Watanzania tumuombee Dkt. Tulia Ackson ashinde Urais wa IPU

Watanzania tumuombee Dkt. Tulia Ackson ashinde Urais wa IPU

Dr Tulia yupo juu ya vigezo .kwa kuwa kama ni suala la uwezo wa kiuongozi,Elimu,uzoefu, maarifa na uwezo wa kujenga hoja anavyo vyote. Dr Tulia amekamilika kila idara.ndio maana anakubalika na kuungwa mkono kutoka jumuiya zote na kanda zote.
Uwezo Hana ila elimu anayo ya makaratasi tu. Zamani kulikuwa na fursa kibao za kusoma tena Bure hata kama ni kilaza unalazimishwa tu usome. Mfano ni tulia kichwani Hana kitu kabisa ila ni PhD. Angalia Jana hata kingereza chake ni kibovu sana
 
Uwezo Hana ila elimu anayo ya makaratasi tu. Zamani kulikuwa na fursa kibao za kusoma tena Bure hata kama ni kilaza unalazimishwa tu usome. Mfano ni tulia kichwani Hana kitu kabisa ila ni PhD. Angalia Jana hata kingereza chake ni kibovu sana
Hivi unafikiri kuna mbumbumbu wa aina yako anaweza kupata fursa ya kusomea na kufundisha sheria chuo kikuu cha Dar es salaam? Unafirikiri Kama wewe ni mweupe unaweza kufaulu shule kuu ya sheria pale mlimani? Dr Tulia ni akili kubwa na mwenye uwezo mkubwa sana wa kupambanua mambo,ndio maana unaona jana namna alivyo wakosha wajumbe wote wa IPU wakati akitoa hotuba yake ya kiwango cha kimataifa yenye ubora ulioweka historia.
 
🚮🚮🚮🚮 uzalendo upi wa kudalalia rasilimali za Taifa letu
 
Huyu chawa sijawahi kuusoma uzi wake nikaumaliza, nikiuona uzi wake najua ni usenge mtupu... Mtoto wa kiume unajipendekeza kisengesenge
 
Mungu mkubwa sana na tunaendelea kumshukuru sana kwa upendo wake kwa mh Dr Tulia Acksoni mwansasu. Kwa hakika ni kwa neema ya Mwenyezi Mungu mpaka kufika hapo alipofika leo Dr Tulia.sifa na Utukufu Tunamrudishia Mwenyezi Mungu.
Kashinda kwa zaidi ya asilimia 57 huyu Mwanamama ana kitu atafika mbali
 
Roho mbaya tu zinawasumbua hasa baada ya matarajio yao kwenda mrama.walitegemea Dr Tulia ashindwe lakini kwa bahati mbaya imekuwa tofauti,kwani Dr Tulia amefanikiwa kuteka mioyo ya mamia ya wajumbe wa IPU na kupata uungwaji mkono wa kishindo.
Hata wewe una roho mbaya kwasababu hata wewe kuna watu huwa hupendi washinde!
 
Uwezo Hana ila elimu anayo ya makaratasi tu. Zamani kulikuwa na fursa kibao za kusoma tena Bure hata kama ni kilaza unalazimishwa tu usome. Mfano ni tulia kichwani Hana kitu kabisa ila ni PhD. Angalia Jana hata kingereza chake ni kibovu sana
Ukichaa huu,Hajawahi kutokea kilaza akiyesoma Law UD kamtafute pengine sio hilo chimbo.
 
Ukichaa huu,Hajawahi kutokea kilaza akiyesoma Law UD kamtafute pengine sio hilo chimbo.
Achana na huyo mshamba .yeye anafikiria unaweza ukasoma sheria udsm na kumaliza salama bila kuliwa kichwa kama ni kichwa cha panzi .
 
Ndugu zangu Watanzania,

Pamoja na kwamba Dr Tulia ni mgombea mwenye sifa kubwa kuliko wagombea wenzake, anayeungwa mkono na jumuiya mbalimbali, anayepewa nafasi ya kuibuka mshindi kwa kishindo, pamoja na kuwa na elimu yake kubwa, lakini Mungu anabaki kuwa Mungu tu. Mungu anabaki kuwa ndiye muamuzi wa mwisho, ndiye mtoa uongozi na ndiye muonyesha njia.

Ndiye mchora ramani ya ushindi, ndiye anayeweza kufanya watu wakamchagua yeye na kuwaacha wengine, ndiye anayeweza kukupa kibali cha kukubalika na kupendwa mbele za watu, ndiye anayeweza kukupa ushindi, ndiye anayeweza kukushindia vita yako ambayo unaiona ni ngumu mbele zako na ikawa nyepesi na ndiye anayeweza kugeuza mioyo ya watu ikakukubali wewe tu.

Ndio maana mimi binafsi kwa kutambua uwezo wa Mwenyezi Mungu katika kila jambo, nimeona na kuwiwa moyo wangu kwa unyenyekevu mkubwa sana kuwaombeni Watanzania wenzangu kwa umoja wetu tupige magoti Tumuombee Dr Tulia Ashinde vita hii ambayo ipo mbele yake ya kuwania nafasi ya Urais wa umoja wa mabunge Duniani. Inawezekana kwa namna moja au nyingine kuna watu Ambao wangekataa kumuombea Dr Tulia kwa sababu za kisiasa au kupishana kwa hali ya kawaida tu ya kibinadamu.

Lakini ningependa kusema neno moja kuwa Dr Tulia ni mwanadamu kama sisi, kama mimi na wewe au wewe na yule. Hajakamilika na hakuna mwanadamu aliyekamilika chini ya jua, hakuna aliye mtakatifu, hakuna asiye kosea, hakuna ambaye hajawahi kosea, hakuna ambaye hakosei. Kwa hali hiyo hata Dr Tulia kuna uwezekano kuna watu amewakosea, amewakwaza, amewaudhi na kuwaumiza kwa namna moja au nyingine kwa maamuzi, matendo, au kauli. Hayo ni mambo ya kawaida kwa mwanadamu na hatuna budi kusameheana.

Jiulize wewe ulipo hapo umewakosea wangapi? Umewakwaza wangapi? Umewaliza machozi wangapi kwa bahati mbaya? Umesamehewa na Mungu wako mara ngapi? Vipi kama kila kosa ungehukumiwa na kupunguziwa hazina ya miaka yako ya kuishi hapa Duniani au pumzi yako katika mtungi wako binafsi? Nani angesalimika? Nani hazina yake ya miaka ingekuwa palepale? Je Dr Tulia siyo mwanadamu? Hakosei? Kwanini tusimsamehe alipotukosea? Kwanini tusizike tofauti zetu na kuungana kama Taifa kimaombi kumuombea kwa Mungu ushindi Dr Tulia ili Mungu amshindie vita hii na kumpa kibali cha Ushindi?

Akishinda Dr Tulia Taifa limeshinda, Watanzania tunakuwa tumeshinda na sote tutakuwa ni washindi. Binafsi namuombea sana huyu Dada yangu. Nitafurahi sana Taifa letu likishinda nafasi hii kupitia Dr Tulia. Kila mmoja kwa imani yake tuendelee kumuombea sana Dr Tulia. Tuweke pembeni tofauti zetu za kisiasa na kusimama pamoja na Dr Tulia kwa kuwa anawakilisha Taifa letu na siyo chama.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
UMUOMBEE ILI IWEJE? ILI USAIDIKE KIVIPI?
 
Back
Top Bottom