Watanzania tumheshimu Rais, hatukufunzwa hovyo hivi

Watanzania tumheshimu Rais, hatukufunzwa hovyo hivi

Leo hii mama mnamtambua Ni Rais aliyetokana na uchaguzi wa 2020 mnaosema ccm iliiba kura,? Na kumbe mnamtambua Ni Rais na mnahitaji msaada wake?
Wee vipi weeweeee! Aliyeiba kura, aliyeharibu uchaguzi, kisha kufa na kuzikwa Chato!
 
Inachukua masaa mangapi kutoa amri kwamba Lissu alipwe haki zake? Kama kafuta kesi 147 FAKE kwanini anashindwa kufuta hukumu za waliohukumiwa na kutozwa faini ya mabilioni au kushindwa kulipa sasa wanaozea lupango? Kutangaza hadharani kwamba COVID 19 si Wabunge hivyo wasiingie tena Bungeni inachukua muda gani? Kumbuka HAKI huinua Taifa Na dhuluma huangamiza Taifa.
Hebu acha uongo banaaaa! Mbona Nusrat Hanje alitolewa usiku usiku kinyume na taratibu ili kutimiza udhalimu wao kwanini hao waliobambikiwa kesi FAKE ishindikane kuwatoa haraka? Ni rahisi kusema apewe muda wakati Watanzania chungu nzima wanaendelea kudhulumiwa haki zao. Ungekuwa ni mmoja wao wa hao waliobambikiwa kesi usingeandika apewe muda.
hahahaa unataka naye aende kwa mtindo wa akina nusrat!?!. Calm down the president will take care of everything step by step kila mtu ana matamanio yake, yako hayajafikiwa kuwa subra yatafikiwa tu. kwa mfano mimi natamani uwepo mfuko wa unemplyoyed beneficial fund tusiokuwa na ajira serikali iwe inatupa posho kwa mwezi, sijakata tamaa, sina hasira, situkani, nina matumaini atanifikia
 
Nchi huru hii, msilazimishe watu wasimkosoe SSH wakati hana sera wala vision zaidi ya ku please kila kundi kwa kugawa na kutapanya ovyo keki ya taifa.
Kweli mzee, makundi yote anayaplease, lakini katutenga sisi MATAGA na SUKUMA gang, sijui tumemkosea nini
 
MATAGA na Sukuma Gang wako busy mitandaoni kumtukana Rais
Nyie mlimtukana magufuli mpaka sasa bado mnaendelea ila mmesahau mnaona kama mmeokoka

Bado sindano lazima iwaingie tu, samia bado ni CCM ni mwenzetu hawezi kujua jirani kabla ya watoto wake.
 
FREEDOM OF EXPRESSION!

Mkosoaji anabaki kuwa mkosoaji tu,na huwezi kumpangia maneno ya kukwambia!

Mleta HOJA unayo hoja ya msingi ila tatizo ni kwamba Taifa kama taifa hatuna Dira ya Taifa.

Bali tuna Dira za makundi ya Viongozi na matakwa yao Vibindoni.

Watu wanakosoa kwa HASIRA sababu wanaona wazi kinachoendelea kujipanga nchini kwa sasa.

Watanzania Tuache unafiki na Makundi ya kimkakati.

Mifano hai ni kama hii
[emoji116]

Unamstaafisha #Anna Mghwira aliezaliwa 1959,kwa kigezo cha Umri huku ukimteaua Makongoro Nyerere pia aliezaliwa 1959?...

Wakati huohuo unaye waziri MuraMura wizarani aliezaliwa 1956?
Tukirudi kwenye uteuzi wa Makongoro......mjumbe pekee wa kamati ya maadili #CCM, ambaye huwa hapepesi macho inapokuja suala la kuwaeleza UKWELI vigogo ndani ya chama bila kupepesa macho!

Tukuelewe vipi mheshimiwa mteuzi?
Kwamba unaondoa vikwazo ndani ya kamati ili kusafisha njia?

Brigedia anakamata Tani moja ya Madawa ya kulevya,badala ya kupongezwa na kupandishwa cheo ili ajiimarishe kitaasisi yake, leo anapewa ubalozi ili akae mbali?

Tunao wastaafu wengi waliolitumikia hili taifa kwa uzalendo uliotukuka,lakini leo hawana hata uhakika wa matibabu yao,lakini huyu mmoja mzee HASSAN,yeye kero yake kubwa ni kupanda gari refu?
Pamoja na kwamba bado anapokea 80% ya mshahara kutoka kwenue kiwango cha mshahara wa rais aliyepo madarakani. Lakini Samia Hassan anamtunukia BENZ la millioni 400[emoji1787]

Watu wakiongea mnasema SUKUMA gang!
Kwa sababu waliokuwa wakiongea hapo awali walikuwa Gang gani?

CCM ilikwishaanza kurejea kwa wananchi na kila mmoja wetu alijisikia kama sehemu ya maamuzi bila kujali kipato chake!

Leo mnaanza kutuletea #CCM vunjabei?

Kwa Maslahi ya nani??

Pale waziri alieahidi kuondoa magugu wizara ya mambo ya nje,halafu anamleta mdogo wake kuwa Balozi,je tumuelewe vipi mteuzi??

□Mambo ni mengi kuyasema humu JF ni kumtwisha mzigo Maxcence bila sababu....

Twende hadharani..........

[emoji1241]2025
View attachment 1797790View attachment 1797791View attachment 1797793
 
Wanabodi,

Nawaomba Sana na kuwasihi Watanzania wenzangu tuitunze na kuienzi tunu yetu ya taifa inayoaksi malezi na maadili yetu ya kitanzania ambayo Ni heshima na uungwana kwa binadamu wenzetu.

Hivi karibuni kuna magenge yanazuka mitandaoni yakimkosoa Rais wa JMT Mh. Samia Suluhu Hassan, kwa bahati mbaya sana wanamkosoa kwa kumsodoa kwa maneno yasiyo na sitaha kwa kiongozi wa nchi, tabia hii haifai kabisa na sio nidhamu tuliyofunzwa Watanzania.

Ikiwa twahitaji kumkosoa Rais Basi na tufanye hivyo kwa lugha yenye staha na heshima, na tukumbuke kuwa huyu Ni Rais wa nchi yetu, huzuni yake Ni yetu pia, heshima yake ni yetu na akidhalilika Ni taifa linadhalilika, ukimdhalilisha Rais wako Ni Nani unayemtegemea amheshimishe?

Tuvumilie na tufunike hisia zenye hasira ndani yetu Kisha tukosoe kwa staha.

Nawasihi sana, Uhuru wa kuongea na kuonyesha hisia zetu usigeuke kuwa Uhuru wa kutukana na kuonyesha hasira zetu.

Mwisho:
Tuna wajibu wa kumsikiliza Rais na kuamini kwamba hakuna mama anayeweza kuwapa watoto wake sumu, hisia za mama ni nzito sana kwa watoto.
Sina hakika kama kuna Rais aliyekejeliwa na kutusiwa kama Magufuli na mpaka sasa ukiangalia nyuzi humu ndani mtu anafungua tu kujaza kashfa kibao mpaka kumuita muuaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina hakika kama kuna Rais aliyekejeliwa na kutusiwa kama Magufuli na mpaka sasa ukiangalia nyuzi humu ndani mtu anafungua tu kujaza kashfa kibao mpaka kumuita muuaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maana nawasihi, tusisukumwe na hisia Wala hasira nawasihi Tena na Tena Rais wa nchi Ni taswira ya taifa lake, na sisi ndio tunatakiwa tumng'arishe kwa kumkosoa kwa staha na weledi, maana kwa Sasa Kila mwenye smartphone anaandika tusi au Jambo linaloonyesha kwamba watanzania hatuna maadili, Kama Ni kukosoa tukosoe Sana lakini Sio kwa lugha ya aibu na dhalili
 
Mkuu hiyo tabia unayoisema ndio umeanza kuiona hivi sasa? je huko nyuma umewahi kukemea? tuache unafiki,watanzania tumekuwa wananfiki na waongo sana.
 
Ukishaona mkosoaji anatumia lugha za hovyo basi ujue hana hoja yeyote ya msingi, mkosoaji mwenye hoja atatumia nguvu kubwa kuipambanua hoja yake ila asiye na hoja ya msingi huwa mkali au hutumia vitisho na lugha za kudhalilisha, ustaarabu kwe siasa za Afrika ni shida sana.
Basi hii ndio tabia ya machadema!

Kumbe huwa hayana hoja bhana
 
Wanaomkosea heshima Rais Samia ni vijana wa mataga ambao wana hasira ya kuondokewa na mpendwa wao Rais Magufuli.

Wengi tulishawahi kuonya kwamba kundi la mataga limejaa vijana wasioweza kufanya siasa za hoja.

Uwezo wa vijana wa mataga upo kwenye kupotosha, kutukana, kudhalilisha, na vurugu.
Na wale waliokuwa wanamkosoa Magu na kumtukana walikuwa watu gani?
 
Kwani kama iliwezekana kumtoa Nusrat ili wafanye udhalimu wao iweje iwe ngumu kuwatoa waliobambikiwa kesi haraka ili kuwatendea haki!?
Kuchelewesha HAKI ya Mtanzania yeyote yule kwa kutumia visingizio visivyo na kichwa wala miguu ni kuendeleza DHULUMA NA UDHALIMU dhidi ya Watanzania wasio na hatia.

hahahaha unataka naye aende kwa mtindo wa akina nusrat!?!. Calm down the president will take care of everything step by step kila mtu ana matamanio yake, yako hayajafikiwa kuwa subra yatafikiwa tu. kwa mfano mimi natamani uwepo mfuko wa unemplyoyed beneficial fund tusiokuwa na ajira serikali iwe inatupa posho kwa mwezi, sijakata tamaa, sina hasira, situkani, nina matumaini atanifikia
 
Leo hii mama mnamtambua Ni Rais aliyetokana na uchaguzi wa 2020 mnaosema CCM iliiba kura,? Na kumbe mnamtambua Ni Rais na mnahitaji msaada wake?

Sasa tunaomba busara ianzie kwako wewe kiongozi vingnevyo ukianza kuleta majigambo na shombo zako utaukimbia huu Uzi wako alaah!! Unahubiri adabu mwenyewe huna!!!..
 
Back
Top Bottom