Pre GE2025 Watanzania Tumlinde na Kumtetea Kwa Nguvu zetu zote Rais Samia Zidi ya Waroho Wa Madaraka

Pre GE2025 Watanzania Tumlinde na Kumtetea Kwa Nguvu zetu zote Rais Samia Zidi ya Waroho Wa Madaraka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ukimlinda wewe peke Yako unatosha lakini watanzania tunaojitambua na wapenda maendeleo hatushawishiki kumlinda au kumtetea Kwa sababu nyingi ikiwemo kuwepo Kwa utekaji wa watu na kuuwawa hovyo kama alivyouawa mzee kibao
Mheshimiwa Rais amelaani sana tukio la kuuwawa kwa mzee All na ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike na kupewa ripoti kamili.Rais wetu ni mtu wa haki nl, mwenye moyo wa huruma,upendo , unyenyekevu mkubwa sana na mwenye hofu ya Mungu
 
Ndugu zangu Watanzania,

Sikatai na wala sipingi moja kwa moja kuwa changamoto ndogondogo hazipo hapa Nchini. Lakini ni ukweli ulio wa wazi kuwa sote tunaona na kushuhudia namna Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan anavyo pambana usiku na mchana kutatua na kumaliza kero mbalimbali .tunaona na kujionea dhamira yake njema katika kutukwamua na kutuinua kiuchumi.

Kupitia Mama yetu na Rais wetu Mpendwa Daktari Mama Samia Tunaona nuru katika nchi yetu,tunaona kesho yetu iliyo njema kuliko leo,tunaona Tumaini mbele yetu,tunaona mwanga katikati yetu,tunaona madaraja katikati ya changamoto ya kimaisha.tunaona namna Rais wetu anavyotuwezesha katika kutimiza ndoto zetu.

Tunaona namna anavyotufariji na kututia moyo na matumaini wakati wote.tunaona namna alivyo bega kwa bega na sisi na kwa kila hatua. Tunaona namna anavyoumizwa na matatizo yetu ,tunaona namna anavyofanya kila kitu kwa ajili yetu sote watanzania.

Anafanya hayo yote kwa ajili yetu watanzania,kwa ajili ya kututua mizigo,kwa ajili ya kutufuta machozi.anajitajidi kwa kadri ya uwezo wake Mama yetu kumfikia kila mmoja wetu kwa namna yake.

Embu fikiria ndugu zangu Taifa kama Marekani lililopata uhuru wake takribani karne mbili zilizopita yaani mwaka 1776 ,lakini leo ukikaa na kusikiliza sera ,ajenda na hata hoja za midahalo ya Mama Kamala Harris pamoja na Donald Trump unaweza kufikiria labda Taifa hilo lilipata uhuru wake pale nchi ya Sudani kusini ilipokuwa inajitenga kutoka Sudani ya kaskazini ya Omar Bashir wakati huo.

Unaweza kufikiria labda Marekani inayozungumziwa na akina Harris na Trump siyo ile iliyoongozwa na George Washington au Franklin Roosevelt au John F Kennedy au Harry Truman au Reonald Regan au Bill Clinton au Barack Obama .kwa sababu utaona Harris na Trump bado wanazungumzia habari za kutengeneza ajira kwa vijana kwa wingi,kuimarisha uchumi ,kupunguza kodi ,kupunguza gharama za matibabu na mengine mengi .

Sasa kama Marekani iliyopata uhuru wake zaidi ya miaka mia mbili na point iliyopita yaani miaka 248 iliyopita ,vipi kwa Tanzania ambayo imepata uhuru mwaka 1961 ikiwa haina wasomi,haina viwanda,haina barabara za lami,haina vyuo wala shule za kutosha ,haina umeme kwa mikoa mingi kama siyo yote,haina mifumo ya aina yoyote ile ya kueleweka ya taasisi mbalimbali? Vipi Tanzania hii iliyokuwa imejaa mamilioni ya watu wasio juwa kusoma na kuandika mwaka 61 ikose changamoto leo ndugu zangu?

Embu tumuungeni mkono Mama yetu Mpendwa kwa juhudi hizi kubwa anazofanya kuliinua Taifa letu kiuchumi. Tutampata wapi Mama Samia mwingine ndugu zanguni? Moyo wangu unaumia sana napoona kuna watu wanamshambulia hovyo bila sababu wala hoja za msingi.Naumia sana moyoni mwangu hasa kwa kuona namna Mama huyu alivyojitolea kuwatumikia watanzania halafu anajitokeza mwingine anaanza kumtolea lugha za matusi na kejeli..

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Naona Nchimbi anamzidi kete mama kuelekea 2025 CCM fanyeni kitu.
 
Kauli ya Dr nchimbi about vijana iliwahusu Sana mtu kama wewe

Unaongea kwenye mfumo wa huruma

Changamoto zipo eeh zinatatuliwaje?

Hayo ndio watu wanataka vijana mseme
Kwani wewe huoni namna zinavyotatuliwa?
 
Mheshimiwa Rais amelaani sana tukio la kuuwawa kwa mzee All na ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike na kupewa ripoti kamili.Rais wetu ni mtu wa haki nl, mwenye moyo wa huruma,upendo , unyenyekevu mkubwa sana na mwenye hofu ya Mungu

I think watu wahawana problem na Rais

Watu Wana problem na watendaji wa chini because wao ndio wanafanya haya mambo

Niliwahi kukwambia kuwa Tanzania ilitulia kabisa ila kuna mtu mmoja akaamua kuanzisha mambo ya kuweka ndani viongozi wa upinzani na alikuwa anajua kabisa nini kutafuata

Na ndio Leo tumefika hapa sasa

Watu wanatekwa watu wanauliwa, chuki Kwa police imekuwa kubwa kabisa
 
I think watu wahawana problem na Rais

Watu Wana problem na watendaji wa chini because wao ndio wanafanya haya mambo

Niliwahi kukwambia kuwa Tanzania ilitulia kabisa ila kuna mtu mmoja akaamua kuanzisha mambo ya kuweka ndani viongozi wa upinzani na alikuwa anajua kabisa nini kutafuata

Na ndio Leo tumefika hapa sasa

Watu wanatekwa watu wanauliwa, chuki Kwa police imekuwa kubwa kabisa
CCM ni wahusika wakuu wa huu utekaji
 
Back
Top Bottom