Watanzania tumekosea wapi? Nilidhani masihara kuwa gharama za vifurushi zimeendelea kupanda

Kwa masikitiko makubwa niende moja kwa moja..

Watanzania wengi hatuelewi na hatujapata bado ufafanuzi sababu zinazopelekea Vifurushi vya Internet kupanda mara kwa mara tena kwa ghafla miezi michache tokea Rais Samia achukie madaraka.

Alianza kuupiga mwingi hadi tukawa tunajifia mitandao kwa kuongoza kwa unafuu wa gharama za internet kipindi Gb1 unapata kwa Tsh1,000/= lakini ghalfa zikaanza kupanda kwa awamu hatimaye leo awamu ya tatu kupanda tokea awe madarakani(kama sikosei) nimekuta Tsh3,000/= mtu unapata Gb 1.5 na mitandao yote vifurushi viko bei ghali kuliko vilivyokuwa ghali awali.

Athari nilizoziona kutokana tokea hali hii ilivyoanza miezi iliyopita na kuongezeka sasa;

1.Kuongezeka wimbi la watu wanaotumia njia haramu za kupata bando za bure mfano Free VPN.

Huko telegram nimechunguza nimekuta magroup maalumu kwa akji ya watu kupeana hayo maujanja ili kuendana na ukali wa hali hata mitaani na hapa Jf ukiwa na connection ya VpN ya free data watu kibao wanakufuata Pm na wengine wapo radhi kukuchangia chochote kitu hivyo inachangia mapato ya serikali kupotea kwa asilimia kubwa.

2.Kupungua Idadi ya views youtube kwa asilimia kubwa na watu kukosa mapato.Hata wasanii wamepigwa za uso miezi hii na haijawahi kutokea kuwa na idadi ndogo namna hiyo kwa fanbase yao

3.Kupunguza motisha ya watu kusaka maarifa mtandaoni .Mimi nilikuwa ninachanel zangu maalumu za kufuatilia makala maalumu na mada za kisanyansi,kihistoria nk huko YouTube lakini nina miezi YouTube naiogopa kwenye simu yangu na naipitia ili nibaki kuperuzi angalau Jf .

4.Ongezeeni wana Jf....

#UziTayari
Ndugu wananchi vita yaUkraine na mlipuko wa uviko-19 umeathiri uchumi wa Dunia, nimezoea kusikia hivyo.
 
Hebu leta hayo maujanja watu tunaumia mno na hali za maisha.
Kuna siku niliweka status kwamba mimi ni Mr VpN ili kupima upepo huwezi amini wadau wameonesha muitikio mkubwa kuhujumu uchumi kwa VpN
IMG_20220801_200758.jpg
 
Aisee sasa hivi uzi unakaa siku nzima na comments sita halafu unakuta zinamhusu mkuu wetu.

Daah.
 
Na ssi tupewe mipango Kaz jins ya kufanya niweze kupat free vpn niachane na bando la nape na samia
Maujanja yapo watu wanapiga kimya kimya sababu kuna kuna maujanja yalivuma sana kipindi cha ilikuwa unateleza kama umeweka bando tena kwa spidi ya juu bila kukwama kwama mahali popote .

Sasa kuna watu ulimbukeni wakawafuata Tigo kwenye social media kuwatambia na kuvimba na wengine wakajiita wazalendo wakaenda kuchoma makao makuu kuwa kuna watu wanawanyonya kwa kuperuzi bure hapo likapita panga kali wakafyeka Vpn zinasapoti spidi kubwa zote.

Baada ya hapo mabaharia wakakubaliana kwenye vikao vyao ngoma ichezwe kimya kimya na ndiyo hali sasa ilivyo.
 
Kwa masikitiko makubwa niende moja kwa moja..

Watanzania wengi hatuelewi na hatujapata bado ufafanuzi sababu zinazopelekea Vifurushi vya Internet kupanda mara kwa mara tena kwa ghafla miezi michache tokea Rais Samia achukie madaraka.

Alianza kuupiga mwingi hadi tukawa tunajifia mitandao kwa kuongoza kwa unafuu wa gharama za internet kipindi Gb1 unapata kwa Tsh1,000/= lakini ghalfa zikaanza kupanda kwa awamu hatimaye leo awamu ya tatu kupanda tokea awe madarakani(kama sikosei) nimekuta Tsh3,000/= mtu unapata Gb 1.5 na mitandao yote vifurushi viko bei ghali kuliko vilivyokuwa ghali awali.

Athari nilizoziona kutokana tokea hali hii ilivyoanza miezi iliyopita na kuongezeka sasa;

1.Kuongezeka wimbi la watu wanaotumia njia haramu za kupata bando za bure mfano Free VPN.

Huko telegram nimechunguza nimekuta magroup maalumu kwa akji ya watu kupeana hayo maujanja ili kuendana na ukali wa hali hata mitaani na hapa Jf ukiwa na connection ya VpN ya free data watu kibao wanakufuata Pm na wengine wapo radhi kukuchangia chochote kitu hivyo inachangia mapato ya serikali kupotea kwa asilimia kubwa.

2.Kupungua Idadi ya views youtube kwa asilimia kubwa na watu kukosa mapato.Hata wasanii wamepigwa za uso miezi hii na haijawahi kutokea kuwa na idadi ndogo namna hiyo kwa fanbase yao

3.Kupunguza motisha ya watu kusaka maarifa mtandaoni .Mimi nilikuwa ninachanel zangu maalumu za kufuatilia makala maalumu na mada za kisanyansi,kihistoria nk huko YouTube lakini nina miezi YouTube naiogopa kwenye simu yangu na naipitia ili nibaki kuperuzi angalau Jf .

4.Ongezeeni wana Jf....

#UziTayari
Ukiona umeshindwa amia Burundi
 
Aisee sasa hivi uzi unakaa siku nzima na comments sita halafu unakuta zinamhusu mkuu wetu.

Daah.
Raia sasa wamesusia serikali sio kama zamani hata machawa wamesusia mechi ,kuna uzi juzi wa teuzi live nilicheka sana kuona haujavuka hata page moja wakati zamani siku 100 za mwanzo kulikuwa na mafuriko na mapambio mengi
 
Nape amesema unahitajika muujiza ili kuweza kuzuia bei za vifurushi zisipande, ni lazima zipande na huo ndio ukweli mchungu
Inabidi tuzoee tu hakuna namna 😢😢😢
 
Back
Top Bottom