kina kirefu
JF-Expert Member
- Dec 14, 2018
- 15,188
- 18,583
Punguza wehu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Msamehe ni mama mjane anatafuta namna ya kujikimuHili chawa linakera sana
Anajaza server ya watu ujinga wake, wao UWT wamuombee mwanamke mwenzaoAcha kujaza server
Kwa wewe maombi yako hayahitaji maana wewe tu hapo ulipo tupo kwenye maombi ya kukuombea ili upone ukichaa wako na kurejea katika akili yako ya kawaida.maana hali uliyofikia kwa sasa ni mbaya sana inayohitaji matibabu ya dharula sana kabla kichaa chako hakijawa kikubwa kama cha SAGAI GALGANO.Bora nimuombee mbwa wangu kuliko kumuombea shetani na kazi zake
Tuliwahi kuwa Na rais huko alitupa faida gani ?Ni faida kwa Taifa letu zima, sauti zetu zitaendelea kusikika Duniani kwote, ni heshima kwa Taifa kuwa na uwakilishi huo wa ngazi ya juu kabisa, Tutaendelea kujenga na kujijengea ushawishi Duniani kwote kwa mambo mbalimbali.
Akina mama wa UWT mtajifunza lini kiswahili?Kwa wewe maombi yako hayahitaji maana wewe tu hapo ulipo tupo kwenye maombi ya kukuombea ili upone ukichaa wako na kurejea katika akili yako ya kawaida.maana hali uliyofikia kwa sasa ni mbaya sana inayohitaji matibabu ya dharula sana kabla kichaa chako hakijawa kikubwa kama cha SAGAI GALGANO.
Ni ujinga tupu wala hakuna la maanaTuliwahi kuwa Na rais huko alitupa faida gani ?
Hakuna MUNGU mjinga kiasi hicho wa kupokea maombi ya kijinga ajili ya watu wa ovuMimi namwombea siku zote na naendelea kumwombea kwa Mungu wakati wote na nawaombeni nanyi watanzania wenzangu tumwombee Dr Tulia kuweza kushinda nafasi hii ya Urais wa IPU.
Kwanza asirudi huku hatumtaki huyo ajuza na sura ake mbayaAsipate hata Kira moja....
Achana na huyo chiziKama mpaka sasa hujajua kuwa kuna wauaji na majambazi wa raslimali Tanzania basi wewe ndiye jini uliyekuwa unatumwa kuua!
Alieiba kura .naomba usiende tena kanisan kwa neno hiloTulia atashinda tu ni speaker makini ila wewe hupati utezi 😅
Ikishinda umeme hakuna mgao eti wewe pimbiNdugu zangu Watanzania,
Pamoja na kwamba Dr Tulia ni mgombea mwenye sifa kubwa kuliko wagombea wenzake, anayeungwa mkono na jumuiya mbalimbali, anayepewa nafasi ya kuibuka mshindi kwa kishindo, pamoja na kuwa na elimu yake kubwa, lakini Mungu anabaki kuwa Mungu tu. Mungu anabaki kuwa ndiye muamuzi wa mwisho, ndiye mtoa uongozi na ndiye muonyesha njia.
Ndiye mchora ramani ya ushindi, ndiye anayeweza kufanya watu wakamchagua yeye na kuwaacha wengine, ndiye anayeweza kukupa kibali cha kukubalika na kupendwa mbele za watu, ndiye anayeweza kukupa ushindi, ndiye anayeweza kukushindia vita yako ambayo unaiona ni ngumu mbele zako na ikawa nyepesi na ndiye anayeweza kugeuza mioyo ya watu ikakukubali wewe tu.
Ndio maana mimi binafsi kwa kutambua uwezo wa Mwenyezi Mungu katika kila jambo, nimeona na kuwiwa moyo wangu kwa unyenyekevu mkubwa sana kuwaombeni Watanzania wenzangu kwa umoja wetu tupige magoti Tumuombee Dr Tulia Ashinde vita hii ambayo ipo mbele yake ya kuwania nafasi ya Urais wa umoja wa mabunge Duniani. Inawezekana kwa namna moja au nyingine kuna watu Ambao wangekataa kumuombea Dr Tulia kwa sababu za kisiasa au kupishana kwa hali ya kawaida tu ya kibinadamu.
Lakini ningependa kusema neno moja kuwa Dr Tulia ni mwanadamu kama sisi, kama mimi na wewe au wewe na yule. Hajakamilika na hakuna mwanadamu aliyekamilika chini ya jua, hakuna aliye mtakatifu, hakuna asiye kosea, hakuna ambaye hajawahi kosea, hakuna ambaye hakosei. Kwa hali hiyo hata Dr Tulia kuna uwezekano kuna watu amewakosea, amewakwaza, amewaudhi na kuwaumiza kwa namna moja au nyingine kwa maamuzi, matendo, au kauli. Hayo ni mambo ya kawaida kwa mwanadamu na hatuna budi kusameheana.
Jiulize wewe ulipo hapo umewakosea wangapi? Umewakwaza wangapi? Umewaliza machozi wangapi kwa bahati mbaya? Umesamehewa na Mungu wako mara ngapi? Vipi kama kila kosa ungehukumiwa na kupunguziwa hazina ya miaka yako ya kuishi hapa Duniani au pumzi yako katika mtungi wako binafsi? Nani angesalimika? Nani hazina yake ya miaka ingekuwa palepale? Je Dr Tulia siyo mwanadamu? Hakosei? Kwanini tusimsamehe alipotukosea? Kwanini tusizike tofauti zetu na kuungana kama Taifa kimaombi kumuombea kwa Mungu ushindi Dr Tulia ili Mungu amshindie vita hii na kumpa kibali cha Ushindi?
Akishinda Dr Tulia Taifa limeshinda, Watanzania tunakuwa tumeshinda na sote tutakuwa ni washindi. Binafsi namuombea sana huyu Dada yangu. Nitafurahi sana Taifa letu likishinda nafasi hii kupitia Dr Tulia. Kila mmoja kwa imani yake tuendelee kumuombea sana Dr Tulia. Tuweke pembeni tofauti zetu za kisiasa na kusimama pamoja na Dr Tulia kwa kuwa anawakilisha Taifa letu na siyo chama.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.
Alieiba kura .naomba usiende tena kanisan kwa neno hilo