Watanzania tumuombee Dkt. Tulia Ackson ashinde Urais wa IPU

Ndugu yangu sikiliza .hapa ni jukwaa huru na mahali huru la mijadala.huwezi ukakubaliana na mada zote zinazoandikwa hapa lakini pia wote kwa pamoja hatuwezi kuwa sawa katika mitizamo juu ya jambo fulani.lakini pia kama unaona mimi nina sifia sana basi ni nafasi yako kutumia jukwaa hili kukosoa pale unapoona mimi nimepotosha.fanya hayo kwa hoja na siyo kuandika tu pasipo ushahidi au kuandika kwa kumshambulia mtu kwa chuki zako binafsi tu.
 
Mwashamba acha kuaibisha ukoo wenu.Kila kukicha wewe ni uchawa tu.Kwa mwendo huu teuzi utazisikia kwenye bomba.Unaonekana kituko.
 
Akishinda mwananchi wa Mwanjelwa atanufaikaje na ushindi wake?
 
Ni wapi alipokosea Dr Tulia anapostahili kulaumiwa? Kwani kosa lake ni lipi wakati kilichopitishwa awali ndicho hicho kimekuja kuzaa mkataba bora na wenye kuzingatia maslahi ya Taifa.? Aliyokuwa anayesema Dr Tulia majukwaani ndio yaliyotokea.Dr Tulia alitutoa hofu watanzania juu ya mkataba ule na kutwambia kuwa hakuna Bandari zetu zilizouzwa kama ambavyo wapotoshaji walikuwa wanasema.je huoni kuwa Dr Tulia alikuwa sahihi na msema kweli?
 
Mwashamba acha kuaibisha ukoo wenu.Kila kukicha wewe ni uchawa tu.Kwa mwendo huu teuzi utazisikia kwenye bomba.Unaonekana kituko.
Kwani kuongea ukweli kuna Ainisha vipi ukoo wangu? Au nani kasema naandika hapa kwa niaba ya ukoo? Nani kasema nimetumwa hapa na ukoo kuandika hapa? Ukoo na maandishi yangu yanaingilia vipi?
 
Wewe kapimwe akili,siku si nyingi utaanza kula majalalani.
 
Huyo ajuza wa kinyakyusa akishinda si ndo tutakuwa hatupumui jamani kha
 
Kwa nini aombewe?Hajiwezi kupambana?
 
Kwa nini aombewe?Hajiwezi kupambana?
Tunapaswa kwa umoja wetu kumuombea.naamini hata yeye anaendelea kumwomba Mungu ili amsaidie lakini hata sisi kila mmoja wetu kwa imani yake tunapaswa kumuombea Dr Tulia. palipo na wawili Mungu yupo katikati yao.katikati ya maombi yetu kama Taifa naamini Mungu atamuinua Dr Tulia.
 
Kwa Neema na Baraka za Mungu, atashinda kwa kishindo...
 
Huyo ajuza wa kinyakyusa akishinda si ndo tutakuwa hatupumui jamani kha
Acha matisi wewe.Dr Tulia ni kiongozi mwenye hofu ya Mungu na huruma sana.ndio maana kupitia yeye vijana wengi sana mkoani Mbeya wamewezeshwa mitaji,kupewa bodaboda na bajaji kwa ajili ya kuendesha biashara na kujipatia kipato cha kuendeshea maisha yao.amewapa na kusaidia vikundi vya akina mama.amesaidia yatima na hata wazee wenye kuhitaji msaada na kusaidiwa. Dr Tulia amegusa maisha ya watu wengi sana na kuleta Tabasamu.maisha yake Dr Tulia yamekuwa ni neema kwa wengi.
 
Leo ndo umejua Tulia;
Ni binadamu,
Hajakamilika,
Anakosea?
Huyu unayemuita shujaa wa Uuzaji bandari naye kumbe anakosea?
Baki na watakatifu wenzio kina Tulia mjiombee wenyewe na mungu wenu mnayemjua atawasikiliza.
Hatuwezi kuwa shirika na watesi wa Watanzania, waliojimilikisha nchi na kujiona wao ni raia wa daraja la Kwanza nchini.
 
Kwa Neema na Baraka za Mungu, atashinda kwa kishindo...
Hakika Mungu wetu aliye muweza wa yote na vyote atamsaidia na kumuwezesha Dr Tulia kushinda kinyang'anyiro hiki cha kuwania nafasi ya urais wa umoja wa mabunge Duniani.
 
Mwombee WEWE
 
Kati ya watu wasiojielewa huyo ni wakwanza.... Kama ana ID humu mtag tuuu ajue ukweli wake

Hatuwezi kuwa na mwanasiasa au mwalimu asiye na msimamo akajulikana yuko mrengo gani?

Wakati wa magu alikuwa kushoto sasa yupo kulia kesho kutwa yupo kati
 
Unamuombeaje kama ana uwezo?Au neno "kuombea" limebadilishwa maana siku hizi?Ushauri:-
1-Aende na Nape wakimbie na masanduku ya kura,
AU
2-Akeshe akisali wakinzani wake wawe hawajui kusoma na kuandika
AU
3-Afufuliwe mtu "yeyote" ampitishe bila kipingamizi.
 
Ukimuombea wewe inatosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…