Watanzania tufunge na Kuomba tukimlilia Mungu?

Watanzania tufunge na Kuomba tukimlilia Mungu?

Mungu ni kila kitu lakini sio kila kitu lazima utufanyie.

Kuna mambo mengi tu katupa uwezo wa kuyatenda na yakafanyika, kumbuka sisi pia ni mfano wa Mungu mwenyewe.

Hata yeye anatushangaa tunapomlilia hata kwa mambo tunayoyamudu tena kwa dhati. Anatuona wapumbavu na Ataamulu watawala watutese zaidi ili tupate akiri ya kujua yeye ni Mkuu na alishatupa uwezo wa kutatua Matatizo yetu mwenyewe bila kumhangaisha kwa issues ndogondogo.

Chukua Hatua. Nichukue Hatua.
Tuchukue Hatua.

Tuchukue hatua zipi??
 
Tuchukue hatua zipi??
Za kusababisha tusilipe Tozo Au za kulipa Tozo. Maombi kwa Mungu hapa hayahusiki. Ni Tulipe au Tupaze Sauti na Vitendo ili kuishinkiza Serikali Tusilipe hizi Tozo za ziada.
 
Mi nadhani tukuombee wewe Ufe kabisa. Nyinyi ndio mnaofanya wote tuonekane Wapumbavu mbele za Mungu. Mkiisha watu wenye mitazamo kama nyinyi. Mambo yatarekebika.
Usinipangie namna ya kupambana na adui yangu kama umechagua kupambana Kwa kutumia mawe na adui aliyekushikia bunduki ni juu yako na ujasiri wako na utahira wako.
 
Inasikitisha sana
Hali mbaya ya kiuchumi serikali haina options zenye akili , wako short sighted kimipango na top hana vision yoyote Kwa jambo lolote Bora liende. Hali ngumu sana
 
Waislaer wana MUNGU wao mnamuita MUNGU wa Yakobo wa Isaka wa Ibrahimu lakini wanamgambo wa palestine wakijikuta na kurusha kombora hata moja upande wa Islaer hakuna cha eti waisaler wanaenda mlilia Mungu wao wanachofanya wanavulumisha makombora kama mvua upande wa Palestine hadi wapalestine wanarudi kumuomba Mungu awape huruma. Emu amkeni acheni kumchosha Mungu kingali nguvu amewapa na zipo kwenye mikono yenu. Linakuja zoezi kubwa hapo kesho kutwa. Fukuza mtu akija nyumbani kwako na takataka zake eti anataka sijui nini nini.
Leo hii ndo mnakumbuka hayo??Si mlifurahia Sana kuhusu mama kuwa top
 
Katika nchi yetu kuanzia juzi vilio vya makato ya miamala ya Kibenk vimetikisa nchi yetu. Kwa bahati mbaya kabisa wenye mamlaka wamekuwa wakitoa majibu ya kejeri na kiburi ndani yake.

Hawasikii Wala hawana uchungu dhidi ya mamilioni ya watanzania wanao ogelea katika dibwi la umasikini huku wao wakiendeshwa Kwenye magari mazuri yanayoendeshwa kwa Kila kitu yaani gharama zote hadi mafuta na mshahara wa dreva na fedha kutoka kwa mama ntilie, machinga na watumishi wa umma wa ngazi za chini.

Kwa kuwa hawasikii wameziba masikio Yao je watanzania wanyonge tupige magoti tumlilie Mungu wetu aje atuokoe?? Ili aibadilishe mioyo ya viongozi wetu isiwe migumu??.
Mungu sio nyie Chadomo au sukuma gang wa kusikiliza upuuzi wenu..

Omba basi tuone nani atapata kichapo Kati ya anaekusanya Kodi ya maendeleo na wewe unaeleta Uchawi.
 
Katika nchi yetu kuanzia juzi vilio vya makato ya miamala ya Kibenk vimetikisa nchi yetu. Kwa bahati mbaya kabisa wenye mamlaka wamekuwa wakitoa majibu ya kejeri na kiburi ndani yake.

Hawasikii Wala hawana uchungu dhidi ya mamilioni ya watanzania wanao ogelea katika dibwi la umasikini huku wao wakiendeshwa Kwenye magari mazuri yanayoendeshwa kwa Kila kitu yaani gharama zote hadi mafuta na mshahara wa dreva na fedha kutoka kwa mama ntilie, machinga na watumishi wa umma wa ngazi za chini.

Kwa kuwa hawasikii wameziba masikio Yao je watanzania wanyonge tupige magoti tumlilie Mungu wetu aje atuokoe?? Ili aibadilishe mioyo ya viongozi wetu isiwe migumu??.
Kuna mambo Mungu ana deal nayo, na mengine alituachia tumalizane nayo wenyewe.
 
Acha mabank ya ongeze gawio.

Kati kakipindi ambacho biashara zinadorora, marejesho kwa wakopaji yanasuasua , amana Nazo haziuziki, Huku gawio linasubiriwa, mnatehemea kifanyike Nini?
 
Huku vijijini watu wanaendelea kuona namna huduma za kijamii zilivyo na zinavyoendelea kuboreshwa kila siku, wanaendelea kumshukuru mh Rais namna anavyowajibika kutimiza majukumu yake yakugusa maisha yao, wanaendelea kufurahi kwa namna kero zao zinavyofanyiwa kazi na kutatuliwa kwa wakati

Wakulima kwa Sasa huku Ni kicheko na furaha baada ya mh Rais mama Samia suluhu Hassani kutoa Ruzuku, lakini pia wanafuraha kuona wakiuza kwa Bei nzuri mazao yao

Wewe unataka upige magoti halafu Nani asimame kikijengwa nchi yako, embu amka uungane na mamilioni ya watanzania walio bega kwa bega na mh Rais katika kuijenga Tanzania mpya
 
Daa Kuna jamaa nilikuwa simuwezi primary tukachonganishwa nikapata na mdhamini wa pambano akanipa bublish za rangi mbili nitafune Kwanza tukapigana nikashinda sikuamini

Uthubutu nikujaribu
Upige magoti ili iweje, hebu tuachege upuuzi! Haya ndio yamefanya mpaka tumefikia kufananishwa na maiti. Watanzania kila jambo mmekuwa watu wa kulia lia tu. Fanyeni action watu waone mnamaanisha. Maneno matupu na kulia lia mitandaoni ni dalili ya kuwa mmeshindwa na mnyanyasaji (bull) ataendelea kuwagandamiza hadi kifo.

Nakumbuka enzi zetu tukiwa za shule za awali kulikuwaga na tabia ya bulling sana toka kwa baadhi ya wenzetu ambao walijiona wakubwa na wababe ila uonevu ulipozidi mwisho wake ilikuwa ni kukata mzizi wa fitina kwa parling. Ile spirit tulikuwa nayo watoto wa zama zile ni ya kupinga uonevu bila kujali anaekuonea ana nguvu kiasi gani. Zitapigwa ngumi hadi kuvujishana damu kisha kuanzia hapo kila mmoja atamuheshimu mwenzie. Kuanzia kesho huwezi tena kuitwa majina ya kudhalilishwa, kila mtu atakutazama kama mwanaume kamili.

Uoga ukizidi sana huzaa udumavu wa kudumu wa akili na unyonge kutamalaki. Tukemee hii roho na tusimame imara kudai katiba mpya kwa nguvu na ujasiri itakayolinda haki na maslahi yetu.
 
Daa Kuna jamaa nilikuwa simuwezi primary tukachonganishwa nikapata na mdhamini wa pambano akanipa bublish za rangi mbili nitafune Kwanza tukapigana nikashinda sikuamini

Uthubutu nikujaribu
Kwa udhamini wa peremende 😂😂😂 ulimkalisha tembo. Ulijiskiaje toka siku hio? Alikusumbua tena?
 
Mwigulu kakosa ubunifu zaidi ya kuibia wananchi
IVI nyie vilaza mnajifanya mnaakili sana ivi kweli huyu Dr mwigulu ananguvu kiasi gani kufanya yote aya mbayo mnamtwika ivi hadi sasa hamjui mamlaka ipi inaidhinisha aya matozo badala kuilaumu serikali nyie kwa uvivu wenu mnamsema waziri kama mtu binafsi

Huu ni upungufu wa akili kabisa
 
Tulia wewe konda wake kwani yeye ni Waziri wa nini,nani anaeulizwa kuhusu pesa,hana ubunifu wa kupata pesa nje ya kodi,tozo na kukopa.
Mbona mkoloni hakutegemea kodi kuendesha nchi na alituletea maendeleo makubwa Sana nchini.
 
Upige magoti ili iweje, hebu tuachege upuuzi! Haya ndio yamefanya mpaka tumefikia kufananishwa na maiti. Watanzania kila jambo mmekuwa watu wa kulia lia tu. Fanyeni action watu waone mnamaanisha. Maneno matupu na kulia lia mitandaoni ni dalili ya kuwa mmeshindwa na mnyanyasaji (bull) ataendelea kuwagandamiza hadi kifo.

Nakumbuka enzi zetu tukiwa za shule za awali kulikuwaga na tabia ya bulling sana toka kwa baadhi ya wenzetu ambao walijiona wakubwa na wababe ila uonevu ulipozidi mwisho wake ilikuwa ni kukata mzizi wa fitina kwa parling. Ile spirit tulikuwa nayo watoto wa zama zile ni ya kupinga uonevu bila kujali anaekuonea ana nguvu kiasi gani. Zitapigwa ngumi hadi kuvujishana damu kisha kuanzia hapo kila mmoja atamuheshimu mwenzie. Kuanzia kesho huwezi tena kuitwa majina ya kudhalilishwa, kila mtu atakutazama kama mwanaume kamili.

Uoga ukizidi sana huzaa udumavu wa kudumu wa akili na unyonge kutamalaki. Tukemee hii roho na tusimame imara kudai katiba mpya kwa nguvu na ujasiri itakayolinda haki na maslahi yetu.
Extrovert kumbuka watu wakiomba na Mungu akajibu, basi hurekebisha kila kitu. Mi mpaka sasa naamini kwa 💯 ameshajibu ni suala la kuanza kuona vitu vinatokea. Haiwezekani nchi imejaliwa rasilimali kibao halafu unawaambia eti watanzania wahamie Burundi, eti yeye ni PhD wa uchumi, yaani ni aibu sana. Naongezea, Rais Samia kajitahidi kuiunganisha nchi na mataifa tajiri, tulitegemea wizara ya Fedha na Mipango ibuni vyanzo vya mapato toka kwenye rasilimali zetu badala ya kurudi kuwaongezea gharama za maisha watanzania ambao wanaonekana wapo Tanzania kwa bahati mbaya yaani wanawafukuza waende Burundi.
 
Extrovert kumbuka watu wakiomba na Mungu akajibu, basi hurekebisha kila kitu. Mi mpaka sasa naamini kwa 💯 ameshajibu ni suala la kuanza kuona vitu vinatokea. Haiwezekani nchi imejaliwa rasilimali kibao halafu unawaambia eti watanzania wahamie Burundi, eti yeye ni PhD wa uchumi, yaani ni aibu sana.
Mimi ni daktari wa uchumi, hampaswi kunitilia shaka, tozo ziko kisheria haziwezi kuondolewa asiyetaka anaweza kwenda Burundi ~ Lameki Tozo King
 
Back
Top Bottom