati hata hizo Dini zimeletwa na hao wazungu siku hizi huko kwao hawana Shobo nazo labda hii ya Uarabuni ambayo nayo kichomi kwa amani ya dunia kwa kuunganishwa na matendo ya kigaidi.

Kuamini uganga, Uchawi, amani za dini zilizopitiliza ni ushamba ambao hauna nafasi kwenye maisha ya kileo.ASANTE
Wagalatia ndo wajinga namba moja,wao kila kitu wana amini kwenye maombi
 
Umesema tuachane na maana zimeletwa na wazungu! Hospital nani kaleta? Zamani wakivunjika miguu walikuwa wanatibiwa na nani?

Binafsi sio muumini wa dini niponipo tu lkn kuhusu tiba sichagui asee kikubwa nipone iwe hospital au Kwa mitishamba.
Kama una imani hizi kichwani mwako una safari ndefu sana ya kuleta mapinduzi kwenye maisha yako ndugu
 
Umesema tuachane na maana zimeletwa na wazungu! Hospital nani kaleta? Zamani wakivunjika miguu walikuwa wanatibiwa na nani?

Binafsi sio muumini wa dini niponipo tu lkn kuhusu tiba sichagui asee kikubwa nipone iwe hospital au Kwa mitishamba.
Utakuja ufe kuamini ujinga ndugu
 
Habari zenu Watanzania,

Jamani mfumo wa maisha umebadilika sana tupo ulimwengu wa Technolojia ya hali ya juu.

Sababu ya kuandika uzi huu imetokana na kupokea habari ya msiba ya aliekuwa rafiki yangu ambae alikuwa anafanya kazi shirika la Umeme TANESCO kuwa amefariki.

Story yenyewe ipo hivi mdada alikuwa anaumwa Pumu, asthma kwa muda mrefu kama unavyojua Mbeya ni mji wenye baridi kali badala ya kumpeleka Hospitali Aunt yake akampeleka kwenye Maombi.

Huko kwenye kambi ya maombi wamekaa na mgonjwa week nzima mgonjwa kazidiwa mpaka amefariki.

Tukio lingine nimekutana nalo ni la kijinga sana yaani ukweni kwangu kuna mtu mzima alitoka bafuni kuoga akatereza kwenye ngazi na kuvunjika mfupa wa mguu mmoja eti wamemvundika ndani wanasema eti kachezewa kwa sababu eti pale alipojikwaa panaoneka sio pa kupelekea kuvunjika mfupa hivyo ukoo mzima unasema KARUSHIWA KOMBORA 😭😭😭😭 yaani nimecheka na kulia hapo hapo anyway ngoja nimalizie hicho kisa cha pili sasa.

Mpaka ninavyoandika hapa hawajampeleka mgonjwa hospitali wamemtumia nauli tulizochanga ndugu mzee fulani kutoka Tabora eti anaunga mifupa bila kugusa sehemu iliyovunjika week imeshapita mguu umeanza kuoza wanapeana tahadhari eti akipelekwa hospital watamkata mguu.

Anyway ngoja niseme kitu hapa Jamii ya WATANZANIA tuache kutumia Formular za kizamani haswa kwenye kusolve matatizo ya kileo.

Imani hizo zimeshapitwa na wakati hata hizo Dini zimeletwa na hao wazungu siku hizi huko kwao hawana Shobo nazo labda hii ya Uarabuni ambayo nayo kichomi kwa amani ya dunia kwa kuunganishwa na matendo ya kigaidi.

Kuamini uganga, Uchawi, amani za dini zilizopitiliza ni ushamba ambao hauna nafasi kwenye maisha ya kileo.ASANTE
Mpaka ccm itoke madarakani uzuzu utaisha kwa wananchi
 
Inasikitisha na kuchekesha kwa pamoja. Haya mambo ni ya ajabu bora yafanywe hata na mtu ambae hajasoma kabisa, wasomi wanayafanya sana.

Haya makanisa na wachungaji wa siku hizi wamegeuza watu mazuzu, sipingi maombi lakini mgonjwa apate tiba ya hospitali kwanza alafu maombi yaendelee.

Unakuta mtu kashinda juani kutwa nzima akifanya kazi ngumu na hajazoea, jioni kichwa kinamuuma anaanza kusema karogwa anaanza kukemea, huu ni uchizi.
 
yaani hueleweki hizo ndio imani zenu , hospital za kuletwa tu
Sorry for your loss
20240520_124032.jpg
 
Kuna jamaa aliugua malaria,ndugu zake wakasema ana pepo inabidi apelekwe Kanisani akaombewe,ndugu mmoja akakataa akampeleka mgonjwa hospitali.Ndugu wengine walokole njaa wakamwambia akifa utamzika mwenyewe,kesho yake majirani wakawasema sana ikabidi waende tu hospitali kishingo upande,wamefika kumuona mgonjwa wakakuta jamaa anakula kiepe yai huku anaendelea vizuri. Mambo ya Dini yanahitaji usome sana vitabu vinavyochambua maandiko na sio kuimbaimba kwaya tu
 
Back
Top Bottom