Watanzania tufunge na Kuomba tukimlilia Mungu?

F4B

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2022
Posts
336
Reaction score
429
Katika nchi yetu kuanzia juzi vilio vya makato ya miamala ya Kibenk vimetikisa nchi yetu. Kwa bahati mbaya kabisa wenye mamlaka wamekuwa wakitoa majibu ya kejeri na kiburi ndani yake.

Hawasikii Wala hawana uchungu dhidi ya mamilioni ya watanzania wanao ogelea katika dibwi la umasikini huku wao wakiendeshwa Kwenye magari mazuri yanayoendeshwa kwa Kila kitu yaani gharama zote hadi mafuta na mshahara wa dreva na fedha kutoka kwa mama ntilie, machinga na watumishi wa umma wa ngazi za chini.

Kwa kuwa hawasikii wameziba masikio Yao je watanzania wanyonge tupige magoti tumlilie Mungu wetu aje atuokoe?? Ili aibadilishe mioyo ya viongozi wetu isiwe migumu??.
 
Upige magoti ili iweje, hebu tuachege upuuzi! Haya ndio yamefanya mpaka tumefikia kufananishwa na maiti. Watanzania kila jambo mmekuwa watu wa kulia lia tu. Fanyeni action watu waone mnamaanisha. Maneno matupu na kulia lia mitandaoni ni dalili ya kuwa mmeshindwa na mnyanyasaji (bull) ataendelea kuwagandamiza hadi kifo.

Nakumbuka enzi zetu tukiwa za shule za awali kulikuwaga na tabia ya bulling sana toka kwa baadhi ya wenzetu ambao walijiona wakubwa na wababe ila uonevu ulipozidi mwisho wake ilikuwa ni kukata mzizi wa fitina kwa parling. Ile spirit tulikuwa nayo watoto wa zama zile ni ya kupinga uonevu bila kujali anaekuonea ana nguvu kiasi gani. Zitapigwa ngumi hadi kuvujishana damu kisha kuanzia hapo kila mmoja atamuheshimu mwenzie. Kuanzia kesho huwezi tena kuitwa majina ya kudhalilishwa, kila mtu atakutazama kama mwanaume kamili.

Uoga ukizidi sana huzaa udumavu wa kudumu wa akili na unyonge kutamalaki. Tukemee hii roho na tusimame imara kudai katiba mpya kwa nguvu na ujasiri itakayolinda haki na maslahi yetu.
 
Ahaa kumbe ukiwa na kadi ya CCM makato hayakuhusu? Basi nielekeze nami niipate niwe "Anachukua anaweka ewaa.
 
Upige magoti ili iweje, hebu tuachege upuuzi! Haya ndio yamefanya mpaka tumefikia kufananishwa na maiti. Watanzania kila jambo mmekuwa watu wa kulia lia tu. Fanyeni action watu waone mnamaanisha. Maneno matupu na kulia lia mitandaoni ni dalili ya kuwa mmeshindwa na mnyanyasaji (bull) ataendelea kuwagandamiza hadi kifo.

Nakumbuka enzi zetu tukiwa za shule za awali kulikuwaga na tabia ya bulling sana toka kwa baadhi ya wenzetu ambao walijiona wakubwa na wababe ila uonevu ulipozidi mwisho wake ilikuwa ni kukata mzizi wa fitina kwa parling. Ile spirit tulikuwa nayo watoto wa zama zile ni ya kupinga uonevu bila kujali anaekuonea ana nguvu kiasi gani. Zitapigwa ngumi hadi kuvujishana damu kisha kuanzia hapo kila mmoja atamuheshimu mwenzie. Kuanzia kesho huwezi tena kuitwa majina ya kudhalilishwa, kila mtu atakutazama kama mwanaume kamili.

Uoga ukizidi sana huzaa udumavu wa kudumu wa akili na unyonge kutamalaki. Tukemee hii roho na tusimame imara kudai katiba mpya kwa nguvu na ujasiri itakayolinda haki na maslahi yetu.
Kumbuka Mungu ni Kila kitu au huamini
 
atika nchi yetu kuanzia juzi vilio vya makato ya miamala ya Kibenk vimetikisa nchi yetu.Kwa bahati mbaya kabisa wenye mamlaka wamekuwa wakitoa majibu ya kejeri na kiburi ndani yake.Hawasikii Wala hawana uchungu dhidi ya mamilioni ya watanzania wanao ogelea katika dibwi la umasikini huku wao wakiendeshwa Kwenye magari mazuri yanayoendeshwa kwa Kila kitu yaani gharama zote hadi mafuta na mshahara wa dreva na fedha kutoka kwa mama ntilie, machinga na watumishi wa umma wa ngazi za chini
Mbaya zaidi wanajiweka madarakani wenyewe, washona na kutatua viraka vya katiba, wanajipangia mishahara, posho, marupurupu wenyewe na sasa wanajimilikisha nchi wenyewe.
 
Kuna muda tuongee na Mungu katika lugha rafiki kama baba,sio kulia lia tu mbele zake.
Nna jirani,anaomba kwa sauti kila asub akilia, huwa nawaza hamna siku aongee na Mungu kwa amani mpaka ampigie kelele?
 
Acheni kumchosha MUNGU na ujinga wenu. Wakati mnaipigia kura fisiemu mnajeza song lao la mbele kwa mbele tumeipenda wenyewe sijui nini nini nini mnacheza hadi nguo zinaanguka mkabeba kura kwenye maboksi mkaharibu uchaguzi leo mnamsumbua Mungu kwenye ujinga wa hivi. Natamani kila atakaepiga goti kufunga Mungu achukue uhai wake pale pale. Mungu hadhihakiwi. Emu acheni ujinga mliutaka sana huu uongozi sasa tulieni na bado tozo ya kupumua inakuja.
 
Katika nchi yetu kuanzia juzi vilio vya makato ya miamala ya Kibenk vimetikisa nchi yetu. Kwa bahati mbaya kabisa wenye mamlaka wamekuwa wakitoa majibu ya kejeri na kiburi ndani yake.

Hawasikii Wala hawana uchungu dhidi ya mamilioni ya watanzania wanao ogelea katika dibwi la umasikini huku wao wakiendeshwa Kwenye magari mazuri yanayoendeshwa kwa Kila kitu yaani gharama zote hadi mafuta na mshahara wa dreva na fedha kutoka kwa mama ntilie, machinga na watumishi wa umma wa ngazi za chini.

Kwa kuwa hawasikii wameziba masikio Yao je watanzania wanyonge tupige magoti tumlilie Mungu wetu aje atuokoe?? Ili aibadilishe mioyo ya viongozi wetu isiwe migumu??.
Mungu ni kila kitu lakini sio kila kitu lazima utufanyie.

Kuna mambo mengi tu katupa uwezo wa kuyatenda na yakafanyika, kumbuka sisi pia ni mfano wa Mungu mwenyewe.

Hata yeye anatushangaa tunapomlilia hata kwa mambo tunayoyamudu tena kwa dhati. Anatuona wapumbavu na Ataamulu watawala watutese zaidi ili tupate akiri ya kujua yeye ni Mkuu na alishatupa uwezo wa kutatua Matatizo yetu mwenyewe bila kumhangaisha kwa issues ndogondogo.

Chukua Hatua. Nichukue Hatua.
Tuchukue Hatua.
 
Kuna muda tuongee na Mungu katika lugha rafiki kama baba,sio kulia lia tu mbele zake.
Nna jirani,anaomba kwa sauti kila asub akilia, huwa nawaza hamna siku aongee na Mungu kwa amani mpaka ampigie kelele?
Acha kuingilia imani za watu.
Kama umeshiba kalale au ukalewe.
 
Hali mbaya ya kiuchumi serikali haina options zenye akili , wako short sighted kimipango na top hana vision yoyote Kwa jambo lolote Bora liende. Hali ngumu sana
 
Mungu kajipambanua pasi kuacha shaka kabisa kuwa ni Mungu wa watu wenye akili,ujunzi,maarifa,ushujaa, uthubutu na wasio waoga,tuchukue mfano mdogo tu wa mashariki ya kati taifa la Israel limezungukwa na maadui lakini Israel inaendelea kuwepo mashariki ya kati kwa sababu wanajipambania ili wawepo na Mungu ndo anawasaidia kwenye mapambo yao ukiwagusa sehemu mbaya hawa kuachi Wala hawaingii kwenye mahekalu yao kuomba ujinga wa Mungu kuwaondolea maadui bali kuchukua siraha na kutembeza kichapo.

Hakuna Mungu wa watu wajinga,wanafiki, mazuzu, mazwazwa,wasio jitambua na kujielewa mfano nyie Watanzania hamna lolote zaidi ya kufaham Diamond anatembeza gari lisilo na plate number ndo mnafanya mjadara wa siku kwa akili hizi Mungu yupi mnao muamini nyie atawasaidia kutatua shida zenu ?

Viongozi Kama wakina mtwa mkwawa,mtemi mirambo nk walipo ona serikali ya kijerumani inaleta mambo ya ajabu ajabu walipigana kulinda heshima zao na nchi yao Cha ajabu ni vijana wa Sasa kulialia Oooh Mungu Oooooh Mungu ,Mungu gani huyu wa watu wajinga Kama nyie [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Mnazidiwa akili hata na bwana Kinjikitile aliye amua kuwa danganya watu kwamba risasi zitageuka maji lengo kuu ilikuwa kupambana na udhalimu wa serikali ya kijerumani,uzuri yeye maji alitoa bure nyie mnakwenda kununua maji kabisa kwa manabii uchwara ili upate mafanikio wakati huo huo huna shughuli yeyote ya kukuingizia kipato[emoji16][emoji16]

"Ama kweli zama hizi vijana ni wajinga kuliko wazee"

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
"JISAIDIE NAMI NITAKUSAIDIA"

tuache kulalama lalama kama vile mungu alitunyima akili, maarifa, mwendo, mikono nakadhalika,
Sisi watanzania ndio chanzo cha haya yoote, siku tukiamua basi hu ujinga utaisha.

Tofauti ya nzi na nyuki ni akili tu, siku nzi akiacha ujinga nae anaweza tengeneza asali.
 
Yaani tumsumbue Mungu kwa ujinga wetu? Alitusaidia mwaka jana Mwezi wa Tatu, kwa sasa tujisaidie wenyewe
 
Katika nchi yetu kuanzia juzi vilio vya makato ya miamala ya Kibenk vimetikisa nchi yetu. Kwa bahati mbaya kabisa wenye mamlaka wamekuwa wakitoa majibu ya kejeri na kiburi ndani yake.

Hawasikii Wala hawana uchungu dhidi ya mamilioni ya watanzania wanao ogelea katika dibwi la umasikini huku wao wakiendeshwa Kwenye magari mazuri yanayoendeshwa kwa Kila kitu yaani gharama zote hadi mafuta na mshahara wa dreva na fedha kutoka kwa mama ntilie, machinga na watumishi wa umma wa ngazi za chini.

Kwa kuwa hawasikii wameziba masikio Yao je watanzania wanyonge tupige magoti tumlilie Mungu wetu aje atuokoe?? Ili aibadilishe mioyo ya viongozi wetu isiwe migumu??.
Mi naona tuwaombee kifo,mauti yaje yawachukue mmoja baada ya mwingine. Mkubwa wao Hadi mdogo wao,ee mola wetu tunanyanyua mikono yenu kwako. Watawala wetu wamekuwa na kibri mno. Majivuno yamezidi,dhulma imekithiri. Ee mola wetu tutetee kutokana na dhulma hii bila kumwaga damu ya wananchi wanyonge wasio na hatia. Tubadilishie viongozi Hawa tuletee viongozi wengine wenye huruma na wasikivu. Ewe mola wetu tunakuomba utuondolee udhia huu,tunanyua mikono kuelekeza maombi yetu kwako tunakuomba utupokelee maombi yetu
 
Mi nadhani tukuombee wewe Ufe kabisa. Nyinyi ndio mnaofanya wote tuonekane Wapumbavu mbele za Mungu. Mkiisha watu wenye mitazamo kama nyinyi. Mambo yatarekebika.
 
Waislaer wana MUNGU wao mnamuita MUNGU wa Yakobo wa Isaka wa Ibrahimu lakini wanamgambo wa palestine wakijikuta na kurusha kombora hata moja upande wa Islaer hakuna cha eti waisaler wanaenda mlilia Mungu wao wanachofanya wanavulumisha makombora kama mvua upande wa Palestine hadi wapalestine wanarudi kumuomba Mungu awape huruma. Emu amkeni acheni kumchosha Mungu kingali nguvu amewapa na zipo kwenye mikono yenu. Linakuja zoezi kubwa hapo kesho kutwa. Fukuza mtu akija nyumbani kwako na takataka zake eti anataka sijui nini nini.
 
Back
Top Bottom