Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?

Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Mama Samia -Samehe tuu.png

Wanabodi,

Hii ni makala yangu ya Wiki hii ya Christmas.

Kunapotokea kosa lolote, mkosaji ana wajibu wa kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria, hivyo kinachoendelea sasa ni kwa sheria kuachwa kufuata mkondo wake, ila sasa kuna kelele nyingi, hivyo hili ni bandiko la swali.

"Watanzania tumshukuru sana Mungu kumpata kiongozi Mkuu mwenye moyo wa kusamehe, na roho ya samaha!. Jee tumuombe asamehe tuu hata bila ya kuombwa msamaha, au au tumwache shujaa wetu aendelee kukomaa nao kwa kusota gerezani hadi kieleweke?

Kuna wahusika wakuu watatu katika issue hii.
  1. Kuna Serikali imesema ina ushahidi wa uhusika wa mtuhumiwa fulani kupanga kutenda jinai ya ugaidi, ikaamua kutumia sheria kufuata mkondo wake, kuuthibitisha huo ugaidi, na ndicho kitu kinachoendelea mahakamani.
  2. Wakati kesi ikiendelea, kukajitokeza 'Askofu Makarios' wetu (Zitto Kabwe), akaomba nafuu za kisheria zitumike kumwachia mwenzao ili kuendelea na harakati za kisiasa na kidemokrasia kwa mustakabali mwema wa siasa za nchi yetu. Jibu lililopatikana ni "Kusamehe Kupo". Hili ni neno kubwa sana lenye maana kubwa, na thamani kubwa sana, na kitu kikubwa zaidi kuhusu neno hilo sio kutamkwa kwa matamshi ya neno hilo, bali ni moyo wa kusamehe alionao mtamkaji. Hili ni jambo la kushukuru sana, na kiukweli Watanzania, tumshukuru sana Mungu, kumpata mtu mwenye moyo wa kusamehe.
  3. Kuna Mtuhumiwa ni mtu mkubwa sana na mwenye heshima sana katika jamii, ni Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania, alikamatwa baada ya kuanza harakati za kudai Katiba mpya, hivyo wanachama wake, wafuasi wake, washabiki wake, wanaamini kabisa kuwa kiongozi wao sio gaidi, hiyo ya kesi ya kubambikiwa hivyo wanamchagiza asikubali suluhu yoyote au msamaha wa aina yoyote, kesi iendelee kusikilizwa hadi mwisho, ili mahakama ndio ithibitishe kuwa kiongozi wao ni gaidi au sii gaidi.
  4. Sote tunafahamu sisi binadamu ni viumbe dhaifu, hakuna mkamilifu, na kuna wakati, umdhanie ndie siye, na usiye mdhania kabisa, ukakuta ndie. Jee tumuombe tuu Mama asamehe tuu, hata kama mtuhumiwa hajaitambua jinai yake, na kuomba kusamehewa?. Kwa mujibu wa katiba yetu, sheria zetu, taratibu na kanuni, nchi yetu inaendeshwa kwa mihimili mitatu ya serikali, Bunge na Mahakama ambayo haipaswi kuingiliwa. Hivyo hapo kesi ilipofikia, hata kama Mama ana moyo wa kusamehe na yuko tayari kusamehe, akisamehe tuu kama ule msamaha wa Mwalimu Nyerere kumsamehe yule mshenzi aliyesema serikali yote ya Tanzania iko mfukoni kwangu, baada ya kuombwa na Askofu Makarios wa Cyprus, Mama atakuwa ameingilia uhuru wa mahakama.
  5. Mtu pekee mwenye nguvu hizo, uwezo huo na mamlaka hiyo kwa mujibu wa katiba yetu na sheria zetu, taratibu na kanuni ni DPP, ila nae anatakiwa kufanya kazi independently bila kuingiliwa na yeyote, ila Mama akiamua, DPP atafanya kinachopaswa kufanyika!.
  6. Mwalimu Nyerere alikuwa ni mtu mwenye moyo wa msamaha, ila alikuwa ni mtu mkali sana kwenye mambo ya kijinga jinga. Katika utawala wake wa miaka 22, alisweka watu wengi tuu kizuizini, ila katika utekelezwaji wa hukumu ya kifo kwa kunyongwa hadi kufa, Mwalimu Nyerere alisaini death warrant mbili tuu, ile ya Mwamwindi, na yule mhindi aliyeua mke na kuteketeza familia ili alipwe bima!.
  7. Kwenye hili la moyo wa kusamehe, naomba nisilizungumze kipindi cha Mwinyi, wale waliojiriwa kwa kazi kunyonga mpaka kufa, hawakukaa bure, angalau angalau walitimiza wajibu wao.
  8. Kipindi cha Mkapa kiukweli sijui.
  9. Kipindi cha JK, pia alikuwa ni mtu mwenye huruma na moyo mkubwa sana wa kusamehe, aliyasamehe hadi yale majizi ya EPA!.
  10. Naomba nisiizungumzie awamu ya JPM for obvious reasons, yaliyopita sii ndwele, tugange haya yaliyopo ya Mama mwenye roho ya kusamehe na yajayo ya kujenga Tanzania njema ya kuameheana.
My Take.
  1. Kunamsemo wa kizungu, usemao, "you can't eat your cake and have it", you either eat your cake na iishe, its gone, au usiile, uingalie tuu iendelee kuwepo, ila hapa natoa ushauri, unaweza kuila keki yako na ikaendelea kuwepo kwa kuimega kidogo kido na sio kuibugia. Maadam sheria ni zetu na tumezitunga wenyewe, ili kuziridhisha pande zote, tunaweza kuimega kidogo kidogo keki yetu na kuila huku ikiendelea kuwepo.
  2. Japo lengo la watu kuwekwa mahabusu ni ili kuwazuia wasitoroke na kuna baadhi ya makosa hayana dhamana, ili mtuhumiwa asitutoroke, tuambiane ukweli, hivi Mbowe anaweza kweli kutoroka nchi na kukimbilia uhamishoni aende kuwa mkimbizi wa kisiasa kama wale waoga wawili?. Kama hata kwenye kesi za mauaji hakuna dhamana, lakini kesi ya Ditopile aliyekuwa anatetewa na wakili Nimrodi Mkono, Wakili Mkono, alijenga hoja maridhawa, Ditopile akaachiwa kwa dhamana hadi pale Mungu alipoamua kumalizana nae. Hivyo kama tuna nia njema, Mbowe awe huru, anaweza kuachiwa kwa dhamana hata bila dhamana hiyo kuombwa, akawa anakuja kuhudhuria kesi akitokea nyumbani kwake.
  3. Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana! Hongera sana, kazi umeianza vizuri. Sasa haki sio tu inatendeka, inaonekana! Kazi Iendelee…
    2814589_Kwa_Maslahi_ya_Taifa_Hongera_DPP_Mpya.jpeg
  4. Kwa kufanya hivi, tutakuwa tumejibu ombi la 'Askofu Makarios' wetu na wale wote wenye nia njema na mapenzi mema kwa Mbowe kuwa jela ni mbaya, hivyo atakuwa huru uraiani kuungana na familia yake, ndugu jamaa na marafiki, na hata kusafiri kwenda kuhiji Moshi kwenye ile hija maarufu ya Wachagga ya Mwezi Desemba, na hata akiamua kusafiri kidogo hadi Arusha, kupitia Kisongo, kumsalimu yule 'jamaa yetu'.
  5. Huku hii kesi ya Mbowe, ikiendelea kuna mawili,
    1. Serikali inaweza kabisa kuwa imeona inakwenda kushindwa kwa aibu na fedheha, hivyo ili kuepuka aibu ya kushindwa kwa fedheha, hivyo DPP, anaweza kupeleka Nolle. Hili lilifanyika, litamfanya Mbowe kuonekana shujaa, na akiachiwa kwa Nolle, huo moto wake ni usipime!.
    2. Mahakama inaweza kabisa ithibitishe Mbowe ni malaika, hivyo alikuwa anasingiziwa tuu, ugaidi, hapo serikali itafedheheka.
    3. Ili kuzuia serikali isifedheheke, hata kama in reality Mbowe sio gaidi lakini ili kumuadabisha, then ni lazima atatiwa hatiani na sheria ichukue mkondo wake kwa kula mvua kadhaa, na hapa sasa ndipo mahali Mama Samia mwenye uwezo napo kwa kutoa msamaha kwa wafungwa. Mbowe ataachiwa shingo chini, hataweza kugombea kitu chochote.
Wanabodi, mnalionaje hili?. DPP afute kesi kwa Nolle, Mbowe aachiwe bila masharti yoyote, Asamehewa tuu bila kuomba msamaha, aachiwe kwa dhamana kesi iendelee, au aendelee kukomaa kama Mandela, no retreat no surrender, akamae nao mpaka kieleweke?

Nawatakia Krismasi Njema.

Paskali.
 
Nakumbuka hata Magufuli nae alikuwa anasamehe, ukirudisha pesa ulizoiba (kama ni kweli) alikuwa anasamehe.

Huyu nae naona anataka kusamehe, lakini hatujui yeye anataka kusamehe kwa kosa gani alilotendwa yeye binafsi au nchi.

Na yule kule gerezani nae anayaka maelezo, kosa lake ni lipi mpaka atafutiwe msamaha na watu wa pembeni, anataka kwanza kulijua kosa lake, ili ikitokea akawaomba msamaha na mkamsamehe, basi asije kulirudia.
 
Huyu Jamaa Ni mnafiki, msamaha utanguliwa na kosa, wewe ndo umethibitisha kosa? Anasamehewa nini? Mbona wewe Jamaa umekuwa mtu wa hovyo Sana?

Anayeumia Ni Mbowe, Kama anajua Ana kosa si angeomba msamaha? Pascal hata Kama una njaa, please upgrade njaa yako, maana njaa yako Kama Ni window basi Ni XP.
 
Huyu Jamaa Ni mnafiki, msamaha utanguliwa na kosa, wewe ndo umethibitisha kosa? Anasamehewa nini? Mbona wewe Jamaa umekuwa mtu wa hovyo Sana?

Anayeumia Ni Mbowe, Kama anajua Ana kosa si angeomba msamaha? Pascal hata Kama una njaa, please upgrade njaa yangu, maana njaa yako Kama Ni window basi Ni XP.
Pascali anazeeka vibaya sana tena hana aibu
 
Watanzania wengi walikuwa wanakitazama CHADEMA kama chama mbadala kinachoweza kupambana na CCM lakini CDM kushirikiana na wanaharakati kupandikiza CHUKI na kugawa watanzania kimepoteza ushawishi. Wananchi wanataka mabadiliko sio visasi na Chuki.
 
Yote matatu yanawezekana na yanaingia akilini kwa kila anaedhani yupo sawa, yaani wa kusamehewa,wakiachiliwa kwa dhamana,na wa kufutiwa kesi .

Ila tujuwe mbowe katika hayo yanayotajikana kwake kwenye kesi hii hakosi uhusika kwa namna moja ama nyingine,ukweli anaujua yeye.

Hivyo maoni yangu kesi ifutwe tu tuangalie mengine.
 
Kama walishawahi kutokea Tanzania 🤑🤑🤑 watu wenye shahada ya unafiki basi watu hao ni Zitto na Mayalla. Mayalla siku zote huwa anaandika kutokana na mwelekeo wa kile anachokipenda na wala siyo kutokana na mwelekeo wa ukweli. Sijawahi kumuona mzee 🤣🤣🤣 anayeishi kishabiki kama huyu
 
CHADEMA Original kipindi cha kina Dr. Slaa wakiwa mwiba kwa serikali kwa kuibua ubadhirifu wa mali za umma, wizi, ufisadi kila Mtanzania aliona ni chama cha UKOMBOZI.
Tunasikitika CDM sasa inaendeshwa SPACE na CLUB HOUSE na wanaharakati kila kukicha porojo TU. Huwa nashangaa huko SPACE Lema, ndiyo msemaji mkuu hamna cha maana.
 
Mbowe amekaa jela kwa zaidi ya siku Mia moja. Mara kadhaa amenyimwa haki yake ya kupatiwa chakula, mara kadhaa kikatili kabisa amenyimwa haki yake ya kutembelewa na wafariji, ushahidi unaotolewa tunauona, maamuzi ya jaji ya uendeshaji kesi tunayaona, maelekezo ya jaji mkuu tumeyasikia, wakamatiji tumewasikia na tumewaona, tulimwona mama akimhukumu Mbowe ni gaidi BBC, na amerudia tena juzi baada ya maombi ya Zitto.

Kuna mahakama tatu zinafuatilia kesi hii:
1. Mahakama ya jaji aliyechaguliwa na mshindani mkuu wa Mbowe, jaji huyu anapokea ushahidi kutoka kwa askari waliopatiwa vyeo na mshindani mkuu wa Mbowe. Jaji na polisi hawa wanalipwa malipo makubwa ya fedha ulinzi na malazi wakati wanatimiza majukumu yao. Lengo la kubwa ni kuthibitisha mama aliposema Mbowe ni gaidi hakudanganya.
2. Mahakama ya UMMA, hawa wapo dunia nzima, hawana malipo ya fedha, malazi au ulinzi. Hawa mwanzo hawakujua kama Mbowe ni gaidi au la. Lakini kadiri kesi inavyoendelea wamejifunza mengi. Tayari wanayo hukumu yao. Hukumu yao si lazima ifanane na ya jaji mteule wa rais anaekula na kusaza.
3. Mahakama ya Mungu huyu anajua kila kitu hata kabla kesi haijaanza. Mawazo yangu kesi iendelee.
 
Back
Top Bottom