Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

Ndugu yangu Mayala, sasa wewe unayejua huo mkataba ni wa muda gani? Nataka kujua ili pindi tutakapokua na uwezo tuiendeshe wenyewe. Pale Bandarini tuliitaji wakurugenzi na mameneja kutoka nje ya nchi ili tujifunze. Sisi tunawaza kupiga tu au kutenda kazi kwa kuogopana hilo ndiyo tatizo letu. Tungefanya utafiti wa haya mambo tungekuwa na majawabu yake. Nchi nyingi na makapuni wanatumia watu wa nje kwa sababu tofauti. Kwa mfano sisi tunaweza kuwatumia utawala wa nje kuondoa kuibiwa hovyo na wanaojifanya wazalendo wa nchi hii.
 

Binafsi naamini serikali yetu inaweza jiendesha na ina watu wenye uwezo mkubwa sana.
Tatizo ni kwamba wanaopewa mamlaka au wanaonunua madaraka wanawanyima wenye uwezo wa kufanya maamuzi na kuchambua mawazo nafasi na ni kwa makusudi kabisa.
Wewe Kama mzalendo fanya kufuatilia mikataba ya DP then ndo uje kuitetea serikali yako.
Ifike mahali watu muache kuwaza na matumbo.
 
Na wengi hawajapata nafasi ila ni waizi
 
Wengi tunamhukumu mwandishi lkn nafkiri hatujasoma bandiko hili vizuri, naungana na Pascal moja kwa moja. Kama nchi tungeweza fanya wenyewe lkn tuna mifumo thabiti ya kusimamia taasisi hizi? Tuna vyombo Kama TAKUKURU, TISS, hata mahakama je ni independent? Mentality za watanzania wengi ni upigaji tu na akionekana mtu anafanya kwa uaminifu basi kila mtu atamshangaa, hapa ndipo tulipofikia. Bandari ibinafsishwe tu bwana ila utaratibu uzingatiwe. Tumechoka na utendaji duni wa baadhi ya taasisi za serikali ikiwemo bandari, mpaka Kagame enzi hizo aliona tatizo pahala.
 
Mzee Bams umeibukia huku? Kwa hiyo unakubaliana na Paskali kwamba Bandari ya Dar wapewe Waarabu wa DP World bila zabuni ya wazi? Hiyo Mou kati ya Serikali na DP World ipo wapi? Kwanini haiwekwi wazi?
Hapana. Sikubaliani naye hata kidogo. Ni ujinga wetu ndio unaofanya rasilimali zetu kutapanywa na kunyofolewa hovyo.

Tumepewa rasilimali nyingi. Mungu wetu amefanya kazi kubwa kwa Taifa letu ila sisi hatujafanya chochote cha maana ndiyo maana vilivyotakiwa kutusaidia, vinaenda kuwanufaisha wageni.

Wabunge wanapelekwa Dubai, wanahongwa pesa na magari ya kifahari, wanarudi, wanaendelea kuwa wabunge, na watu wa majimboni kwao wanaendelea kuwashangilia!! Hapo kweli tuna wananchi wenye akili?

Tunasema kuwa tupiganie katiba mpya, tupate katiba inayompa nguvu mwananchi kuwawajibisha viongozi, jitu tena lina degree, na wakati fulani hata degree 2, utalisikia linasema, wananchi hawahitaji katiba mpya, wanataka maji na barabara, na majitu mengine yanampigia makofi!! Kweli majitu kama hayo yana akili? Lakini utashangaa jitu kama hilo linapongezwa na kupigiwa makofi eti limeongea jambo la maana.

Tungekuwa na katiba nzuri, wale wabunge wote 10 waliohongwa na mwarabu, sahizi wasingekuwa bungeni, wangekuwa wanahojiwa huko na vyombo husika.
 
Tatizo wewe na hao wanaofanya maamuzi wanahisi mnamawazo bora, yaani nyinyi mnajua sana kuliko raia, nyinyi mmesoma sana na kuijua vizuri dunia.

Ukiona wewe huwezi; usihisi kila mtu awezi kama ulivyoshindwa wewe.

Tokeni madarakani.
Kina msukuma et ndo wanatoa mawazo kwajil ya taifa. Wameshndwa wao simple achia madaraka tu
 
Wala hatubishi kwamba watanzani tumeshindwa kusimamia mali za umma kwa sababu ya wizi na kulindana hilo wala halina ubishi

Lakini pia wala hatukatai kusaidiwa wala hatuna hoja kwenye hilo kwa sababu ni kweli kabisa tanzania tumeshindwa kabisa kusimamiana na kuwajibishana

Lakini hoja ya msingi ni aina ya kusaidiwa na mikatabana ya hao wanao taka kutusaidia hapo ndipo kwenyw shida na ndipo panapo lalamikiwa
 
Pride ya ujinga ya kujaza umasikini, Wacha watu waendeshe vijana wapate ajira na Uchumi ukue
 
Mkuu
Una kazi kubwa sana ya kuwaelimisha hawa wanyika
Kuna wale wa zamani wa UPE na mawazo mgando
Ila sasa hivi kuna kundi kubwa la wajinga kupita maelezo katika hizi zama zetu
Kila la heri...
 
P
Yapi maoni yako kuhusu DP World?
Au na wewe umeshalambishwa bahasha?
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Karibu sana.
Kwanza nilianzia hapa, Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

ikaja kuwaomba waheshimiwa wabunge wetu, kwenye kuridhia IGA ya DPW, watangulize mbele maslahi ya taifa Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!.

Na baada ya Bunge letu Tukufu kuridhia mkataba huo bila kufanya due diligence yoyote kumhusu Mwarabu wa Dubai na hadhi ya mkataba wenyewe, kwanza nikasisitiza kuunga mkono hoja, Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?.

Kisha nikahoji uwezo wa Bunge letu na uwezo wa wabunge wetu kujadili jambo kubwa kama hili Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu? .

Pia nikatoa angalizo la maeneo yenye ukakasi ili HGA iwe imenyooka Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! na kesho Jumapili, nitaandika makala kwenye gazeti la Nipashe kuhusu huu mkataba
P
 
Wazenji huwa hawajiamini ni hadi wamuweke mtu mweupe mweupe mbele, wameedhirika na historia ya utumwa.

Mfano mwarabu hakai foleni zenji.
Kwenye kikao atatafutwa mwarabu japo teja akae meza ya mbele hata kama hajui aseme nini.
Kazi yoyote hawajiamini hadi wafanyiwe na mweupe (mwarabu au muhindi).

Wazenji hawajui kuiba, hubeba vyote mchana peupeee😂😂😂
 
Lakini wewe hujakubali kuwa mkeo amekushinda ukatupatia sisi wadau tuishi naye. Why? Uzalendo uanzie kwenye mambo madogo. Nyie motivational speakers huwa mnajichanganya padogo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…