Watanzania tulio wengi tunampenda Hayati Rais Magufuli, hamtafanikiwa kubadilisha ukweli huo kamwe!

Watanzania tulio wengi tunampenda Hayati Rais Magufuli, hamtafanikiwa kubadilisha ukweli huo kamwe!

Napenda nitoe tahadhari kwa ccm, viongozi wa serikal na vyama vya siasa kuwa kwa sasa Hayati Dr John Pombe Magufuli hatunaye tena. Ametangulia mbele za haki. Sii jambo la busara kila kukicha kumtaja na kumshutumu marehem as if alikuwa akiendesha hili taifa peke yake.

Nataka niwakumbushe taifa hili lina watu ambao wanamshauri Rais na hao watu au hiyo team ina inatoka ktk National Securty Team kutoka ktk vyumba vya ndani vya wana usalama hawa hutoa report nankimshauri Rais na Rais kwa utashi wake huchaguwa mbivu na mbichi au hutoa maoni yake before action.

Hakuna jambo linafanyika au linakuwa impliment linalo husu mambo yakiusalama la hili taifa hawa jamaa wasiwepo. Ndio maana mwisho wa Yote Rais hashitakiwi jiulize why?

Jambo lakusimama kwenye mimbari na kwenye vyombo vya dunia nakumpaka tope Magufuli niswala lita ligawa hili taifa pamoja na chama na idara zake. Tuwe wakweli kila zama na kitabu chake Mwinyi alifanya makosa, Nyerere Mungu amrehem alifanya makosa, Jakaya alifanya makosa, Mkapa Mungu amrehem alifanya makosa. Iweje Magufuli ndio imekuwa story of town.

Mimi nitasema jambo moja na wenye akili mtanielewa. Magufuli alipo ingia kwenye serikali jambo zito sana sana alikutana nalo ilikuwa swala la kutoka siri za serikali hii kitu aliikomesha kwa mkono wa chuma na tuseme ukweli ilifika muda watu walishindwa kuijuwa kesho ndani ya ikulu jambo hili liliwaumiza watu wengi sana.

Kama mnajuwa au hamjuwi unaposema Magufuli alifanya hivi au vile kama kweli unamanisha basi chama cha ccm hakipaswi kuwepo kinapaswa kufutwa kama Nazi kule german Yes huwezi msema mtu aliekuwa ndani ya chama kama mwenyekiti na clips zore zipo mnamsifia leo mnasema alikuwa mbaya naomba niseme ukweli tutakuwa wanafiki na mnafiki dawa yake ni moja kumuweka pemebeni. Leo Mwenza wake alie rithi kiti aseme JPM alikuwa mbaya yani huyo hafai hata kwa kumuweka chumvi na hii sio kanuni yangu ni kanuni inaongoza usalam wa dunia.

Tunamsema sana huyu baba na familia yake inaumia sana maana tuseme ukweli hakuna waziri wala Rais amewahi kifikia viwango vya kazi ya huyu mwamba. Wazungu wenyewe pamoja na propaganda wanajuwa jamaa alikuwa chuma cha pua na alikiwa Rais mwenye akili sana na ipo siku watoto wa watoto wetu watamfukua nakumpima uwezo wake. Kwa kipindi cha miaka sita ametuacha kama taifa tuna duwaa, na kwasababu ya chuki zetu ndani ya mioyo leo tunamsema vibaya ili kuficha udhaifu wetu maana tunajuwa jamaa alikuwa mwamba na hata formla alitumia kuendesha taifa wote tupo puzzled.


Tunamfedhehesha kuhusu issue ya covid 19 while upo ukweli baraza ka usalama wa Taifa uliutowa juu ya lockdown na hathari za muda mrefu kwa uchumi wetu na ndipo ikakubalika tusifunge uchumi hali itakuwa mbaya kuliko ugonjwa wenyewe na ikakubalika iwe siri vifo ili watu wasiwe na hofu. Jambo leo dunia yote hakuna anaye toa data wala kusema issue ya covid ukiacha china. Hatukutoa vaccine yes ila nalo lilielezwa mlitakaje? Mbona walioenda kimya kimya walidondoka na hatunao?

Ktk hali kama hii kusimama na kumlaumu Magufuli ni dhambi haya nchi simmekabidhiwa sasa mbona hamfungi watu ndani na kutoa idadi wanakufa kila siku kwa Covid 19 Mbona hatusikii kelele za wanao piga chanjo zore ni historia tupo royal tour?

Mnajisikiaje mnapo kutana na mjane na watoto wake mnao wasema kila siku baba yao na masikini marehem hawezi kujitetea. Je mnafikiri ccm itakuwa madarakani 100 ijayo? Na kama haitokuwa what if mtoto wa magufuli au mjukuu wake atashika atam maana msijisahau mkadhani mtakuwa nyie tu hapo ikulu au mtakuwa nyinyi tu watoto wa marais upo wakati watu watakuwa huru kushika hiyo nafasi ombeni asiwe mtoto wa magufuli au mjukuu waka au kitukuu chake. U will pay the price hata kama mmelala.

Jifunzeni kwa wengine zama zina badilika na wananchi wana akili angalien Brazil Yule Rais mstaafu Lula Da Siliva walimfunga miaka kadhaa kwa ufisadi ndio wananchi wana mpenda, angalie hapo Zambia rais wa sasa Aikande kama sijakosea alifungwa kwa kosa la kutopaki pembeni wakati rais alie mpisha kiti akipita barabarani tena walimpa jinai leo ndio Rais wa Zambia. Twenda kule Philippines wamemchaguwa mtoto wa Alie kuwa dictator aliongoza taifa kwa mkono wa chuma kama Magufuli leo mtoto wamempenda... Sasa endeleeni tu kunanga Magufuli ambaye hayupo nasi ila kazi zake zipo na zitakuwepo mpaka miisho yote.

Magufuli hayupo nasi, Magufuli alipewa kitabuncha risi na kazi zakufanyia kazi akazifanya kwa mkono wa chuma hasa swala la madawa ya kulevya alifyeka wote ndani. Hili liliwauma sana tunajuwa, ujambazi ilikuwa mama mkanye mwanao alifyeka wote ndani mnajuwa hili nainawauma sana, wizi na ubadhirifu mali ya umma yani hiíiíiííiiií aliwaliza sana najuwa hamuwezi kumpenda.

Aliipa idara ya usalama nguvu kubwa sana mithili ya nyakati za mwalimu yani vigogo na matajiri walijamba cheche idara iliweza ku track mpaka sindano kwenye sehem hazifikiki shikamoo Baba Magufuli hili liliwatesa sana wanaume wa Tz... Yaniiii Hiiiiiiiii nawanajuwa yani aliwachezesha sana... Siwezi kusema sanaa ..

Aliwapenda wanyonge na aliwaota wanyonge na wanyonge walipata haki zao na pesa waliona acheni huyu baba alale hakuna mtu wa chini utamuuliza kuhusu Magufuli amseme vibaya ktk moja ya mahojiano na kijana mmoja pale kariakoo aliniambia anatamani kuwe na Magufuli day na walitamani siku awaite yani wangefunga uwanja wa Benjamini Mkapa. Acheni huyu Mzee apumzike.
Itaendelea
 
umesema kweli sana tupaazi sauti zetu na itabidi tuwashughulikie wanaomsema jpm tumechoka sana inauma sana chadema ni watu ovyo wao ndio kwanza kumsema makufuli kisa mfalme mbowe akupata nafasi ya ubunge na kuwekewa stop na sabaya. nyerere kafanya mengi mabaya hamsemi, mkapa pia kikwete ndio zaidi lakini mpo kimyaa
 
umesema kweli sana tupaazi sauti zetu na itabidi tuwashughulikie wanaomsema jpm tumechoka sana inauma sana chadema ni watu ovyo wao ndio kwanza kumsema makufuli kisa mfalme mbowe akupata nafasi ya ubunge na kuwekewa stop na sabaya. nyerere kafanya mengi mabaya hamsemi, mkapa pia kikwete ndio zaidi lakini mpo kimyaa
Umshughulikie bibi yako labda. Akili za kimagufuli hizi, mkishindwa hoja ni vitisho, kupiga , kuteka na kuua. Umbwa kabisa. Washamba. Kutumia maguvu bila akili.
 
Hatutaki asahaulike kamwe,we loved him dearly.Roho zetu zinaumia sana,tumepoteza jembe,mjenzi halisi wa Mama Tanzania.
Wengine tutamkumbuka zaidi kwa madhila aliyosababishia Watanzania, kifo chake kilileta faraja na furaha kwa baadhi yetu kwani maisha ya kuishi kwa kuwindana kama Simba na Swala mbugani hayapo tena.
Huo mpasuko unaousema Mwendakuzimu ndiyo aliuleta lakini sasa Samia ana-heal majeraha yaliyoachwa na Magu, ilikuwa hali ya ajabu watu waliwindwa na kuuawa, kujeruhiwa, kutekwa na kuteswa kwa sababu tu ya tofauti za kiitikadi. Mpumbavu yule alikuwa katili mwenye roho mbaya sana.
 
2025 ndio hatima yao mafedhuri wote wanao shangilia kifo cha JPM.... kuna ujinga mwingi sana umerejea na mijitu inashangilia tu kwa upofu wa chuki na uzandiki.
Jiwe aliharibu nchi afadhari alikufa mapema mbwa yule
 
A blind man indeed.Yote hayo yangefanikiwaje bila yeye kumaliza muda wake na kuwa na continuity.Sina haja ya kutetea his legacy,even a normal man in the village can see.Ukimsikiliza Magufuli,ukiangalia body language yake na matendo yake,you see a new Tanzania.That is who he was.
He was a disgrace to our country
 
Huwezi kunilisha maneno mjinga wewe!!
Mpumbavu anaweza kuosha vyombo vya chakula kwa kutumia maji taka kwa kuwa tu ameona wengine wakiosha.
Maneno yapi niliyokulisha? Kama yapo nioneshe niyaondoe, sina sababu yoyote ya kufanya hivyo.
 
Nashauri tungetengeneza character wa kucheza umagufuli katika katuni, waoneshwe watoto wetu wajifunze model ya uzalendo na maamuzi.

Tutunge na hadithi za stori zake [hadithi za stori!😂😂] zinazomuonesha kiongozi wa mfano. Tuwekemo makosa kiasi yaliyofafanuliwa kuweka balansi kidoogo. Wafundishwe watoto maana vijana ni wabishi sana. Vijana wawafundishe watoto wao.

Huu ndio unaiywa uwekezaji wa muda mrefu. Taifa linahitaji kuongeza idadi ya watu ambao ni wakuaminika/trustworthy. Bila ma role model tutawaaminishaje kizazi chetu?

Kwa maslahi mapana ya taifa
 
Lakini pia uongouongo sio mzuri kwa taifa, watu wanakosa trust. Mwishoni wanakosa upendo/uzalendo

Wajitokeze tu hadharani waseme kama ni COVID mixer Moyo mbona hivi vitu sio mutually exclusive hata! Wengi wanaosumbuliwa na covod wanakufa kwa matatizo yao mengine ya kudumu so kama walisema ni moyo labda tuseme walisema nusu ya ukweli wafanye kuukamilisha tu. Eaasy.

So Mathanzua ukweli ni kitu kipana sana wala usinabaike, yabebe yote tu
 
Nitamkumbuka daima Rais Magufuli kwa kuwa alikuwa mtu mwenye maamuzi na maamuzi mengi yaliwakilisha asilimia 80 ya Wananchi wa Tanzania.
 
Awamu ya fulani nimeisahau jina,Waziri Mkuu alikwenda nchi fulani akakuta vigari vidogo vingi,viswift,visuzuki akaambiwa hivi vigari ndio wanatumia Mawaziri,Waziri Mkuu wetu alishangaa,akaishia kusema kule kwetu basi tu sijui kama inawezekana,Waziri Mkuu lakini alikuwa hana maamuzi🤔
 
Awamu fulani nimeisahau jina Rais aliletewa list ya Mafisadi papa akaishia kusema awa wakiguswa nchi itatikisika.
 
Rais Magufuli alikuwa anasimama anasema Serikali inahamia Dodoma na mara moja ofisi zinaanza kujengwa na Serikali inahamia Dodoma,hakuna longolongo.
 
Nitamkumbuka daima Rais Magufuli kwa kuwa alikuwa mtu mwenye maamuzi na maamuzi mengi yaliwakilisha asilimia 80 ya Wananchi wa Tanzania.
 
Niliposikia kwa mara ya kwanza kwamba hii Sinema ya Royal Tour (ambayo Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ni Main Actor and Tour Guide) ina assert kwamba kifo cha Hayati John Pombe Magufuli kimesababishwa na Covid,nilistuka na sikuamini masikio yangu!Kwa maoni yangu hii inam-compromise sana Rais Samia ambaye ndiye aliyetutangazia kifo cha Hayati Magufuli na kutufahamisha kwamba kilichomuua Rais Hayati Magufuli ni Ugonjwa wa Moyo! Sasa haya ya COVID-19 yametoka wapi tena?!

Najiuliza
a) Hivi Rais Samia alikubalije kushiriki sinema inayopotosha taarifa ya serikali kuhusu jambo zito kama hili?!
b) Kwa nini hakudai hicho kipande kiondolewe?!!
Sitashangaa sana akitokea "mtetea chochote" akisema Rais Samia hakuiona script na kujiridhisha kwamba script ipo sahihi(if it is all acceptable) kabla ya uzinduzi wa movie huko Marekani! That would be a serious blunder and an act of gross incompetence on the part of her presidential advisers.
Kwa maoni yangu anayeongea kwenye hii script ni "Spin Master", na utetezi wake umekaa kipuuzi na hauna mashiko. Ashakum si matusi.
Iwapo anachosema "Spin Master" ndiyo hoja na majibu ya serikali (kwamba kilichosemwa kuhusu sababu ya kifo cha Magufuli ni COVID-19 ni kauli ya Wanaharakati (ambao wanatajwa kwa majina), mimi naomba kuuliza mbona sasa hawakusema (kwenye hiyo sinema ya Royal Tour) kwamba "kuna na Watanzania wengi wengine (na hata watu wa nje),ambao wanaamini Rais Magufuli kauawa?!
Rais Samia aliwahi kuwakemea kwa hasira wanaodai Hayati Rais Magufuli kauawa.Akasema wenye ushahidi kwamba Hayati Rais Magufuli kauawa wampelekee.

Baada ya sinema ya Royal Tour kulikoroga, ni wazi sasa kwamba kumbe kweli kuna umuhimu wa kuunda Tume Huru ya kuchunguza kifo cha Rais John Pombe Magufuli. Wadanganyika tunataka kujua kwa uhakika: Je, Rais Magufuli alikufa kwa Ugonjwa wa Moyo (ambao haukusababishwa na mkono wa Mtu), alikufa kwa COVID-19 au aliuwawa?! Na alikufa lini exactly?!
Naamini Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ataona umuhimu huu. Asipuuze hili, hasa ikizingatiwa kwamba yeye ndiye Main Actor and Main Guide in this movie that has come up with this act of not only gross disrespect for our late President but also explosive provocation directed towards our Nation and all Tanzanians!
Namshauri pia Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan awe mwangalifu sana kutambua kwamba kifo cha Magufuli kimeligawanya Taifa... na hivyo afanye kazi ya ziada kutuunganisha badala ya kutugawa na kuruhusu Watu (na hasa) Viongozi kutonesha vidonda kila kukicha!

Kauli tata zimeshamiri nchini na zinaleta taharuki kila kukicha!
Mfano wa kauli tata!
a) "...ile ilikuwa Nidhamu ya woga tu!"
b) "Nchi imeharibiwa sana hii!"
c) "Sasa tunairudisha Tanzania Duniani!"
d) N.k.

Kwa bahati mbaya sana, kauli zinazotolewa kila kukicha kumkandia na kuchafua jina la Hayati Rais Magufuli zinachochea wasiwasi na hasira kwa baadhi ya Watanzania! Kama nilivyosema, zinaleta taharuki. Baadhi ya Wadanganyika tunajiuliza:
a) Kwa nini wenzie waliomo serikalini ndio wanaongoza mashambulizi?!
b) Kwa nini serikali ya Awamu ya 6 inaonekana ku-enjoy kuitupia madongo serikali ya awamu ya 5,yaani serikali ya Magufuli?Strangely, by more than 90%, serikali ya awamu ya 6 ndiyo serikali ya awamu ya 5!! Rais wa sasa ndiye alikuwa Makamu wa Rais Magufuli (na Mshauri wake Mkuu), Makamu wa Rais wa sasa ndiye alikuwa Waziri wa Fedha, Waziri Mkuu yuleyule, Mkuu wa Usalama wa Taifa yuleyule, IGP yuleyule, CDF yuleyule, Jaji Mkuu yuleyule n.k., n.k.
c) Kwa nini baadhi ya Viongozi wa serikali ya awamu ya 6 wanatoa matamshi ambayo yanaashiria kwamba kumbe (labda) walikuwa na Chuki kubwa kwa Rais, Mwenyekiti na Amiri Jeshi Mkuu wao, Rais Magufuli?!
d) Inakuwaje wale wote waliotofautiana na Rais Magufuli wamepandishwa vyeo na kauli zao na matendo yao yanaonyesha hawajutii walichofanya?! Ni kama vile wanatamba kwa "Ushujaa" wao wa kupambana na Rais Magufuli?! Wote tunazikumbuka zile audio clips...!!
e) Kwa nini baadhi ya viongozi wa "Matawi ya Juu" nchini wako bize kumbomoa Magufuli and his Legacy! Hivi hii well-coordinated attempt at "Character Assassination" ina lengo gani na faida gani?! Imesababishwa na nini?!
f) Kwa nini serikali na Chama hamumtetei Magufuli?! Saa zote ni kimya au mashambulizi tu! Kwa nini???
g) Hivi mmesahau kwamba mwenzenu amepumzika na hana tena Uwezo wa Kujitetea?
h) Hivi mmesahau kwamba Hayati Rais Magufuli ameacha Mke na Watoto ambao mnawaumiza sana kwa Mashambulizi yenu na/au kimya chenu? Kwa nini msiwaache walau wakauke machozi? Hivi mnasahau kwamba wao ni Bin Adam na wanawashangaa sana, to say the least?

Hivi ni sawa kweli kwamba Serikali, Chama Tawala, Wabunge, Mawaziri, Taasisi mbalimbali, Jumuia mbalimbali (mfano: UV-CCM, UWT, Wastaafu, n.k.)... wote mko kimya kabisa kila Hayati Magufuli anavyotukanwa na kudharirishwa?! Eti hata Viongozi wa Dini nao mko kimya! Mbona haiingii akilini?!Unafiki huu, mmm...! Au labda ni ukondoo tu...?! Au ni guilty consciousness...?!

Sasa kama Magufuli alikuwa Rais mbaya kiasi hicho (which I don't believe anyway), inawezekanaje nyinyi washirika wake wote muwe wasafi kiasi hicho cha kuthubutu kumtupia mawe mazito hivyo Mwenzenu?!
a) Collective Responsibility iko wapi?!
b) Hivi nyie wengine mnaponaje?!
c) Hivi mnajua kwamba kwenye sheria za kimataifa iliwekwa precedent kwenye Nuremberg Trials (baada ya Vita Kuu ya Dunia)?! Kesi za Washirika wa Hitler...! Kwa kifupi, Mahakama ya Kimataifa iliamua kwamba Rais/Kiongozi Mkuu hawezi kuwa Shetani na Mawaziri/Wasaidizi wake wote wakawa Malaika...!! Never!
d) Mbona mnatufanya wadanganyika mafala?!
e) Mbona mnajichanganya hivyo?!

Narudia!
a) Wasiwasi na hasira za Wadanganyika zinasababishwa na mengi,na sina shaka yeyote kwamba siku moja sitakuja kuzaa matunda.
b) Mungu anayajua maovu yetu yote,huwezi kuficha,na hukumu zake ni za kweli.
c) Tusicheze na moto!

MUNGU IBARIKI TANZANIA!

Zaidi hapa[emoji116]


Ukweli umeshabadilishwa mama anapendwa na zaidi ya 95% ya watanzania na 100% ya wasio watanzania

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
 
Uongo dhambi jpm alikuwa kiongozi pendwa na watu hakuna kama yeye acheni unafiki sawa
 
Ukweli umeshabadilishwa mama anapendwa na zaidi ya 95% ya watanzania na 100% ya wasio watanzania

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
Upigaji kama kawaida,utendaji ume-stall,Kikwete yuko madarakani,inflation is at all time high,mabepari wamepewa nchi atapendwaje?Kwa anayejitambua,hawezi kumpenda Samia,ni panya anayeuma na kupulizaia.Bado Samia haingii kwenye akili za Wananchi na wanaojitambua.Upendo unaozungumzia wewe ni wa mitandaoni.

Mfanyakazi kuongezewa eti 23% mshahara,na sio wote ni lower cadre,hiyo si inamezwa na inflation.Halafu eti wafanyakazi wanashangilia,jamani uzuzu mwingine huu.

Finally Davos tumepeleka Mawaziri wanne!Hivi hii haikuonyeshi tu kwamba nchi imeuzwa,halafu unakenua,ajabu sana.Unajua kinachoendelea Davos kweli wewe.Kule wanapanga mipango ya kuua binadamu na mipango miovu ya kuendeleza kutuibia ili wafanikishe mipango yao ya kuendelea kutuua na kuitawala Dunia.Sasa kwa kupeleka Mawaziri wanne,ina maana Samia anakubaliana na uovu wa NWO wanao-tufanyia,wewe utampendaje,si uzuzu huo.Jamani amkeni,mmelala mno.

Soma hii 👇uone uovu unaopangwa Davos,wala sijui kama utaelewa,mmelala tu.


 
Back
Top Bottom