Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

Kuna vitu Watanzania hatuwezi na tunashindwa sio kwasababu ni vilaza, au hatuna uwezo, tunashindwa kwasababu tuu hatujui kutazama mbali!
Kama alivyo tazama Simon Mwanza Kapwepwe (R.I.P) ?
Ambaye alisema, na nukuu" If we won't handle our independence carefully colonisers will come back in the name of investors" mwisho wa kunukuu.

Ukiwa na njaa huwezi kuwa mwandishi mkweli
Fani ya uandishi wa habari ni moja ya noble professional, ni kazi ya wito kama ualimu, tunafanya kwa mapenzi tuu na sio kwa mapato, hivyo ni kweli uandishi wa habari ni kazi ya kimasikini na mara kibao sisi waandishi tunalala na njaa, ila tuko kama Kozi, mwana mandanda, kulala njaa kupenda, na bado tunaandika ukweli kama bandiko hili.
P
 
Pascal, ukiabdikaga bandiko lililonyooka huwa hatukusifii?

Uturuhusu pia tukukosoe tunapohisi kuwa umepotoka.

Kwa aina ya uandishi unaoandika kuhusu DPW unastahili kupewa hati ya mashaka.

Ikiwa unaandika makala yenye mizania ya kuuchimba ukweli...huwezi kuanza na neno...PUUZIENI...

Mimi sio mwandishi wa habari lakini hii ina harufu ya "samaki"

Rudi relini iwapo ulipotoka...hujachelewa.
 
Bwana Mayala nini tunachokiweza iwe mfano kwa wenzetu, kama wao walivyomfano kwetu ? Toa mfano wa jambo moja ambalo ni mfano wa kuigwa.
Je huoni chama kinachotawala ndio kimeshindwa na si watanzania wote? Kwa nini ujumuishe tumeshindwa wakatii huo wapo watu hawahahusiki na kushindwa kwako?
Kwa nini usikae pembeni uwaache wengine watumie karama zao?
Hapa namaanisha kukaa pembeni iwe ndani ya ccm au nje ya ccm, wapewe nafasi wengine wafanye mabadiriko.
Mfano 2025 wabunge wote na mawaziri waliopo ndani ya ccm wapishe waingie wengine au ccm ipishe kiingie chama kingine.
Halafu suala la uraisi kuwa ni chaguo la mungu unaeeza kututhibitishia hio kauli hio.
Sina kadi chama chochote, hivyo unijibu kama mtu huru bila kujali ukada wako.
 
Wakili Msomi Paskali!

Hongera sana!

Andiko lako ni Magnificent kaka!

Bandari me naona wanatuchelewesha tu ingeanza tangu juzi!

Ni kweli kabisa kwamba Mpango wa SGR ni mzuri mnooo lakini kwenye Uendeshaji tutanasa!

Hapa tunahitaji Programming na TEHAMA first class!

Huo uwezo hatuna kaka!

Kwenye Ndege...zile Air Bus ziko wrong planned.

Huwezi kurusha Ndege ya Masafa Marefu kwenye masafa Mafupi na ukabaki salama!

Hiyo ni sawa na Kuendesha Scania kutoka Dodoma mpk Dar kwa kutumia Gear Namba Moja tu!

Block ya Engine itapasuka!!

Ndicho kinachotokea kwenye ATC!

Nadhani Andiko lako litatusaidia sana!

Pongezi nyingi!!!

Mwenye masikio....na asikie
 
Mkuu ChoiceVariable , asante kwa bandiko hili, Rais Samia Awaambia TRC/Wizara ya Uchukuzi "Nimechoka na Vijisababu,SGR Dar-Dom Lazima Ianze Kabla ya July 2024.", hili la ya GSR, kina sisi tumelisema sana, Reli ya SGR: Je, Tujifunze kwa wenzetu Kenya kuepusha SGR yetu kuwa β€˜A White Elephant’? Wenzetu yameshawakuta... sio tunajidharau, bali tunamatatizo makubwa ya upangaji vipaumbele vyetu, kama watu hawa wameshindwa kuendesha a simple meter gauge railway to its full capacity, what do you expect kwenye complex SGR?!.

Wakati tunabinafshisha Bandari yetu kwa DPW, nilisema humu Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie? kisha nikaandika Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?

Happy New Year!
P
 
Pascal, ukiabdikaga bandiko lililonyooka huwa hatukusifii?
Mkuu Colgate3 , kwanza asante kuchangia bandiko hili na samahani kuchelewa kujibu, hili bandiko ndio naliona leo.
Uturuhusu pia tukukosoe tunapohisi kuwa umepotoka.
Rukhsa kabisa mimi kukosolewa
Kwa aina ya uandishi unaoandika kuhusu DPW unastahili kupewa hati ya mashaka.
Nitakushukuru sana kama utaniambia mashitaka yangu kwenye issue ya DPW na Bandari zetu.
Ikiwa unaandika makala yenye mizania ya kuuchimba ukweli...huwezi kuanza na neno...PUUZIENI...
Hapa naomba nifafanulie
Mimi sio mwandishi wa habari lakini hii ina harufu ya "samaki"
Kuna wengi sio waandishi lakini wana jicho zuri na uwezo mkubwa kuliko waandishi, nitakushukuru kama utaninusisha hiyo harufu na mimi niisikie
Rudi relini iwapo ulipotoka...hujachelewa.
Asante sana kwa ushauri, nitauzingatia.
Happy New Year!
P
 
Samia ana hulka moja ya unyenyekevu anajua kwamba hajui kila kitu na anahitaji siku zote kufahamishwa na anajua anahitaji kufanya kazi na wajuzi zaidi yake. Hiyo ni hulka ambayo marehemu JPM hakuwa nayo.

DP World sio mwendeshaji wa mwisho kuja na ni kwa faida za kiuchumi za nchi hii, bandari inakwenda kuwa na waendeshaji watatu kwa maana ya kuwepo mwingine wa magati namba nane mpaka kumi na moja.

Kuna sekta tupende tukatae, zinahitaji makampuni ya kigeni yenye maarifa ili haya ya kwetu yaweze kuchangamshwa.

Hata sekta ya nishati inahitaji sana waendeshaji wengine wanaokwenda kupambana na TANESCO ili urasimu na upigaji uweze kushindwa kabisa.
 
Bwana Mayala nini tunachokiweza iwe mfano kwa wenzetu, kama wao walivyomfano kwetu ? Toa mfano wa jambo moja ambalo ni mfano wa kuigwa.
Mkuu Tangantika ,kwanza asante kuchangia bandiko hili na samahani kuchelewa kujibu, hili bandiko ndio naliona leo. Kuna vitu vingi Tanzania tunaweza na ni mfano, mfano, uhuru, umoja, upendo, amani na mshikamano. Tanzania ni kisiwa cha amani.
Je huoni chama kinachotawala ndio kimeshindwa na si watanzania wote?
Kwa vile hakijiweki, kinawekwa na sisi Watanzania wote, kikishindwa ni tumeshindwa wote under a collective responsibility clause.
Kwa nini ujumuishe tumeshindwa wakatii huo wapo watu hawahahusiki na kushindwa kwako?
A collective responsibility clause inajumuisha wote, hata kauli collective kama "Tanzania ni nchi masikini, applies kwa Watanzania wote including matajiri kama Bhakhresa.
Kwa nini usikae pembeni uwaache wengine watumie karama zao?
Hili neno!, na ndio essence ya uzi huu, kuna vitu hatuwezi, tukubali hatuwezi, tukubali kusaidiwa.
Hapa namaanisha kukaa pembeni iwe ndani ya ccm au nje ya ccm, wapewe nafasi wengine wafanye mabadiriko.
Hili neno!
Mfano 2025 wabunge wote na mawaziri waliopo ndani ya ccm wapishe waingie wengine au ccm ipishe kiingie chama kingine.
Hili pia neno, ila tatizo ni chama gani chenye uwezo gani?.
Halafu suala la uraisi kuwa ni chaguo la mungu unaeeza kututhibitishia hio kauli hio.
Uthibitisho ni sala ya kuanza kikao cha Bunge kuwa "Mungu ndiye huweka serikali za mataifa.
Sina kadi chama chochote, hivyo unijibu kama mtu huru bila kujali ukada wako.
Niliingia CCM 1987 nikiwa JKT Makotupora kwa mujibu wa sheria, siku zote, japo mimi ni kada, ni kada very objective kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, hivyo hata chama changu kinapotukosea Watanzania, tunakipiga spana!.
Happy New Year!
P
 
Samia ana hulka moja ya unyenyekevu anajua kwamba hajui kila kitu na anahitaji siku zote kufahamishwa na anajua anahitaji kufanya kazi na wajuzi zaidi yake. Hiyo ni hulka ambayo marehemu JPM hakuwa nayo.
Mkuu Steven Joel Ntamusano , kwanza Happy New Year !, kiukweli siku zote naipenda sana objectivity yako.
DP World sio mwendeshaji wa mwisho kuja na ni kwa faida za kiuchumi za nchi hii, bandari inakwenda kuwa na waendeshaji watatu kwa maana ya kuwepo mwingine wa magati namba nane mpaka kumi na moja.
Asante sana for this
Kuna sekta tupende tukatae, zinahitaji makampuni ya kigeni yenye maarifa ili haya ya kwetu yaweze kuchangamshwa.
naungana na wewe ila hayo makampuni ya kigeni yatujengee uwezo wa ndani, mkataba ukiisha, tunaendesha wenyewe.
Hata sekta ya nishati inahitaji sana waendeshaji wengine wanaokwenda kupambana na TANESCO ili urasimu na upigaji uweze kushindwa kabisa.
Naunga mkono hoja,

P
 
Tunashindwa au tunahujumiwa kirahisi kwa kuongozwa na vilaza au watu fisadi waroho wenye njaa kali.πŸ˜‚πŸ€£.
...Iko hivi
1: Vigogo wanataka kandarasi miundombinu na kadhalika kwa lengo kuu wapige cha juu na/au kupewa rushwa.
2: Wakigeuga wanakuta wamewekeza cha juu zao na rushwa kwenye malori mabasi etc kwa hivyo lazima wahujumu vya umma kuepa ushindani hadi wanapendekeza wabinafsishiwe uwekezaji wa umma kwa bei kama bure.
Ni ufisadi tu ndio shida, na ndio maana umma wa wananchi wanataka uongozi wa kijpm na wamelia sana kumpoteza mzalendo John Pombe Magufuli. Hadi tupate magufuli mpya ndio nchi tutaweza kwenda mbele tena. Hakuna tusiloliweza ila nchi tunaacha inaongozwa na genge la fisadi. 2025 lazima tuamke.
 
Tanganyika ilikufa mwaka 1962 tulipoua UPINZANI kwa kufuta VYAMA VINGI kwa madai ya KUJENGA NCHI kumbe ilikuwa ni KUJENGA CHAMA na kuendeshwa na mawazo ya mtu moko ambaye hakupenda MIGONGANO YA KIMAWAZO na CHANGAMOTO kwenye UTAWALA..

HAYA YOOOTE NI MATOKEO TU... LEO USIPOKIWA MFUASI KIITIKADI BASI KIMFUMO...

WATU WAPO KULINDANA KWA KIVULI CHA U-CHAMA....NA CHIPUKIZI NAO HAOOOOO NJIAINI πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
You said it πŸ‘‡πŸ‘‡
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…