tindo bwana mbona unafananisha vile vijisenti vya MCC na hili gharika la ushindi alioupata Magufuli?
Ile hela ya MCC ilikuja na masharti kuwa
* tufute sheria zetu za makosa ya mitandao,
* tubatilishe maamuzi ya Jecha katika ule uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.
Serikali yetu ikawapa MCC the middle finger na kuwaambia, kama ni huo msaada wenu ndio unaomipa jeuri ya kutuingilia tunavyoendesha nchi yetu, (basically kutupokonya sovereignty yetu) basi msitupe.
Hiki ni kitendo cha kijasiri na kujivunia. Watanzania wote tunapaswa kutembea vichwa juu na vifua mbele kwa uamuzi ule.
Kuhusu makubaliano ya serikali na Barrick yaliyotangazwa, kama sikosei ni hivi:
☆ $300m za kutuangukia kwa usumbufu waliotupa.
☆ Tunamiliki 16% ya machimbo
☆ Mgao wa faida ni 50-50 kati ya wachimbaji na serikali.
☆ Mapato ya haya makampuni yatawekwa kwenye mabenki ya ndani.
☆ Watakachochimba zaidi ya dhahabu, shaba na fedha yote itakuwa ni mali ya serikali.
☆ Watawaajiri Watanzania na kuwafunza taaluma za juu za uendeshaji migodi.
☆ Watahamisha ofisi zao kuu kutoka Afrika Kusini na Uingereza na kuzileta Tanzania.
☆ Nafikiri kuna vingine nilivyovisahau.
Mkuu unataka kufananisha zile $450m za masimango na mpukuti huu tunaoupata kwa makubaliano haya?
Pia ukumbuke kuwa, kuanzia sasa makubaliano yote yatakayofanyika kati ya wanaotaka kuchimba madini Tanzania na serikali yatafuata precedence hii.
Hebu piga makofi kidogo umpongeze Rais wako.