Watanzania tulio wengi tunampenda Hayati Rais Magufuli, hamtafanikiwa kubadilisha ukweli huo kamwe!

Napenda nitoe tahadhari kwa ccm, viongozi wa serikal na vyama vya siasa kuwa kwa sasa Hayati Dr John Pombe Magufuli hatunaye tena. Ametangulia mbele za haki. Sii jambo la busara kila kukicha kumtaja na kumshutumu marehem as if alikuwa akiendesha hili taifa peke yake.

Nataka niwakumbushe taifa hili lina watu ambao wanamshauri Rais na hao watu au hiyo team ina inatoka ktk National Securty Team kutoka ktk vyumba vya ndani vya wana usalama hawa hutoa report nankimshauri Rais na Rais kwa utashi wake huchaguwa mbivu na mbichi au hutoa maoni yake before action.

Hakuna jambo linafanyika au linakuwa impliment linalo husu mambo yakiusalama la hili taifa hawa jamaa wasiwepo. Ndio maana mwisho wa Yote Rais hashitakiwi jiulize why?

Jambo lakusimama kwenye mimbari na kwenye vyombo vya dunia nakumpaka tope Magufuli niswala lita ligawa hili taifa pamoja na chama na idara zake. Tuwe wakweli kila zama na kitabu chake Mwinyi alifanya makosa, Nyerere Mungu amrehem alifanya makosa, Jakaya alifanya makosa, Mkapa Mungu amrehem alifanya makosa. Iweje Magufuli ndio imekuwa story of town.

Mimi nitasema jambo moja na wenye akili mtanielewa. Magufuli alipo ingia kwenye serikali jambo zito sana sana alikutana nalo ilikuwa swala la kutoka siri za serikali hii kitu aliikomesha kwa mkono wa chuma na tuseme ukweli ilifika muda watu walishindwa kuijuwa kesho ndani ya ikulu jambo hili liliwaumiza watu wengi sana.

Kama mnajuwa au hamjuwi unaposema Magufuli alifanya hivi au vile kama kweli unamanisha basi chama cha ccm hakipaswi kuwepo kinapaswa kufutwa kama Nazi kule german Yes huwezi msema mtu aliekuwa ndani ya chama kama mwenyekiti na clips zore zipo mnamsifia leo mnasema alikuwa mbaya naomba niseme ukweli tutakuwa wanafiki na mnafiki dawa yake ni moja kumuweka pemebeni. Leo Mwenza wake alie rithi kiti aseme JPM alikuwa mbaya yani huyo hafai hata kwa kumuweka chumvi na hii sio kanuni yangu ni kanuni inaongoza usalam wa dunia.

Tunamsema sana huyu baba na familia yake inaumia sana maana tuseme ukweli hakuna waziri wala Rais amewahi kifikia viwango vya kazi ya huyu mwamba. Wazungu wenyewe pamoja na propaganda wanajuwa jamaa alikuwa chuma cha pua na alikiwa Rais mwenye akili sana na ipo siku watoto wa watoto wetu watamfukua nakumpima uwezo wake. Kwa kipindi cha miaka sita ametuacha kama taifa tuna duwaa, na kwasababu ya chuki zetu ndani ya mioyo leo tunamsema vibaya ili kuficha udhaifu wetu maana tunajuwa jamaa alikuwa mwamba na hata formla alitumia kuendesha taifa wote tupo puzzled.


Tunamfedhehesha kuhusu issue ya covid 19 while upo ukweli baraza ka usalama wa Taifa uliutowa juu ya lockdown na hathari za muda mrefu kwa uchumi wetu na ndipo ikakubalika tusifunge uchumi hali itakuwa mbaya kuliko ugonjwa wenyewe na ikakubalika iwe siri vifo ili watu wasiwe na hofu. Jambo leo dunia yote hakuna anaye toa data wala kusema issue ya covid ukiacha china. Hatukutoa vaccine yes ila nalo lilielezwa mlitakaje? Mbona walioenda kimya kimya walidondoka na hatunao?

Ktk hali kama hii kusimama na kumlaumu Magufuli ni dhambi haya nchi simmekabidhiwa sasa mbona hamfungi watu ndani na kutoa idadi wanakufa kila siku kwa Covid 19 Mbona hatusikii kelele za wanao piga chanjo zore ni historia tupo royal tour?

Mnajisikiaje mnapo kutana na mjane na watoto wake mnao wasema kila siku baba yao na masikini marehem hawezi kujitetea. Je mnafikiri ccm itakuwa madarakani 100 ijayo? Na kama haitokuwa what if mtoto wa magufuli au mjukuu wake atashika atam maana msijisahau mkadhani mtakuwa nyie tu hapo ikulu au mtakuwa nyinyi tu watoto wa marais upo wakati watu watakuwa huru kushika hiyo nafasi ombeni asiwe mtoto wa magufuli au mjukuu waka au kitukuu chake. U will pay the price hata kama mmelala.

Jifunzeni kwa wengine zama zina badilika na wananchi wana akili angalien Brazil Yule Rais mstaafu Lula Da Siliva walimfunga miaka kadhaa kwa ufisadi ndio wananchi wana mpenda, angalie hapo Zambia rais wa sasa Aikande kama sijakosea alifungwa kwa kosa la kutopaki pembeni wakati rais alie mpisha kiti akipita barabarani tena walimpa jinai leo ndio Rais wa Zambia. Twenda kule Philippines wamemchaguwa mtoto wa Alie kuwa dictator aliongoza taifa kwa mkono wa chuma kama Magufuli leo mtoto wamempenda... Sasa endeleeni tu kunanga Magufuli ambaye hayupo nasi ila kazi zake zipo na zitakuwepo mpaka miisho yote.

Magufuli hayupo nasi, Magufuli alipewa kitabuncha risi na kazi zakufanyia kazi akazifanya kwa mkono wa chuma hasa swala la madawa ya kulevya alifyeka wote ndani. Hili liliwauma sana tunajuwa, ujambazi ilikuwa mama mkanye mwanao alifyeka wote ndani mnajuwa hili nainawauma sana, wizi na ubadhirifu mali ya umma yani hiíiíiííiiií aliwaliza sana najuwa hamuwezi kumpenda.

Aliipa idara ya usalama nguvu kubwa sana mithili ya nyakati za mwalimu yani vigogo na matajiri walijamba cheche idara iliweza ku track mpaka sindano kwenye sehem hazifikiki shikamoo Baba Magufuli hili liliwatesa sana wanaume wa Tz... Yaniiii Hiiiiiiiii nawanajuwa yani aliwachezesha sana... Siwezi kusema sanaa ..

Aliwapenda wanyonge na aliwaota wanyonge na wanyonge walipata haki zao na pesa waliona acheni huyu baba alale hakuna mtu wa chini utamuuliza kuhusu Magufuli amseme vibaya ktk moja ya mahojiano na kijana mmoja pale kariakoo aliniambia anatamani kuwe na Magufuli day na walitamani siku awaite yani wangefunga uwanja wa Benjamini Mkapa. Acheni huyu Mzee apumzike.
Itaendelea
 
umesema kweli sana tupaazi sauti zetu na itabidi tuwashughulikie wanaomsema jpm tumechoka sana inauma sana chadema ni watu ovyo wao ndio kwanza kumsema makufuli kisa mfalme mbowe akupata nafasi ya ubunge na kuwekewa stop na sabaya. nyerere kafanya mengi mabaya hamsemi, mkapa pia kikwete ndio zaidi lakini mpo kimyaa
 
Waliompenda ni wenye upofu na upeo mdogo sana.
 
Umshughulikie bibi yako labda. Akili za kimagufuli hizi, mkishindwa hoja ni vitisho, kupiga , kuteka na kuua. Umbwa kabisa. Washamba. Kutumia maguvu bila akili.
 
Hatutaki asahaulike kamwe,we loved him dearly.Roho zetu zinaumia sana,tumepoteza jembe,mjenzi halisi wa Mama Tanzania.
Wengine tutamkumbuka zaidi kwa madhila aliyosababishia Watanzania, kifo chake kilileta faraja na furaha kwa baadhi yetu kwani maisha ya kuishi kwa kuwindana kama Simba na Swala mbugani hayapo tena.
Huo mpasuko unaousema Mwendakuzimu ndiyo aliuleta lakini sasa Samia ana-heal majeraha yaliyoachwa na Magu, ilikuwa hali ya ajabu watu waliwindwa na kuuawa, kujeruhiwa, kutekwa na kuteswa kwa sababu tu ya tofauti za kiitikadi. Mpumbavu yule alikuwa katili mwenye roho mbaya sana.
 
2025 ndio hatima yao mafedhuri wote wanao shangilia kifo cha JPM.... kuna ujinga mwingi sana umerejea na mijitu inashangilia tu kwa upofu wa chuki na uzandiki.
Jiwe aliharibu nchi afadhari alikufa mapema mbwa yule
 
He was a disgrace to our country
 
Huwezi kunilisha maneno mjinga wewe!!
Mpumbavu anaweza kuosha vyombo vya chakula kwa kutumia maji taka kwa kuwa tu ameona wengine wakiosha.
Maneno yapi niliyokulisha? Kama yapo nioneshe niyaondoe, sina sababu yoyote ya kufanya hivyo.
 
Nashauri tungetengeneza character wa kucheza umagufuli katika katuni, waoneshwe watoto wetu wajifunze model ya uzalendo na maamuzi.

Tutunge na hadithi za stori zake [hadithi za stori!😂😂] zinazomuonesha kiongozi wa mfano. Tuwekemo makosa kiasi yaliyofafanuliwa kuweka balansi kidoogo. Wafundishwe watoto maana vijana ni wabishi sana. Vijana wawafundishe watoto wao.

Huu ndio unaiywa uwekezaji wa muda mrefu. Taifa linahitaji kuongeza idadi ya watu ambao ni wakuaminika/trustworthy. Bila ma role model tutawaaminishaje kizazi chetu?

Kwa maslahi mapana ya taifa
 
Lakini pia uongouongo sio mzuri kwa taifa, watu wanakosa trust. Mwishoni wanakosa upendo/uzalendo

Wajitokeze tu hadharani waseme kama ni COVID mixer Moyo mbona hivi vitu sio mutually exclusive hata! Wengi wanaosumbuliwa na covod wanakufa kwa matatizo yao mengine ya kudumu so kama walisema ni moyo labda tuseme walisema nusu ya ukweli wafanye kuukamilisha tu. Eaasy.

So Mathanzua ukweli ni kitu kipana sana wala usinabaike, yabebe yote tu
 
Nitamkumbuka daima Rais Magufuli kwa kuwa alikuwa mtu mwenye maamuzi na maamuzi mengi yaliwakilisha asilimia 80 ya Wananchi wa Tanzania.
 
Awamu ya fulani nimeisahau jina,Waziri Mkuu alikwenda nchi fulani akakuta vigari vidogo vingi,viswift,visuzuki akaambiwa hivi vigari ndio wanatumia Mawaziri,Waziri Mkuu wetu alishangaa,akaishia kusema kule kwetu basi tu sijui kama inawezekana,Waziri Mkuu lakini alikuwa hana maamuzi🤔
 
Awamu fulani nimeisahau jina Rais aliletewa list ya Mafisadi papa akaishia kusema awa wakiguswa nchi itatikisika.
 
Rais Magufuli alikuwa anasimama anasema Serikali inahamia Dodoma na mara moja ofisi zinaanza kujengwa na Serikali inahamia Dodoma,hakuna longolongo.
 
Nitamkumbuka daima Rais Magufuli kwa kuwa alikuwa mtu mwenye maamuzi na maamuzi mengi yaliwakilisha asilimia 80 ya Wananchi wa Tanzania.
 
Ukweli umeshabadilishwa mama anapendwa na zaidi ya 95% ya watanzania na 100% ya wasio watanzania

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
 
Uongo dhambi jpm alikuwa kiongozi pendwa na watu hakuna kama yeye acheni unafiki sawa
 
Ukweli umeshabadilishwa mama anapendwa na zaidi ya 95% ya watanzania na 100% ya wasio watanzania

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
Upigaji kama kawaida,utendaji ume-stall,Kikwete yuko madarakani,inflation is at all time high,mabepari wamepewa nchi atapendwaje?Kwa anayejitambua,hawezi kumpenda Samia,ni panya anayeuma na kupulizaia.Bado Samia haingii kwenye akili za Wananchi na wanaojitambua.Upendo unaozungumzia wewe ni wa mitandaoni.

Mfanyakazi kuongezewa eti 23% mshahara,na sio wote ni lower cadre,hiyo si inamezwa na inflation.Halafu eti wafanyakazi wanashangilia,jamani uzuzu mwingine huu.

Finally Davos tumepeleka Mawaziri wanne!Hivi hii haikuonyeshi tu kwamba nchi imeuzwa,halafu unakenua,ajabu sana.Unajua kinachoendelea Davos kweli wewe.Kule wanapanga mipango ya kuua binadamu na mipango miovu ya kuendeleza kutuibia ili wafanikishe mipango yao ya kuendelea kutuua na kuitawala Dunia.Sasa kwa kupeleka Mawaziri wanne,ina maana Samia anakubaliana na uovu wa NWO wanao-tufanyia,wewe utampendaje,si uzuzu huo.Jamani amkeni,mmelala mno.

Soma hii 👇uone uovu unaopangwa Davos,wala sijui kama utaelewa,mmelala tu.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…