Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 4,153
- 3,800
Watanzania wenzangu, kuna kitu hakiko sawa!
Tutachanganyiwa lugha zote kuwa tunafungua nchi kumbe kuna hila ndani yake.
Sikubaliani kabisa viongozi kuzunguka dunia nzima kuomba pesa na uwekezaji.
Tunajidhalilisha!
Tuna bunge, Mawaziri, Wasomi, Wanasiasa, Wafanyabiashara maarufu nk, tumeshindwa kutulia na kukipanga hata iwe miaka 100 ijayo tukaijenga nchi yetu wenyewe? Hiyo haraka ni ya nini?
Wazee wetu kina Warioba, Msekwa, Malecela, Msuya nk niwaulize, mmekubali wajukuu zenu na elimu zao kuwa manamba wa Wazungu? Ndivyo hivyo Mwl. Nyerere aliwausia? Vijana,wajukuu zenu serikali iliwasomesha hadi vyuo vikuu ili wawe ombaomba duniani? Au waendesha bodaboda tuu na siyo kusimamia rasilimali zetu?
Ni kwa nini kila Rais aingiapo tunaruhusu alete mambo yake mapya na siyo kuendeleza ya mtangulizi au yaliyoasisiwa na nyie wazee wetu?
Mwl. Nyerere alituachia rasilimali tuzitumie kujiletea maendeleo au kuzinadia duniani?
Tujitizame.