Watanzania tumekosea wapi? Nilidhani masihara kuwa gharama za vifurushi zimeendelea kupanda

Watanzania tumekosea wapi? Nilidhani masihara kuwa gharama za vifurushi zimeendelea kupanda

Internet ni huduma ya msingi kwa zama hizi sioni hata sababu ya kusema watu waanze kulia wakat internet inawezwa kuwekwa hata mitaani humo watu wakawa wanafanya postpaid service na inakua unlimited.
 
Waziri nape anaishi nchi gani ?
Screenshot_20220816_214056.jpg
 
Wazee wa Vitonga wanazidi kuongezeka
Screenshot_20220816_214514.jpg
 
Hali ya maisha kiukweli imekua juu sana Tanzania!! Mama alichotufanya anajua mwenyewe!
Inasikitisha sana naweka bando la eflu tatu halafu YouTube na Insta naiogopa ili utoboe nalo hata siku 5 zamani mtu unajiachia popote.
 
Inasikitisha sana naweka bando la eflu tatu halafu YouTube na Insta naiogopa ili utoboe nalo hata siku 5 zamani mtu unajiachia popote.
Bei ya vifurushi imekua juu sana hasa kwenye data ndio kabisaaa!
 
Gb 2 imefikia buku tano na nina miezi kama miwili na kitu sasa sijaingia YouTube maarifa yananipita bure .
 
Mimi nowadays najiunga GB 1 kwa elfu mbili. Sie wa Zantel /TIGO ndio sielewi hasa naona naona tu.

Bando ghali na ukijiunga tu linaenda kasi ajabu [emoji22]
 
Inasikitisha sana naweka bando la eflu tatu halafu YouTube na Insta naiogopa ili utoboe nalo hata siku 5 zamani mtu unajiachia popote.
Basi mie nikajua sie wa Zantel tu ndio imekuwa hivyo baada ya migration kwenda tigo.

Kumbe kote hali ni tete.

Nikijiunga GB25 kwa mwezi kwa elfu 35. nikitumia kwa fujo, ilikuwa mpk zikikaribia siku kwisha GB zipo za kutosha hadi na download movie Netflix.

sasa napata GB 19 tu. Na nikipwesa tu zimeisha [emoji24]
 
Mimi nowadays najiunga GB 1 kwa elfu mbili. Sie wa Zantel /TIGO ndio sielewi hasa naona naona tu.

Bando ghali na ukijiunga tu linaenda kasi ajabu [emoji22]
Serikali imeweka kodi kubwa ndio maana wenye mitandao wanatubana sisi na mapato lazima yapatikane kwani kuingia mtandaoni ni Alosto ya wengi zaidi ya teja kukosa madawa hivyo ni lazima watu wajiunge tu ,sasa hali mbaya mno mtu hata kuingia YouTube unawaza mara mbili vifurushi ghali na vinakimbia mno .
 
Wanataka tu faida mara tano tano na utakuta wenye mali ni wazungu na wachina mifaida inapelekwa kwao
 
Zinazidi kuongezeka tena na bado, Kitaalamu inaitwa kupigwa mpaka kuchakaa.
 
Starlink nayo inawekewa vikwazo kibao mpaka maji tuite mma.
 
Mpaka sasa zinazidi kupanda gharama ya kujinga kifurushi cha kawaida mpaka upate Gb1 unatumia gharama kubwa sana tofauti na awali na zinazidi kupanda tu .
 
Starlink nayo inawekewa vikwazo kibao mpaka maji tuite mma.

Ndio maana inafikia pahala wawekezaji wenyewe wanashindwa masharti ya hili linchi lililojaa rushwa, ulaji, ukandamizaji, ufisadi na uporaji badala yake wanakimbia na kuhamishia biashara zao nchi zinazowajali.

Kila unapogusa unakumbana na kodi. Aise huyu mama yetu ajiangalie sana, hii nafasi aliyonayo ni dhimma na ataenda kuulizwa maswali. ALLAH amuongoze.
 
Back
Top Bottom