KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Kumbe 'umezama' kidogo kuliko nilivyotegemea niliposoma mada yako huko ukurasa wa kwanza?Contents za subject matter unayojaribu kuadress ni bayana,lakini"Approach" yetu Ina kizungumkuti. Bado nasisitiza"Tujipime" tukae tupange tunachohitaji kama nchi,kabla ya"kufukuzia" kama ulivyosema fursa za wawekezaji na uwekezaji. Haraka ya nini? Tumepata Uhuru miaka 60 plus iliyopota,hatukujua population ya watu inaongezeka,leo tukurupuke hatuna madawati au madarasa? Na je,tutakopea vingapi endapo hata chaki ya mwalimu ni ya mkopo?
Juzi hapa,Mama yetu kaleta fedha za madarasa na madawati,umeona ilivyotumika nguvu kubwa kutetea hoja yake kwa wananchi! Wananchi wanasema nchi imejaa misitu kedekede ya kutengeneza madawati,leo wanaingizwa madeni kwa kofia ya Covid-19bila sababu za msingi!!!.
Unapomleta mwekezaji wa nje kwenye nchi,unatengeneza ajira 10,unavuruga 100 na za kudumu endapo kazi hiyo ingefanywa na sie wenyewe. Hilo liko wazi na mifano ipo!! Sera zetu za fedha hasa za mikopo ya nje haziko bayana!! Kila kiongozi anatumia "approach" tofauti hasa kujikwezea na kuunda"minorities" wa kumsemea , hapa Ina walakini. Mara nyingi imeonekana kwa nchi nyingi manufaa yake hayawezi kukuza uchumi ndani ya muda muafaka,pale mkopo unapolenga huduma za kijamii,. Kwani muda wa kurejeshwa tungeacha haraka,kwa nguvu za wananchi na "rasilimali "zilizopo hiyo kazi ingekuwa imeisha bila kuiminya jamii kufaidisha wageni.
Nina maono makubwa na Nchi yangu,tusijione wanyonge,na tusijidekeze,tunaweza. Kumchukua Mwarabu Oman kuja kuwekeza kilimo cha Zabibu ni fedheha kwa Taifa!
Nimetumia lugha nyepesi nieleweke.
Heshima mkuu.
Lakini sidhani kwamba mkuu 'chige' ataweza kukuelewa kwa haya uliyoweka hapa. Huyu kapofushwa na usakaji wa u'oligarch'wa kiTanzania.