Watanzania tumekosea wapi? Nilidhani masihara kuwa gharama za vifurushi zimeendelea kupanda

Watanzania tumekosea wapi? Nilidhani masihara kuwa gharama za vifurushi zimeendelea kupanda

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
12,207
Reaction score
26,521
Kwa masikitiko makubwa niende moja kwa moja.

Watanzania wengi hatuelewi na hatujapata bado ufafanuzi sababu zinazopelekea Vifurushi vya Internet kupanda mara kwa mara tena kwa ghafla miezi michache tokea Rais Samia achukie madaraka.

Alianza kuupiga mwingi hadi tukawa tunajifia mitandao kwa kuongoza kwa unafuu wa gharama za internet kipindi Gb1 unapata kwa Tsh1,000/= lakini ghalfa zikaanza kupanda kwa awamu hatimaye leo awamu ya tatu kupanda tokea awe madarakani(kama sikosei) nimekuta Tsh3,000/= mtu unapata Gb 1.5 na mitandao yote vifurushi viko bei ghali kuliko vilivyokuwa ghali awali.

Athari nilizoziona kutokana tokea hali hii ilivyoanza miezi iliyopita na kuongezeka sasa;

1. Kuongezeka wimbi la watu wanaotumia njia haramu za kupata bando za bure mfano Free VPN.

Huko Telegram nimechunguza nimekuta magroup maalumu kwa akji ya watu kupeana hayo maujanja ili kuendana na ukali wa hali hata mitaani na hapa Jf ukiwa na connection ya VpN ya free data watu kibao wanakufuata Pm na wengine wapo radhi kukuchangia chochote kitu hivyo inachangia mapato ya serikali kupotea kwa asilimia kubwa.

2. Kupungua Idadi ya views youtube kwa asilimia kubwa na watu kukosa mapato.Hata wasanii wamepigwa za uso miezi hii na haijawahi kutokea kuwa na idadi ndogo namna hiyo kwa fanbase yao

3. Kupunguza motisha ya watu kusaka maarifa mtandaoni. Mimi nilikuwa ninachanel zangu maalumu za kufuatilia makala maalumu na mada za kisanyansi, kihistoria nk huko YouTube lakini nina miezi YouTube naiogopa kwenye simu yangu na naipitia ili nibaki kuperuzi angalau JF.

4. Ongezeeni wana JF....

#UziTayari
 
Kutumia free VPN kumbe ni haramu! Nilikuwa sifahamu
Ni kosa kisheria ,lakini sasa FreeVpn na maujanja ya kupata bando bure imekuwa maarufu sana bongo mimi nilikuta grupu lina members kama buku Kazi kupeana madini tu mpaka nikabaki nacheka jinsi watu wanavyohangaika humo.
 
Mkuu kwa airtel hii

freebasics inakubali?!
Ni kwa halotel tu zamani ilikuwa mitandao karibia yote na nimesajili halotel kwa sababu ya Freebasic ikiondolewa navunja laini kabisa maana kwa uzoefu wangu halotel wanachukua bando haraka sana na ipo namba 2 kwa mtindo huo usukani ukishikiliwa na Airtel.
 
Mkuu mm niliuninistall APPS ya INSTAGRAM
nikitaka kuingia natumia CHROME BROWSER
INSTAGRAM ndio lilikuwa JINI baya sana la kumaliza bando kwenye simu yangu
ilikuwa ngumu sana lkn kutokana na ukali wa maisha ilibidi nizoee

INSTAGRAM autoplay VIDEO haijawahi kumuacha mtu salama kwenye BANDO
 
Changamoto sana ila ndio time ya survival for fittest.

kiswahili ni Afrika Mashariki, Kiswahili ni Tanzania, Kiswahili ni Amani na Upendo.
 
Ni kwa halotel tu zamani ilikuwa mitandao karibia yote na nimesajili halotel kwa sababu ya Freebasic ikiondolewa navunja laini kabisa maana kwa uzoefu wangu halotel wanachukua bando haraka sana na ipo namba 2 kwa mtindo huo usukani ukishikiliwa na Airtel.
Hahahah, wazalendo wacha tulipe kodi😂😂
 
Mkuu mm niliuninistall APPS ya INSTAGRAM
nikitaka kuingia natumia CHROME BROWSER
INSTAGRAM ndio lilikuwa JINI baya sana la kumaliza bando kwenye simu yangu
ilikuwa ngumu sana lkn kutokana na ukali wa maisha ilibidi nizoee

INSTAGRAM autoplay VIDEO haijawahi kumuacha mtu salama kwenye BANDO
Mimi insta ndio naiogopa kabisa ,nahisi inakaribia miezi sita tokea niingie mara ya mwisho.
 
Back
Top Bottom