Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Kwanza napenda kupongeza taarifa iliyotolewa leo baada ya majadiliano ya karibia miezi miwili na Barrick. Tumepata tulichopata na makubaliano mengine ambayo itabidi tusubiri kuona faida yake huko mbeleni. Nirejee kwenye mada, wote tunajua mwaka jana tuligomea msaada wa MCC wa dola 450m za bure kwa sababu hatukutaka msaada wa masharti. Ni kweli pesa zile tulizokosa kwa kushindwa tu kutumia busara ya kidiplomasia kwa makosa yetu ya kudharau demokrasia. Kwa bahati siku nazo hazigandi. Tukapata tume mbili zilizoshiba uzalendo zikachunguza wizi wa madini yetu hasa dhahabu. Tume zikafanya kazi kwa uzalendo kabisa na kutuletea data zisizoacha shaka kwa wizi tuliofanyiwa. Taasisi yetu ya mapato ikakokotoa wizi tuliofanyiwa ikakuta tunadai $190b zisizoacha shaka.
Leo hii wengine tunaukumbuka baadhi ya mambo tumepigwa na butwaa kwa kusikia mazungumzo ya wezi wetu wa Barrick yamefikia mwisho mwisho, lakini ni kama maamuzi halisi yameshatolewa. Maamuzi hayo ni pale mwizi wetu alipoona stahili yetu ni $300m tena za uaminifu kwamba yeye sio mwizi, na hizo atazitoa baada ya bodi yao huko London kuridhia! Watanzania tukalipuka kwa shangwe kwamba mwizi kanyoosha mikono. Wengine sisi tukaamua kwenda mbali zaidi na kujiuliza, iweje mwaka tu ulioisha tugomee $450m za bure kisha tuheshimu demokrasia, lakini tukubali $300m toka kwa mwizi tuliye na ushahidi nao mwaka mmoja mbele? Hapa hatunyoosheani vidole, lakini watanzania na waliochukua maamuzi hayo wametumia busara? Je hali hii ya kushindwa kupokea hela za bure kisha tuheshimu demokrasia na kupokea $300m toka kwa mwizi ipi ni maamuzi ya busara? Mawazo yoyote ni sawa kwani hii ndio demokrasia
CC: Paskali Mayalla, Quinine, Yehodaya, Jingalao, Mwigulu Nchemba, Zitto Junior