Watanzania tuchangamkie fursa kibao zitazokuja na DP-World

Kuna watu wameambiwa bandari kapewa "mwarabu" hawajui kuwa Dpworld inaendeshwa na Wamarekani.....
Ile chuki Kwa waraabu inaweza fanya watu wapishane na gari la fursa...
DP World ni mtoto wa Dubai World ambalo ni mali ya waarabu wa dubai. Chanzo cha kufanya DP World iendeshwe na Wamarekani ni kwasababu bunge la Marekani halikuwataka waarabu waendeshe bandari za kimarekani na kuitia unajisi nchi yao, kitu ambacho sisi Tanganyika tumekiruhusu. Wamarekani walikubali DP World lifanye kazi nchini kwao kwa masharti ya kuendeshwa kupitia kampuni la Wamarekani liitwalo Ports America.

Huku kwetu watakuja kuendesha waarabu wenyewe, jambo ambalo ni hatari mno kwa usalama wa Tanganyika. Waarabu ni watu wa hovyo mno, utawatetea tu kwasababu za kidini, ila ni watu wa hovyo kwelikweli.
 
Mkuu hawa wapingaji wengi tatizo lao ni "Waarabu" ndio maana Mzungu anajipigia madini wanaona sawa tu,angepewa Mzungu bandari wangesifu kwa kila mapambio,

Sio kila issue muwe mnahusisha race au dini.
Watu wanachopinga ni terms za mkataba na muda wake, acheni kufanya spinning.
 
Bandari, reli, Tanesco, TTCL na airports zipewe managements companies hata kama ni za nje cha msingi mikataba ipitiwe thoroughly.
 
Huu ujinga wakuokota vitaarifa vya kampuni fulani mitandaoni na kuvipitisha kwenye google translate nakutuletea hapa ufike mwisho .pumbavu sana mleta uzi.
 
Majengo ya Kariakoo sio tatizo kwenye nchi hii ambayo raia wake wengi wanaishi vijijini kusiko na maji, umeme au barabara za lami.
 
Bandari, reli, Tanesco, TTCL na airports zipewe managements companies hata kama ni za nje cha msingi mikataba ipitiwe thoroughly.
Yaani Critical SOEs/Infrastructure za nchi yapewe makampuni ya nje ???
Hahahaha, kaaaaazi kwelikweli.....
 
Huu ujinga wakuokota vitaarifa vya kampuni fulani mitandaoni na kuvipitisha kwenye google translate nakutuletea hapa ufike mwisho .pumbavu sana mleta uzi.
Unafahamu maana ya neno IT?
. Hivi haoa JF tunatumia nini kuwadmsiliana?

Au hukupenda linetokea kwa wazee wa Madrassa?

Jibu kibingwa.
 
Ukoloni wa kisasa,ila kwa Tanzania na Afrika ni haki yetu kwani tuko usingizini bado bora Kuwa makoloni kwa mara nyingine,huenda tukazinduka usingizini 🤸🤸
 
Nchi ipo kwenye hali mbaya sana, haina pesa na madeni huku na kule. Ifirisike au ikodieshe bandari. Hata wewe ungekodisha bandari. Tuelewe hali halisi kama watu wazima, japo hatuambiwi ukweli wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…