Jumbe Brown
JF-Expert Member
- Jun 23, 2020
- 12,035
- 12,814
Unataka sera zipi na wakati mh.SSH ni mwendelezo wa AWAMU ILIYOPITA ambayo ndiyo iliyoinadi ILANI YA CCM?!!!Nchi huru hii, msilazimishe watu wasimkosoe SSH wakati hana sera wala vision zaidi ya ku please kila kundi kwa kugawa na kutapanya ovyo keki ya taifa.
duuh unadhani atafanya yote hayo in a flash?!?, ile kusema atakutana na viongozi wa vya siasa vingine/wapinzani ili akae nao waone wataipelekaje nchi mbele kwa pamoja ni hatua njema sana maana hapo nyuma kidogo hilo halikuwepo kabisa ilikua nia uadui 100%. hebu naombeni tusubiri ataongea nao nini pengine kupitia jukwaa hilo ndio hizo ahueni unazosisema kuhusu akina TL tutazisikia. kufuta kesi na kutoa mtu jela ni vitu vyenye mchakato tofauti mpe mda mama. nyota njema huonekana mapema
Nyie washabiki wa wanasiasa ni vile hamjipi nafasi kujitafakari, mnaowasema hapa sasa ndio wale waliowasema ninyi wakati wa Magufuli ila sema nyani haoni kundule na unapojitahidi kulisha kiu yako daima unamuona alie kinyume chako hajielewi.....wanaomkosea heshima Rais Samia ni vijana wa mataga ambao wana hasira ya kuondokewa na mpendwa wao Rais Magufuli.
..wengi tulishawahi kuonya kwamba kundi la mataga limejaa vijana wasioweza kufanya siasa za hoja.
..uwezo wa vijana wa mataga upo kwenye kupotosha, kutukana, kudhalilisha, na vurugu.
Umejisahau mara hii ulimvyokuwa ukimtukana huyo unaemuita Rais wa Mataga na sukumagang?MATAGA na Sukuma Gang wako busy mitandaoni kumtukana Rais
Wakati hao wanaotukana Sasa kwa mujibu wako walipotukanwa wakati ule ulitoa neno?Mkuu, usiingie kwenye mtego huo,
Maana ukianza kuwajibu kwa hasira na lugha Kama hiyo utafanana nao waliokosa heshima mkuu wangu,
Mjinga akikutukana mbele za watu, mtazame na utabasamu, atajidharau sana
That's it, hii ndio ilipaswa kuwa mada yako kuu na sio kushangaa watukanaji na wakosoaji wa Sasa halafu hukuwashangaa wale waliomtukana na kumkosoa Magufuli ambao mpaka Sasa wanaendelea akiwa kaburini anasikia Kama IPO hiyo nafasiNadhani Ni busara Sana kwetu watanzania tukajikita kuchambua Sera za nchi na mwelekeo tuutakao kwa taifa letu kwa kuiweka mbele taswira chanya ya taifa letu.
Ni mbegu mbaya Sana ikiwa tutaendekeza kutengenezeana timu zinazojiita majina yanayotukuza kiongozi mmoja huku yakimdhalilisha na kumkosea heshima mwingine
Kwani CCM imebadilika baada ya uongozi wa Samia kutoka CUF?Huwezi kutengeneza taswira chanya kuhusu nchi iliyojaa dhuluma na udhalimu. Juzi tu kesi 147 zimefutwa kwa sababu zilikuwa ni za kubambikiwa na wahusika hawajachukuliwa hatua zozote zile za kisheria. Nyingine chungu nzima zilikuwa zimeshahukumiwa na wahusika kulipishwa faini ya mabilioni au kuhukumiwa kifungo cha miaka mingi na wakati huo huo mama yuko kimya kuhusu kuwatendea haki Watanzania hawa. Mama yuko kimya kuhusu COVID-19 ambao wanalipwa mabilioni ya pesa za walipa kodi pamoja na kuwa wameokotwa barabarani na kikatiba hawana hadhi ya kuwa Bungeni. Lissu kadhulumiwa sana haihitaji hata dakika 10 kwa mama kutoa amri kwamba Lissu aliyewahi pesa yake yote matibabu lakini bado akapiga kimya sijui hadi lini!? Bado tuna safari ndefu sana katika nchi hii.
Ajabu nyingine hiyo....nchi Ina watu wa ajabu kweli kweli hiiLeo hii mama mnamtambua Ni Rais aliyetokana na uchaguzi wa 2020 mnaosema ccm iliiba kura,? Na kumbe mnamtambua Ni Rais na mnahitaji msaada wake?
Ikawaje then?Unadhani kwanini Mkapa mwaka 2019 alitaka uchaguzi wa 2020 usimamiwe na Tume huru ya uchaguzi? Na huyo ni mtu wa ccm aliyewahi kuwa Rais na Mwenyekiti wa maccm. Kwa sababu alijua Tume iliyopo ni FAKE na KAMWE haiwezi kusimamia uchaguzi huru na wa haki.
View attachment 1797695
Na waliomtukana Baba walikuwa wakina Nani?Hahaha, MATAGA ndiyo wanamtukana Mama?
Hawaoni matendo yao hakika, unafiki uliopitiliza, hawakumtambua Magufuli mwizi wa kura wanamtambua mgombea mwenza wa Magufuli mama yao alietoka CUF kwenda CCM kuwaokoa....hatari sanaMkuu, sisi tunamfuatisha kiongozi wetu lisu (aka mashikishwa ukuta, zezeta, dishi limeyumba), ndiye alianzisha huo mchezo wa matusi. Aliwatukana wabunge kwa kusema wanaunga mkono mambo ya kijinga, kisha akahamishia matusi kwa rais aliyepita Hayati Dr John Pombe Magufuli. Wafuasi wake kina BAK, tindo, Mmawia, nk wote wanarusha matusi humu mitandaoni kwa muda mrefu sasa.
Wanae wanaumia asikosolewe mama yao kutoka ufipaYeye kasema tumkosoe.. Tena kwa ukali.. Vp tena. !!
Wanashindwa kusema asikosolewe kwakuwa anawaplease ndio hulalama kana kwamba wao hawakosoi wengine, maisha bila unafiki hayawezekani nchi hiiNchi huru hii, msilazimishe watu wasimkosoe SSH wakati hana sera wala vision zaidi ya ku please kila kundi kwa kugawa na kutapanya ovyo keki ya taifa.
Wakati wakimtukana Magufuli ilikuwa haki eehh?Uko sahihi Sana.....
Ni ADABU MBOVU....
Ni UKOSEFU WA NIDHAMU NDANI YA NAFSI ZAO.....
Ni MALEZI MABOVU WALIYOPATA UTOTONI....
Inakuwaje kijana mkubwa anamtukana mtu mzima....tena RAIS na AMIRI JESHI WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA?!!! Khaaa khaaaa.....
Mtu huyohuyo hawezi hata kumtukana "mgambo" njiani....Leo mtandaoni anamtukana RAIS WA NCHI Khaaa khaaaa SIASA ZA HOVYO KABISA......
Mfano wa tabia hizo alikuwa nazo Tundu Lissu katika KAMPENI ZA UCHAGUZI ULIOPITA.......
#KaziIendelee
Ataongea porojo tu nasi tutashangilia hakuna matokeo yoyote kikubwa atawaplease watu anaowaona tishio kwa utawala wake maana Hana uwezo wa kuhandle makasiriko yao.duuh unadhani atafanya yote hayo in a flash?!?, ile kusema atakutana na viongozi wa vya siasa vingine/wapinzani ili akae nao waone wataipelekaje nchi mbele kwa pamoja ni hatua njema sana maana hapo nyuma kidogo hilo halikuwepo kabisa ilikua nia uadui 100%. hebu naombeni tusubiri ataongea nao nini pengine kupitia jukwaa hilo ndio hizo ahueni unazosisema kuhusu akina TL tutazisikia. kufuta kesi na kutoa mtu jela ni vitu vyenye mchakato tofauti mpe mda mama. nyota njema huonekana mapema
Huyo jamaa ni uliyemjibu nadhani ni mtu aliyeathirika sana kwa namna moja ama nyingine kutokana na Magufuli kuwa Rais!Nyie washabiki wa wanasiasa ni vile hamjipi nafasi kujitafakari, mnaowasema hapa sasa ndio wale waliowasema ninyi wakati wa Magufuli ila sema nyani haoni kundule na unapojitahidi kulisha kiu yako daima unamuona alie kinyume chako hajielewi...
Sasa hivi ninyi mliokosoa serikali ya CCM chini ya Magufuli wenye ufahamu wameshawaona hamkuikosoa serikali bali shida yenu ilikuwa Magufuli na bado ameshakufa anawatesa dhamira zenu, tukiwauliza leo CCM imekuwa mpya mtakosa majibu maana CCM Ni ile ile kazi yake kuwageuza geuza Kama chapati,Rais alierithi Sasa alitoka nje ya CCM? Hakuwa msaidizi wa karibu wa Magufuli? Lipi jipya au porojo mpya zenye kutafuta music unadundaje wakati huu?
Nchi inahitaji watu wanaohitaji nchi na hii midundo ya wanasiasa wenye huba zetu haijawahi kutusaidia nchini...
CCM Ni ile ile, tatizo linalojitegemea.
Usiniulize mimi...kwani sijawahi kumtukana MAGUFULI...siwezi kumtukana MWENYEKITI WANGU WA CHAMA BORA na AMIRI JESHI....Wakati wakimtukana Magufuli ilikuwa haki eehh?
Chuki zake na ubinafsi tu hana lolote.Huyo jamaa ni uliyemjibu nadhani ni mtu aliyeathirika sana kwa namna moja ama nyingine kutokana na Magufuli kuwa Rais!
Amekuwa kama zumbukuku flani hivi. Yeye kila kitu kwake sasa hivi kina revolve around Magufuli tu!
Anawatwisha watu projections zake. Anadhani eti watu wanaomkosoa Samia ni watu walioumizwa sana na kifo cha Magufuli!
Nadhani yeye ndo alikuwa anaumizwa sana na urais wa Magufuli na sasa anaya-project hayo maumivu yake kwa watu wengine.
Ni mmoja kati ya watu niliokuwa nawaheshimu sana humu. Sasa hivi kageuka takataka.
Sasa namdharau kabisa. Sijui Magufuli alimfanyaga nini tu.
Uliwakemea waliomtukana Mwenyekiti wako?Usiniulize mimi...kwani sijawahi kumtukana MAGUFULI...siwezi kumtukana MWENYEKITI WANGU WA CHAMA BORA na AMIRI JESHI....
Usitutie KAPU MOJA....
Kule kwenye madarasa ya ITIKADI YA CCM kunafundishwa nidhamu ya SIASA na kiongozi mkuu wa nchi "hakosolewi" kwa maneno makali na mabaya.....
#KaziIendelee
#SiempreCCM
Miaka 6 nilipambana na hilo.....Uliwakemea waliomtukana Mwenyekiti wako?