Watanzania tuige mfano wa Ujerumani, tunapaswa kumsahau Magufuli na kuweka bidii kusonga mbele

Tungemsahau kama Serikali ya Samia isingeyakumbatia majizi Sugu!! Yaani Mwigulu ni Waziri wa fedha kabsaa halafu tumsahau Mzalendo Magufuli? Makamba na Nape kabsaa!!! Haoana hapana lazima tutabaki na Magufuli katika mioyo yetu
Kuendelea kumkumbuka Magufuli na kumlinganisha Samia na Magufuli, kunatatua tatizo la kuwa na hao majizi katika serikali ya Samia?
 
Kipimo cha ubaya ni uzuri. Kwa mabaya kwenye uongozi wa Samia hakuna namna lazima tuyakumbuke mazuri ya Magufuli.

Kitendo tu cha huyu mama kuwauzia bandari na mbuga Waarabu ndo kaharibu big time. Kafanya mambo ambayo hata Rais dhaifu kuliko wote(jk) hakuyafanya. Muda utasema
 
Magufuli ni sehemu ya historia ya Tanzania. Huwezi kukwepa kumtaja.

Umpende, usimpende, ni historia.

Historia haikwepeki.
Hitler ni sehemu ya historia ya Germany. Anatajwa katika historia ya Germany, sio katika kuiendeleza Germany. Acha Magufuli awe historia pia, hilo sijakataa.
 
Uzalendo ni nini?

Unataka kuhalalisha ujinga wowote na kichaa chochote kwa kutumia mwamvuki wa uzalendo?

Ukibeti mali zote za taifa lenu kwenye odds mbaya sana za kushindwa kabisa ukazipoteza mali zote, unaweza kusema ume bet hivyo kwa sababu ya uzalendo?
 
Huyo mwamba hawezi kusahaulika aba dana. Watanzania wanampenda kwa kazi nzuri aliyoifanya kipindi cha uhai wake. Rip Jpm daima utabaki mioyoni mwetu.
 
Sasa hilo jambo ndilo tunapaswa kushughulikia, na it has nothing whatsoever to do with Magufuli. Huhitaji kumtaja Magufuli kutatua matatizo anayosababisha mama, kama umeweza kuyaona tayari
 
Hitler ni sehemu ya historia ya Germany. Anatajwa katika historia ya Germany, sio katika kuiendeleza Germany. Acha Magufuli awe historia pia, hilo sijakataa.
Kwanza kabisa, Hitler ni sehemu ya historia ya dunia, alitaka kutawala dunia, akaanzisha vita ya pili ya dunia, si historia ya Germany tu.

Pili, huwezi kutenganisha historia na maendeleo. Ili uendelee inabidi uijue historia yako uendeleze mazuri, usirudie mabaya.
 
Ukidhani kwamba kumtaja taja Magufuli kutamfanya Samia aogope na kurekebisha hayo mambo kwenye hiyo list, basi wewe ndio tatizo katika nchi hii, sio Raisi Samia kama unavyosema
Angalau angeweza kuiga utendaji wa mtangulizi wake hata kwa 40% tusingefika hapa tulipo
 
Angalau angeweza kuiga utendaji wa mtangulizi wake hata kwa 40% tusingefika hapa tulipo
Mpe viwango vya kupima utendaji wa kazi kama raisi bila kumtaja Magufuli halafu ndio um-judge kufaulu au kufeli kwake. Hilo haliwezekani?

Nilipokuwa UDSM, sikuambiwa ili ufaulu lazima uwe kama Palamagamba Kabudi, upate first class kama Prof. Kabudi. Sikuhitaji mtu anitajie Kabudi ili nifaulu mitihani yangu.
 
Kwanza kabisa, Hitler ni sehemu ya historia ya dunia, alitaka kutawala dunia, akaanzisha vita ya pili ya dunia, si historia ya Germany tu.
Magufuli pia alitaka kuiweka Tanzania katika top tena za dunia. Kuifanya donor country. Kumbuka malengo yake? Dar es Salaam iwe kama Ulaya.
 
Watanzannia wanapaswa kusahahu Utumwa mamboleo....

Uangamizaji wa Wamaasai

Uuzwahinwa Bandari n.k n.k

Itoshe Kusema, Tanzania haijawahi kuwa kama Nchi ya Kijerumani na J.P. Magufuli, Hayat Rais wa JMT hakuwahi kuwa Dikteta. Kwa lugha nyingine, aliyoyafanya Magufuli hayawezi kulinganishwa na yaliyofanywa na Hitler hata siku moja.

Mama yenu kauza Nchi kwa Wajomba.
 
Kuna kumsahu Magufuli, na kusahu historia. Hakuna mahali nimesema tusahau historia ya Tanzania. Usichanganye haya mambo mawili.
 
Umefananisha Simba na Nyani.

Mifano yako Haina uhusiano sawa.

JPM awe kama Hitler kweli? Au unahadithi za vijiweni?
Unafananisha sura au philosophy? Mie niko kwenye mentality, na usije ukaniambia mbona Magufuli hakuanzisha gari kama Hitler. Nitakuambia nenda shule kasome.
 
Sasa hilo jambo ndilo tunapaswa kushughulikia, na it has nothing whatsoever to do with Magufuli. Huhitaji kumtaja Magufuli kutatua matatizo anayosababisha mama, kama umeweza kuyaona tayari
Mkuu,

Mimi huwa napenda kufanya "immanent critique". Yani kupinga kwa kuanza kukubaliana nawe, hata pale ambapo sikubaliani nawe, ili kuonesha ukubwa wa makosa yako, hata kama nataka kukubaliana nawe. Kuonesha internal contradictions katika hoja zako hata kama nataka kuanza kukubaliana nawe.

Hata kama nataka kukubaliana nawe kwamba Magufuli alikuwa rais mzuri (kitu ambacho sikubaliani nacho), Magufuli ali fail kuweka mabadiliko ya kimsingi ma kimfumo kuzuia mabaya anayoyafanya Samia.

Magufuli ndiye aliyesisitiza ukubwa wa Rais na kuponda utawala wa sheria.

Hata pale alipofanya marekebisho ya sheria kuweka ulinzi wa rasikimali za kitaifa kishwria, hakuondoa mfumo wa rais mwenye nguvu sana na uchawa uliosababisha Samia aweze kurudi bungeni na kutengua sheria hizo.

Tena Magufuli alikuwa anasema kabisa kwamba inawezekana rais anayekuja akaharibu mambo, lakininas long as yeye ni rais hatakubali mambo yaharibike. Hiyo ni kauki ya rais ambaye amekubali kuwa hawezi kuweka mfumo endelevu. Rais asiyeele2a kuwa urais ni taasisi na si mtu mmoja.

Hilo ni tatizo, hata kwa anayekubali mazuri ya Magufuli niblazima aone kuwa Magufuli hakuwa broad minded enough kuweka mabadiliko ya kimfumo, alikuwa anacheza na akiki za watu tu kufanya maigizo ya mabadiliko wakati kwenye mambo ya msingibkama katiba mpya kakataa mabadiliko.

Na ikiwa kuna mambo ya kimsingi Rais akikosea anakuwa si Rais mzuri, na hili la kujenga mambo endelevu ni miongoni mwa hayo, basi Rais Magufuli hawezi kuepuka lawama kwenye madudu yanayoendelea leo.
 
Wakitaka Magufuli asahaulike;

1. Wahakikishe wanachukia RUSHWA!!

2. Wahakikishe wanawahurumia wananchi wa kipato Cha chini.

3. Wahakikishe maoni ya wananchi yanasikilizwa.

4. Wahakikishe pesa za umma hazicheziwi Wala kuibwa, na miradi ikamilike Kwa wakati.

Hapo atasahaulika, tofauti na hapo, KITI hicho hakitakalika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…