Watanzania tumuombee Dkt. Tulia Ackson ashinde Urais wa IPU

Watanzania tumuombee Dkt. Tulia Ackson ashinde Urais wa IPU

Kati ya watu wasiojielewa huyo ni wakwanza.... Kama ana ID humu mtag tuuu ajue ukweli wake

Hatuwezi kuwa na mwanasiasa au mwalimu asiye na msimamo akajulikana yuko mrengo gani?

Wakati wa magu alikuwa kushoto sasa yupo kulia kesho kutwa yupo kati
Msimamo wa Dr Tulia ni mmoja tu siku zote ambao ni kutanguliza mbele maslahi ya Taifa na kuwatumikia watanzania wote kwa usawa na haki. Amedhihirisha hayo kwa matendo na kauli zake.katika hilo hayumbi wala kuyumbishwa hata kidogo.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Pamoja na kwamba Dr Tulia ni mgombea mwenye sifa kubwa kuliko wagombea wenzake, anayeungwa mkono na jumuiya mbalimbali, anayepewa nafasi ya kuibuka mshindi kwa kishindo, pamoja na kuwa na elimu yake kubwa, lakini Mungu anabaki kuwa Mungu tu. Mungu anabaki kuwa ndiye muamuzi wa mwisho, ndiye mtoa uongozi na ndiye muonyesha njia.

Ndiye mchora ramani ya ushindi, ndiye anayeweza kufanya watu wakamchagua yeye na kuwaacha wengine, ndiye anayeweza kukupa kibali cha kukubalika na kupendwa mbele za watu, ndiye anayeweza kukupa ushindi, ndiye anayeweza kukushindia vita yako ambayo unaiona ni ngumu mbele zako na ikawa nyepesi na ndiye anayeweza kugeuza mioyo ya watu ikakukubali wewe tu.

Ndio maana mimi binafsi kwa kutambua uwezo wa Mwenyezi Mungu katika kila jambo, nimeona na kuwiwa moyo wangu kwa unyenyekevu mkubwa sana kuwaombeni Watanzania wenzangu kwa umoja wetu tupige magoti Tumuombee Dr Tulia Ashinde vita hii ambayo ipo mbele yake ya kuwania nafasi ya Urais wa umoja wa mabunge Duniani. Inawezekana kwa namna moja au nyingine kuna watu Ambao wangekataa kumuombea Dr Tulia kwa sababu za kisiasa au kupishana kwa hali ya kawaida tu ya kibinadamu.

Lakini ningependa kusema neno moja kuwa Dr Tulia ni mwanadamu kama sisi, kama mimi na wewe au wewe na yule. Hajakamilika na hakuna mwanadamu aliyekamilika chini ya jua, hakuna aliye mtakatifu, hakuna asiye kosea, hakuna ambaye hajawahi kosea, hakuna ambaye hakosei. Kwa hali hiyo hata Dr Tulia kuna uwezekano kuna watu amewakosea, amewakwaza, amewaudhi na kuwaumiza kwa namna moja au nyingine kwa maamuzi, matendo, au kauli. Hayo ni mambo ya kawaida kwa mwanadamu na hatuna budi kusameheana.

Jiulize wewe ulipo hapo umewakosea wangapi? Umewakwaza wangapi? Umewaliza machozi wangapi kwa bahati mbaya? Umesamehewa na Mungu wako mara ngapi? Vipi kama kila kosa ungehukumiwa na kupunguziwa hazina ya miaka yako ya kuishi hapa Duniani au pumzi yako katika mtungi wako binafsi? Nani angesalimika? Nani hazina yake ya miaka ingekuwa palepale? Je Dr Tulia siyo mwanadamu? Hakosei? Kwanini tusimsamehe alipotukosea? Kwanini tusizike tofauti zetu na kuungana kama Taifa kimaombi kumuombea kwa Mungu ushindi Dr Tulia ili Mungu amshindie vita hii na kumpa kibali cha Ushindi?

Akishinda Dr Tulia Taifa limeshinda, Watanzania tunakuwa tumeshinda na sote tutakuwa ni washindi. Binafsi namuombea sana huyu Dada yangu. Nitafurahi sana Taifa letu likishinda nafasi hii kupitia Dr Tulia. Kila mmoja kwa imani yake tuendelee kumuombea sana Dr Tulia. Tuweke pembeni tofauti zetu za kisiasa na kusimama pamoja na Dr Tulia kwa kuwa anawakilisha Taifa letu na siyo chama.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Uzalendo kwako ni kuunga mkono wauaji, wanyonya damu, wasaliti na wauzaji wa raslimali za nchi??
 
Ila JF imekuwa kituko. Ndio maana inapoteza hadhi yake. Machawa wamejaa humu wanaandika ujinga. Tumewahi kuwa na Naibu Karibu Mkuu wa UN Asha Rose Migiro alitusaidia Nini?. Hicho cheo ni kuajili ya yeye kula na sio kwa manufaa ya wananchi.
 
Uzalendo kwako ni kuunga mkono wauaji, wanyonya damu, wasaliti na wauzaji wa raslimali za nchi??
Usipende kuongea vitu usivyokuwa na ushahidi navyo. Unaweza ukaniambia na kueleza kwa ushahidi ni nani muuwaji na alimuuwa nani?
 
Ila JF imekuwa kituko. Ndio maana inapoteza hadhi yake. Machawa wamejaa humu wanaandika ujinga. Tumewahi kuwa na Naibu Karibu Mkuu wa UN Asha Rose Migiro alitusaidia Nini?. Hicho cheo ni kuajili ya yeye kula na sio kwa manufaa ya wananchi.
Wewe huwezi kuelewa kitu chochote kile kwa kuwa tayari ulishajipatia upofu wa akili na macho. Ndio maana hata ukielezwa faida zake hutaelewa bado. Ili uelewe ni mpaka upewe kwanza matibabu ya upofu wako wa akili na macho.
 
Wewe SAGAI GALGANO ndiye unatakiwa kuendelea kupimwa akili mara kwa mara ili kuangalia ni dawa gani itakuponya matatizo yako ya akili na kurejea katika hali yako ya kawaida.
Nimeshawasiliana na ndugu zako wakupeleke mirembe,na wamekubaliana na mimi,wewe hujijui tu lakini umesharukwa akili. Ni kama vile mtu ukilaaniwa huwezi kujijua ila watu wa karibu yako ndiyo wanajua kuwa tayari umeshaharibikiwa.
 
Back
Top Bottom