Magonjwa Mtambuka
JF-Expert Member
- Aug 2, 2016
- 32,246
- 31,176
Lowasa muadilifu yupo. Tuendelee kuzungusha mikono.Mtaelewa tu..c ndo watawala wenu...me ngoja nitafute ugali wangu...
NOTE:: LAKIN AKIPATIKANA MTAWALA MZALENDO NA MUADILIFU. MSIACHE NITAARIFU NIMSAPORT....
tindo bwana mbona unafananisha vile vijisenti vya MCC na hili gharika la ushindi alioupata Magufuli?
Ile hela ya MCC ilikuja na masharti kuwa
* tufute sheria zetu za makosa ya mitandao,
* tubatilishe maamuzi ya Jecha katika ule uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.
Serikali yetu ikawapa MCC the middle finger na kuwaambia, kama ni huo msaada wenu ndio unaomipa jeuri ya kutuingilia tunavyoendesha nchi yetu, (basically kutupokonya sovereignty yetu) basi msitupe.
Hiki ni kitendo cha kijasiri na kujivunia. Watanzania wote tunapaswa kutembea vichwa juu na vifua mbele kwa uamuzi ule.
Kuhusu makubaliano ya serikali na Barrick yaliyotangazwa, kama sikosei ni hivi:
☆ $300m za kutuangukia kwa usumbufu waliotupa.
☆ Tunamiliki 16% ya machimbo
☆ Mgao wa faida ni 50-50 kati ya wachimbaji na serikali.
☆ Mapato ya haya makampuni yatawekwa kwenye mabenki ya ndani.
☆ Watakachochimba zaidi ya dhahabu, shaba na fedha yote itakuwa ni mali ya serikali.
☆ Watawaajiri Watanzania na kuwafunza taaluma za juu za uendeshaji migodi.
☆ Watahamisha ofisi zao kuu kutoka Afrika Kusini na Uingereza na kuzileta Tanzania.
☆ Nafikiri kuna vingine nilivyovisahau.
Mkuu unataka kufananisha zile $450m za masimango na mpukuti huu tunaoupata kwa makubaliano haya?
Pia ukumbuke kuwa, kuanzia sasa makubaliano yote yatakayofanyika kati ya wanaotaka kuchimba madini Tanzania na serikali yatafuata precedence hii.
Hebu piga makofi kidogo umpongeze Rais wako.
Ndo hapo tunapoitwa wapumbavuKwanza napenda kupongeza taarifa iliyotolewa leo baada ya majadiliano ya karibia miezi miwili na Barrick. Tumepata tulichopata na makubaliano mengine ambayo itabidi tusubiri kuona faida yake huko mbeleni. Nirejee kwenye mada, wote tunajua mwaka jana tuligomea msaada wa MCC wa dola 450m za bure kwa sababu hatukutaka msaada wa masharti. Ni kweli pesa zile tulizokosa kwa kushindwa tu kutumia busara ya kidiplomasia kwa makosa yetu ya kudharau demokrasia. Kwa bahati siku nazo hazigandi. Tukapata tume mbili zilizoshiba uzalendo zikachunguza wizi wa madini yetu hasa dhahabu. Tume zikafanya kazi kwa uzalendo kabisa na kutuletea data zisizoacha shaka kwa wizi tuliofanyiwa. Taasisi yetu ya mapato ikakokotoa wizi tuliofanyiwa ikakuta tunadai $190b zisizoacha shaka.
Leo hii wengine tunaukumbuka baadhi ya mambo tumepigwa na butwaa kwa kusikia mazungumzo ya wezi wetu wa Barrick yamefikia mwisho mwisho, lakini ni kama maamuzi halisi yameshatolewa. Maamuzi hayo ni pale mwizi wetu alipoona stahili yetu ni $300m tena za uaminifu kwamba yeye sio mwizi, na hizo atazitoa baada ya bodi yao huko London kuridhia! Watanzania tukalipuka kwa shangwe kwamba mwizi kanyoosha mikono. Wengine sisi tukaamua kwenda mbali zaidi na kujiuliza, iweje mwaka tu ulioisha tugomee $450m za bure kisha tuheshimu demokrasia, lakini tukubali $300m toka kwa mwizi tuliye na ushahidi nao mwaka mmoja mbele? Hapa hatunyoosheani vidole, lakini watanzania na waliochukua maamuzi hayo wametumia busara? Je hali hii ya kushindwa kupokea hela za bure kisha tuheshimu demokrasia na kupokea $300m toka kwa mwizi ipi ni maamuzi ya busara? Mawazo yoyote ni sawa kwani hii ndio demokrasia
CC: Paskali Mayalla, Quinine, Yehodaya, Jingalao, Mwigulu Nchemba, Zitto Junior
Nirejee kwenye mada, wote tunajua mwaka jana tuligomea msaada wa MCC wa dola 450m za bure kwa sababu hatukutaka msaada wa masharti. Ni kweli pesa zile tulizokosa kwa kushindwa tu kutumia busara ya kidiplomasia kwa makosa yetu ya kudharau demokrasia.
Mwisho wa siku hiyo $300m haki yetu sio haki yetu!?
Wenye upeo mdogo wa kufikiri wataamini,hii ni danganya toto asee,50/50 ni ndoto.
Haki yetu ni $190b na sio $300m tena zinaitwa za kujenga imani ya uaminifu. Mwizi anatoa $300m? Ingekuwa tume zetu na TRA hawajakokotoa hiyo hela hapo ningesema ni mambo ya mtaani. Lakini mpaka mamlaka ya mapato imesema wizi ni wa kiwango hicho unataka tueleweje?
Kwa hiyo ungekubali tu-legalize ushoga, kinyume cha maadili yetu, ili MCC watupe $450m ambazo ni theluthi (30%) ya makusanyo yetu ya kodi ya kila mwezi? Kweli mkuu?Kwanza nikupongeze kwa kutetea hata penye kosa la dhahiri. Sibezi makubaliano yaliyofikiwa lakini pesa za MCC zilikuwa nyingi kuliko hizi alizotupa mwizi wetu. Maamuzi ya kuzikosa hela za MCC yalikuwa ni kwa faida ya ccm na sio taifa kama unavyotaka tuamini. Maamuzi yale yalikuwa ni ya kiburi cha kukiuka demokrasia full stop.
Tuachane na hayo, tuje kwenye haya makubaliano yaliyofikiwa hasa hapa kwenye 50/50. Sio ww au mwingine yeyote anayetolea ufafanuzi wa mgawanyo wa 50/50. Je huu mgawanyo ni wa faida tu ama ni pamoja na gharama za uendeshaji? Iwapo hiyo 50/50 ni pamoja na gharama za uendeshaji sioni faida kubwa kama matarajio yetu yalivyo. Hao wazungu ni wajanja kuliko sisi, tena sio wajanja tu bali ni washenzi kabisa. Kwanini nasema hivyo? Kama tumeunda tume za maprofessor zaidi ya 2 zikadhibitisha tunaibiwa, mamlaka ya mapato ikapiga mahesabu tukakuta tunadai $190b. Hivi leo wametushinda na hatuwadai chochote, sanasana wametupa pole ya usumbufu ndio unadhani tutafanya lolote. Nipe ufafanuzi wa 50/50 kisha nikuambie kitu.
Yote hayo yamekuja kwa sababu ya ile pesa tunayowadai ni nyingi sana. Kama wangetulipa kiasi kile wangelikuwa wanamda mfupi sana wa kusavaiv, ndo maana wakakubali hivyo ("heli ya nusu shari kuliko shali kamili" wanaamini ACASIA)
Wenye upeo mdogo wa kufikiri wataamini,hii ni danganya toto asee,50/50 ni ndoto.
tindo bwana wewe, kila ninapotaka kulala ndio unanijibu?[emoji38][emoji38]
Vipi mkuu hujambo? Sasa ngoja nikulabue.
Kwa hiyo ungekubali tu-legalize ushoga, kinyume cha maadili yetu, ili MCC watupe $450m ambazo ni theluthi (30%) ya makusanyo yetu ya kodi ya kila mwezi? Kweli mkuu?
Halafu tukizungumzia hizi $300m. Sijui kama uliyasoma/sikiliza yale makubaliano vizuri. Kabla ya yale majadiliano kuna lile deni la kodi na faini ya kutolipa kodi walilosukumiwa ACACIA.
Hili halijaamuliwa bali BARRICK wamekubali kuna makosa yaliyofanywa. Kwa hiyo BARRICK wamesema, ili mjue tuna nia njema (good faith), hebu shikeni hizi $300m kwanza halafu kikosi kazi (working group) chenu kitajadiliana na ACACIA ili tupate muafaka. Tukipata muafaka basi tutalipa hicho cha ziada.
Nakushauri mkuu ukayasome yale makubaliano upya.
Swali zuri sana. Watu wengi wanashabikia huu mgao wa 50-50 wa faida na wanafikiri ni hela nyingi sana, hapana.
Katika hii migodi kuna wawekezaji ambao wanategemea kulipwa hisa (dividends) kila baada ya miezi 3 (quarter). Sisi tuna hisa ya 16%. Na kuna wengine, wakubwa sana ni BARRICK na ACACIA.
Kwa hiyo mapato ya mgodi kwanza ni lazima yalipie:
* gharama za uchimbaji na usafirishaji.
* hisa za wawekezaji wote
* gharama za utafiti na maendeleo (research & development)
Kinachobakia ndio faida ambayo ACACIA wangeweza kununua hisa nyingine au kuiweka kwenye fungu litakalotumika kuendeleza shughuli zao nyingine duniani. Sasa hii ndio faida tutakayogawana nao 50-50.
Hii faida sio kubwa lakini haiwezi kuwa negative kwa sababu kabla ya kugawa hisa wanahakikisha hawatakuwa na negative profit. Hii inaweza kutokea tu kama dividends zote ni sifuri, yaani hakuna mwanahisa anaelipwa kitu.
Kwa hiyo ni vizuri kuwa tutapata hii 50% ya faida lakini sio kubwa hivyooo.
Wew piga talumbeta hujui hata maana ya haki.....Haki yetu ilikua tel 400 na sio bln 700!!!!Mbona tunakua majinga hvi?Tutaendelea kuibiwa tu mana tumekua mijitu ya kushangilia tu.Hii ndo main point huko kwengine kote umeandika pumba tuu,umeshasema pesa za masharti sisi tumekataa hayo masharti shida ipo wapi??Hizi pesa za ACACIA sio za msaada na wala sio za masharti ni haki yetu.
Anayedhani fedha za MCC ni za bure anajaribu inabidi akapimwe uelewa wake...Na dola milioni 300 ni malipo ya awali wakati jopo dogo linapoendelea na mazungumzo ya kukokotoa malipo halisi na halali yanayopaswa kulipwa.....
Ni mafanikio makubwa hata hivyo, hasa tukikumbuka utabiri wa wale mitume wa kuzimu waliodhani kuwa ni taboo kudai chetu, na tungelipishwa mabilioni ya dola watakapotufikisha mahakama ya kimataifa ya usuluhishi, kwa jeuri yetu ya kupambana kichwa kichwa na wawekezaji hao!
Kama kawaida yao hiyo ni habari chungu kuikubali kama inawezekana. Watasubiri sana.
Hela zilikuwa na masharti yakiwemo hayo ya kutaka wanaume washike ukuta wavue chupi kwenye makalio wakutane na wanaume watoa misaada. Chadema nyie kazichukueni hizo pesa. Nyie si bila aibu mchana kweupe mlitangaza operation UKUTA nchi nzima? Mambo ya Ukuta na operesheni ukuta na kukamata ukuta nyie ndie wajuzi. Kawaombeni wawape pesa za UkutaJibu la kichovu, hiyo hela ya MCC haikuwa mara ya kwanza kuipokea. Ila safari tatizo lilikuwa uchaguzi wa Znz. Mnakimbilia kuhusu ushoga ila kuficha ukweli hasa wa tatizo ambao ni kuchezea demokrasia.
Kwanza napenda kupongeza taarifa iliyotolewa leo baada ya majadiliano ya karibia miezi miwili na Barrick. Tumepata tulichopata na makubaliano mengine ambayo itabidi tusubiri kuona faida yake huko mbeleni. Nirejee kwenye mada, wote tunajua mwaka jana tuligomea msaada wa MCC wa dola 450m za bure kwa sababu hatukutaka msaada wa masharti. Ni kweli pesa zile tulizokosa kwa kushindwa tu kutumia busara ya kidiplomasia kwa makosa yetu ya kudharau demokrasia. Kwa bahati siku nazo hazigandi. Tukapata tume mbili zilizoshiba uzalendo zikachunguza wizi wa madini yetu hasa dhahabu. Tume zikafanya kazi kwa uzalendo kabisa na kutuletea data zisizoacha shaka kwa wizi tuliofanyiwa. Taasisi yetu ya mapato ikakokotoa wizi tuliofanyiwa ikakuta tunadai $190b zisizoacha shaka.
Leo hii wengine tunaukumbuka baadhi ya mambo tumepigwa na butwaa kwa kusikia mazungumzo ya wezi wetu wa Barrick yamefikia mwisho mwisho, lakini ni kama maamuzi halisi yameshatolewa. Maamuzi hayo ni pale mwizi wetu alipoona stahili yetu ni $300m tena za uaminifu kwamba yeye sio mwizi, na hizo atazitoa baada ya bodi yao huko London kuridhia! Watanzania tukalipuka kwa shangwe kwamba mwizi kanyoosha mikono. Wengine sisi tukaamua kwenda mbali zaidi na kujiuliza, iweje mwaka tu ulioisha tugomee $450m za bure kisha tuheshimu demokrasia, lakini tukubali $300m toka kwa mwizi tuliye na ushahidi nao mwaka mmoja mbele? Hapa hatunyoosheani vidole, lakini watanzania na waliochukua maamuzi hayo wametumia busara? Je hali hii ya kushindwa kupokea hela za bure kisha tuheshimu demokrasia na kupokea $300m toka kwa mwizi ipi ni maamuzi ya busara? Mawazo yoyote ni sawa kwani hii ndio demokrasia
CC: Paskali Mayalla, Quinine, Yehodaya, Jingalao, Mwigulu Nchemba, Zitto Junior
Naona umeamua kutanua goli braza! Mimi nimeongelea ulichokisema juu ya madini ambayo Lissu alisema si mali yetu! Period.Kamuulize Lissu kama he was very right mbona hawajatushtaki huko MIGA kama alivyosema?