Watanzania tumjulie hali Mr Nice

Watanzania tumjulie hali Mr Nice

Muungwana ugonjwa hauombwi ni kweli kabisa lakini una weza ukajitakia kuwa nao kama unavyo agiza msosi ulio chagua kwenye menu ila kumhurumia binadamu mwenzio ndio kilimwengu bwana mdogo alitumia wakati wake vibaya hilo halina uficho yaliyo baki ni kumtakia heri tu.
Kuna nguvu huwa zinatawala maisha yetu na ukibugi step kidogo tu umekwisha...binadamu tumenyimwa kitu kimoja kikubwa sana OUR NEXT MOMENT kama angejua yajayo nina hakika angeshafanya kitu
 
Hii leo kapost kwenye page yake ya facebook yuko kwao Rombo
ImageUploadedByJamiiForums1457101743.922488.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1457101757.407334.jpg
 
Mungu na amjalie uzima ili arudi kwenye game pindi akipona, lakini pia hilo linatakiwa kuwa somo kwake kwamba akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki mwema
 
Muungwana ugonjwa hauombwi ni kweli kabisa lakini una weza ukajitakia kuwa nao kama unavyo agiza msosi ulio chagua kwenye menu ila kumhurumia binadamu mwenzio ndio kilimwengu bwana mdogo alitumia wakati wake vibaya hilo halina uficho yaliyo baki ni kumtakia heri tu.
Enzi zake alikua ni pombe na madem na maneno ya kejeri,so wat u xpect? Sijui hata kama aliwahi kutoa msaada wowote kwa watoto yatima ,alikua na tabia mbaya hii nayo inachangia kukosa msaada,mungu ni mwingi wa rehema amponye na ajifunze
 
Watanzania tunakuwaje lakini?

Leo hii Mr Nice ni mgonjwa sisikii watanzania hasa vyombo vya habari pamoja na wasanii wakimfatilia kumjulia hali hata kujua anaendeleaje au hata yamkini kujua mahitaji ya ugonjwa wake angalau kusaidia kimnya.

Wanasubilia yakitokea ya kutokea utasikia redio station zote wanapiga nyimbo zake huku wakimwaga sifa kedekede kwake na maneno tuliyazoea ati pengo lake halitozibikaa Mara ohoo alikuwa mtu wa watu nk.

Magazeti nayo page zote za mbele zitapambwa na habari zake. Nasema kama mmekaa kimnya kipindi hiki mkae kimnya milele nisisikie. Mtauliza Mimi ni nani hill haliwahusu. Ila sio vema kuendelea na huu unafiki kwa mtualiyetoa vibao mmurua kama kuku kapanda baiskel bata kavaaa laizoni.

Nasema nanyi pia mliomtumia kipindi cha campaign 2005 Leo hii mmetupa hamna habari naye kabisaa. Wengine ni wasanii mko kimnya nasikia na nimeota wengine mmepewa mlungura wa million 50 hata kutoa kidogo kwa mwenzenu mko kimnyaa kabisaa.

Nimeona picha yake akiwa hospital hali yake si nzuri kwa maadili siwezi weka hapa ila anahitaji maombi yetu na kujitoa kwetu kusaidia sio yatokee ya kutoakea ndio tuanze unafiki Mara Ohoo alikuwa rafiki yangu pengo lake halitozibika, halitozibika bibi yako?

Shenzy

Wacha kulalama; take the initiative; anzisha utaratibu jinsi ya kumsaidia watu watakuunga mkono; kama anaumwa na kakaa kimya au anafanya siri wadau watajuaje?! Mbona mwili wa yule kijana aliyefariki India ulirudihwa na kuzikwa baada ya Baba yake kufunguka! Majuzi Ray C kafunguka kwenye runinga; leo hii keshapata usaidizi!? Jaribu kuwa sehemu ya ufumbuzi wa tatizo; usiwe tatizo au sehemu ya tatizo!
 
ule umoja wa wasanii uliosema kuwa wameandaa sherehe ya kumuaga Kikwete kwa pesa zao inaonyesha wana fungu la maana,
kwanini wasimege pesa kidogo wamlipie mwenzao matibabu??

Bongo kuna wasanii au magumashi? Mtu anakopi beats za watu (bongo fleva) anajiita msanii wakati ni pirate tu.
 
Ale vizuri, afanye mazoezi, apumzishe mwili wake. Akizingatia haya ataishi kwa.........
By the way anayo nafasi, kujiamini.
 
Wasanii wa bongo wamejaa unafiki na ubinafsi siku wakisikia amekufa watajazana na makamera utadhani wako location, maisha yao wengi ni ya kuigiza tu
 
[emoji86] [emoji87] [emoji87] [emoji87]
 
Kuna nguvu huwa zinatawala maisha yetu na ukibugi step kidogo tu umekwisha...binadamu tumenyimwa kitu kimoja kikubwa sana OUR NEXT MOMENT kama angejua yajayo nina hakika angeshafanya kitu
Ndio hivyo kwa bahati mbaya sana majuto huja baadae.
 
Enzi zake alikua ni pombe na madem na maneno ya kejeri,so wat u xpect? Sijui hata kama aliwahi kutoa msaada wowote kwa watoto yatima ,alikua na tabia mbaya hii nayo inachangia kukosa msaada,mungu ni mwingi wa rehema amponye na ajifunze
Amina, ila si ndio kejeli hizo zili mfanya akachezea sana vichapo.
 
Piga hoti umuombe Mungu wako haya sio ya kucheka wala kuyajadili humu
 
Piga hoti umuombe Mungu wako haya sio ya kucheka wala kuyajadili humu
ni kweli tupu.hakuna ajuaye kesho yake imebeba nini. la maana ni kutiana nguvu na kshauriana kutokukata tamaa . maadamu yu hai bado ana nafasi nzuri ya kuanza maisha upya kwani ana kipaji na uzoefu wa maisha. tumwombee mungu amtie nguvu na amwonyeshe njia.
 
" kikulaachooo kumbe ki nguoni mwako X2
Rafiki yaako kumbe adui yako eeh x2
Tuna kula nae, tuna kunywa nae kumbe mwenzangu Ana ona gereee o o o o...
Wanang'ata na kupuliza fuuu Kama panya buku wee..(hapa anaweka mdomo wake upande)"
Kila mpanda ngazi, hushuka.
Mali bila daftari, hupotea bila habari.
Mwenyezi Mungu ukinijaalia Mali, nijaalie pia akili ya kukumbuka kuweka akiba maana walimwengu Ni watu wabaya Sana, hawachelewi kukunanga ufuliapo!!
 
Back
Top Bottom