Sidhani kama kuna Mtanzania ambae hajui mazuri ya Magufuli akiwa raisi wa Tanzania, atapinga kwamba Magufuli hakuwa na roho ya uzalendo kwa Tanzania, alichukia ufisadi, alichukia watu ambao anawaona walikwamisha bidii zake za kuindeleza Tanzania. Hakuna Mtazania atakaepinga kwamba Magufuli alikuwa mchapa kazi kweli kweli, mwenye kupenda nchi yake na raia wa Tanzania, mzalendo namba moja.
Lakini hilo linakukumbusha nini?
Linatukumbusha kiongozi aliewahi kuwa na hulka ya Magufuli pale Germany, Adolf Hitler. Hitler alikuwa mzalendo kweli kweli. Alisimamia Germany na kuifanya Germany kuwa taifa lenye uchumi wenye nguvu kuliko mataifa yote. Alipenda uzalendo, alichukia ufisadi na usaliti dhidi ya nchi yake. Hitler alikuwa muasisi wa gari za VW, Volks Wagen (People's Car) ili kila raia wa Germany aweze kumudu kuwa na gari. Hakuna kiongozi katika Germany anaeweza kusemwa alileta maendeleo kwa nchi yake kama alivyofanya Hitler, mzalendo namba moja wa nchi yake.
Lakini sasa, nani leo unamsikia akimsifia Hitler kwa makubwa aliyoifanyia Germany? Hakuna, kwa sababu hakuna mtu aliyesahau machungu yaliyosababishwa na Hitler.
Hakuna mtu hapa Tanzania asiyejua machungu yaliyoletwa na Magufuli katika azma yake ya kuiendeleza Tanzania, machungu ambayo hayana utetezi hata uyaangalie kwa mtazamo upi. Hayana justification.
Hata hivyo, kwa tulio hai, kuwachukia Hitler au Magufuli, ambao tayari wamekufa, ni dalili kwamba tuna matatizo ya afya ya akili, tunahitaji psychiatric help. Kuwasifia pia ni tatizo, kwa sababu tunaumiza wale walioumizwa nao, ambao bado wapo hai pamoja nasi. Tutapanda gari za VW za Hitler, tutapita kwenye flyover za Magufuli, lakini hatutaimba sifa zao.
Kama Germany ilivyoamua kumsahau Hitler pamoja na mazuri aliyoifanyia nchi yake, Tanzania tunapaswa kumsahau Magufuli pamoja na mazuri aliyoifanyia nchi yetu.
Tuangalie mbele sasa. Tusahau yaliyopita, tuachane na kulinganisha uongozi wa sasa na uliopita. Tuvunje magenge. Tuanze upya.
The world and your country need YOU now, not Hitler, not Magufuli.
Human being don't understand logic, reasons, mouth narration but how you touch them instinctively and our own intuition make us to understand what are you doing to us.
Don't try to control nature my friend.
Kwani wakiwa wanamsifia wanakuja kukuambia ama kila wanaloongea wajerumani hata saivi mtu yupo ndani na beibi wake wanakulana wanaongea about their hero basi unanasa sauti zao .
Pia miaka mingapi imepita tokea Hitler afariki.
Kama kuua mbona Kama mafisadi ndio wanaoua kuliko anayeua anayemuingilia anayejenga Taifa lake.
Ama nikuambie mafisadi wanavyoua na Tena wanaua wengi taratibu mno na kwa muda mrefu sema ni indirect huwezi ona na ndio Mana huko china mla rushwa bro anauliwa na sahihi kabisa auliwe yaani angekuwa anakatwa kwanza kiungo kimoja kimoja mpaka afe.
Sema Sheria za nchi hii kama Kuna mtu mmoja anaamua kuwa ziwe anavyopenda anavyoona kuwa zitambeba. Hivi tukisema kila mwenye Mali aonyeshe alivyozipata na alilipia wapi mapato na kipato chake aliwezaje kuwekeza Mali ikakua ndio ujue watu wanakula jasho la watu na wao wanakufa ama wanauliwa wanaporwa jasho lako.
Mafisadi na viongozi wote Wanaojua kuwa wameuza Mali za watanzania kwa manufaa yao Bali sio Tanzania wanawauaje watanzania zaidi kuliko ambao wameuliwa na jpm ama Hitler.
1- Tafuta data za wamama wajazito waliojifungua huko vijijini wakakosa dawa, huduma nzuri ya dawa na kidaktari Mana dawa zinapigwa/hazinunuliwi na madaktari hawawekewi mazingira rafiki wao wakae huko ili wawahudumie walipa Kodi. Tafuta vijiji vyote Tanzania ujue ni wangapi wanaofariki wakati wa kujifungua ndio uje kuongea ujanja wako hapa
2- Tafuta ni akina mama wangapi wanaofariki njiani wakipelekwa hospital kubwa Ila hakuna ambulance, zinaharibika njiani kisa roads mbaya. Tafuta ujue data zao na sio kuleta mambo Kama ushabiki tu ama huna kazi sema hujui tu Hawa mafisadi na baadhi ya vizee vilivyotuuzia nchi yetu.
3- Tafuta walimu wa physics and mathematics ratio to students iko ngapi kwa shule nzima Tanzania. Watoto wapo alfu mbili mwalimu mmoja wa maths na physics hakuna na hili suala ni la mzungu ama tubinafsishe.
Watoto wanaofeli kisa hakuna walimu wazuri baadaye Hawa watt wanaishia kuwa wadangaji, Malaya, vibaka, vibarua, Wala dawa za kulevya ili kupunguza machungu ya maisha yao, watt wanapata magonjwa na mimba Mana maisha hata ya kusoma sio rafiki kwao wangesoma angalau akapambana akawa nesi, mwalimu, nk.
Tafuta ujue haya madhara mpaka kifo vijana wanaanza kuwa vibaka Mana maisha ni makali shule hakuna , vibarua hakuna shule wanafeli Mana walimu hawapo , vitabu na mazingira mazuri ya masomo ya maabara .
3-Tafuta namba ujue ni watu wangapi vifaa ama Mali zao ama biashara zao zinaharibika kisa Kuna umeme wa kifurushi. Vijana wanashindwa kujiajiri huko vijijini kisa umeme wa uhakika na ndio Mana jpm aka African Hitler alitaka umeme wa uhakika saivi bwawa limewashinda maji yamefunguliwa yameua watu 35 huko rufiji haya sio mauaji ya binadamu Kama huyo mmewe aliyeuwa. Nikuulize ivi kweli jpm angekuwepo haya mauaji yangetokea huko rufiji. Uelewe watu wameshapiga zao mradi sio Kama enzi za marehemu. Unajua ni kiasi gani dizaini imechenji hata kwa sgr mahala palipotakiwa pawekwe nguzo kisa Kuna mkondo mkubwa wa maji saivi wanajaza kifusi mlima na huku ilitakiwa nguzo za zege train ipite juu.
4- Unajua ni vijana wangapi hawapati ajira kisa tu hawana mtu kwenye system wa wakulima wanabakia wengine kubeba unga ama kuwa wadangaji na kufanya kazi ambazo ni risk kwao unajua ni wangapi hapa wanaokufa.
5- Unajua wakulima wangapi wanashindwa kusafirisha mazao yao kisa tu barabara mbovu yanaozea shambani.
Naweza nikaendelea na list ni ndefu
Ngoja kwanza nisaini hapa mktaba wa bilioni 75 tukodi software ya kunijuza umeme Kama umekatika kutoka India. Yaani hii Ni hela tu ya kukodi software huko tanesco waza ni wanafunzi wangapi wanakaa chini na wapo madarasa ya udongo ambao wanaweza wakaangukiwa .
Kuna shule hapa hapa mwanza mjini watoto wanakaa chini, hakuna Hitler wa kuweza kutoa sauti kuwa watoto wasikae chinim darasa moja watoto Mia moja unaona haya ndio Yana akili.
Haya bana ulitaka demokrasia umeipata Mana Simba wa yuda hayupo saivi hakuna uwoga. Hamjamaliza kusafisha mitambo Mana ilikuwa inawaka ikiwa mibovu watu waliogopa kutumbuliwa.
Ngoja nipige tour kucheki mito ikoje na kina chake na helicopter baadaye nijiandikie pdm na hela ya kukodi helicopter ni ndefu Bora ingenunua dawa.
Sawa mvua zimesnyesha zimeharibu mitambo.
Treni ya moro to dar sgr inasubiria Nini ama tuna refurbish vichwa ili tupige Cha juu. Kumpa mtu uongozi mwenye kuwaza chakula na ni masikini Ni sawa na kumpa Bora mzungu na Ni Bora apewe masikini ambaye ana Nia ya kuinyanyua nchi like sokoine, NYERERE ama Mandela. Unadhani hao akina NYERERE angekuwa Kama huyo mjanja wenu unadhani mngekuwaje