Watanzania tuachaneni na imani zilizopitwa na wakati

Wagalatia ndo wajinga namba moja,wao kila kitu wana amini kwenye maombi
 
Umesema tuachane na maana zimeletwa na wazungu! Hospital nani kaleta? Zamani wakivunjika miguu walikuwa wanatibiwa na nani?

Binafsi sio muumini wa dini niponipo tu lkn kuhusu tiba sichagui asee kikubwa nipone iwe hospital au Kwa mitishamba.
Kama una imani hizi kichwani mwako una safari ndefu sana ya kuleta mapinduzi kwenye maisha yako ndugu
 
Umesema tuachane na maana zimeletwa na wazungu! Hospital nani kaleta? Zamani wakivunjika miguu walikuwa wanatibiwa na nani?

Binafsi sio muumini wa dini niponipo tu lkn kuhusu tiba sichagui asee kikubwa nipone iwe hospital au Kwa mitishamba.
Utakuja ufe kuamini ujinga ndugu
 
Mpaka ccm itoke madarakani uzuzu utaisha kwa wananchi
 
Inasikitisha na kuchekesha kwa pamoja. Haya mambo ni ya ajabu bora yafanywe hata na mtu ambae hajasoma kabisa, wasomi wanayafanya sana.

Haya makanisa na wachungaji wa siku hizi wamegeuza watu mazuzu, sipingi maombi lakini mgonjwa apate tiba ya hospitali kwanza alafu maombi yaendelee.

Unakuta mtu kashinda juani kutwa nzima akifanya kazi ngumu na hajazoea, jioni kichwa kinamuuma anaanza kusema karogwa anaanza kukemea, huu ni uchizi.
 
Kuna jamaa aliugua malaria,ndugu zake wakasema ana pepo inabidi apelekwe Kanisani akaombewe,ndugu mmoja akakataa akampeleka mgonjwa hospitali.Ndugu wengine walokole njaa wakamwambia akifa utamzika mwenyewe,kesho yake majirani wakawasema sana ikabidi waende tu hospitali kishingo upande,wamefika kumuona mgonjwa wakakuta jamaa anakula kiepe yai huku anaendelea vizuri. Mambo ya Dini yanahitaji usome sana vitabu vinavyochambua maandiko na sio kuimbaimba kwaya tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…