ProcrastinatorInChief
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 13,027
- 29,556
Best Comment na Imejaa Usomi zaidi..Habari! Naomba na mimi kuchangia mawazo yangu hapa.
Kitu ambacho ninaamini tunapaswa kuweka juu ya vitu vyote vingine ni watanzania wote kuwa na maisha wanayostahili kuwa nayo na kuwa na maendeleo na amani nchini. Ndiyo kunamgawanyiko nchini na sio kitu kizuri hata kidogo. Uchawa unaua nchi kwasababu kwenye demokrasia, wananchi wanapaswa kuruhusiwa kutoa maoni yao kuhusu serekali na mambo yanayoendelea nchini. Wafanyakazi wa serekali na wanasiasa ni binadamu kama sisi, kuna mambo wanafanya ambayo ni mema na pia wanamakosa pia. Hamna binadamu asiye na makosa na ukikosa inabidi ukubali kuambiwa na kujaribu kurekebisha mambo. Maraisi wote, kwanzia Mwalimu Nyerere mpaka Mama Samia kuna vitu ambavyo wamepatia sana na kuna vitu vilivyohofisha wananchi. Uchawa unaharibu vitu kwasababu unafanya watu waabudu mtu, wanampigia debe mtu mpaka wanatia shaka kuwa lazima kunatatizo hapa.
Kuna mphilosophia muingereza, Thomas Hobbes, ambaye hujulikana kama mmoja wa watu waliondika kuhusu the social contract -- ambayo ni wazo kuwa watu kwasababu ya huduma serekali zinazowapa wanachi kama kulinda usalama na kujenga na kuendesha mashule na mahospitali etc inakubali serekali na kuipa nguvu. Wananchi wanakuwa na imani kuwa serekali yao inawasaidia kuwa na miasha mazuri. Huu mkataba (theoretically) kati ya wanachi na serekali usipokuwa imara, shida huanza. Shida zinakuja wananchi wakikosa imani na serekali na ndio maana wima wa wananchi ndio unapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza katika maamuzi yote ya serekali.
Kitu ambacho husaidia mahusiano kati ya serekali na wananchi, raisi na wanachi ni mawasiliano. Wananchi wanapaswa kuwa na njia za uwazi za kujadili na serekali. Serekali inapaswa kuwaonyesha wananchi kuiinawajali sana. Watu wakiamini kuwauchawa ndio utawasaidia kuwapa maisha mazuri ni shida kwasababu kwa ukweli serekali inapaswa kusaidia kila mwananchi, sio tu wanaowasifia.
On a sidenote: Mimi kabla hatasijasoma hoja nzima JF naweza kujua kama umeandikwa na chawa nikiona kwenye paragraph moja mheshimwa raisi kaitwa daktari mara 10. Kwa mawazo yangu, taji la mama linaheshima kuliko hata daktari. Ukiwa na honorary doctorate unaweza kuitwa daktari lakini sio lazima. Kuna watu walipewa hizo shahada za heshima nyingi sana kama Nelson Mandela na Oprah Winfrey na hamna siku hata moja tunawasikia wanaitwa daktari. Nilibahatika kukutana na raisi mstaafu wa Malawi, Joyce Banda, na sikujua nimuite nani, mheshimwa, raisi ? Nikamuuliza kama naweza kumuita Mama Banda, akasema sasa unite nini kingine ?
Aminata Wewe Ndo Yule mtoto wa Kaka Yangu Kinana?