Watanzania tumuombee Nchimbi: sasa naelewa mtifuano ndani ya CCM ni ukombozi kwa Taifa

Watanzania tumuombee Nchimbi: sasa naelewa mtifuano ndani ya CCM ni ukombozi kwa Taifa

Na wale Wanasiasa wababe na viziwi ndo wenye huchu wa madaraka, ndo wale wanaotaka kuitawala nchi hii Kwa nguvu ya Dola pamoja na pesa walizotuibia sisi Wananchi.
Sahihi kabisa. Angalia watu kama Simbachawene alivyokuwa Waziri wa Mambo ya ndani, muangalie Ndugai alipotoa onyo kuhusu nchi kupigwa mnada, muangalie na huyu Nchimbi! Utagundua baadhi yao wanaamini kwenye utawala wa sheria, siasa za kuchukuliana na kuvumiliana, nk.

Lakini hawa wenzangu wengine wenyewewe wanaamini kwenye mkono wa chuma, ubabe, nguvu nyingi na vitisho! Huwa hawataki kujishusha, kukosolewa, kujitathmini, nk. Na hapa ndipo kwenye tatizo. Hata wanapokosea wanataka wewe ndiyo uwaombe msamaha au uwapigie magoti!
 
  1. Nchimbi amekuwa akitoa kauli zinazojitenga na mambo ya aibu na ukatili yanayotendwa na Samia pamoja genge lake
  2. Kikao cha Kamati Kuu CCM kilichofanyika Unguja kimevuja kuwa Nchimbi atapelekwa Kamati ya Maadili ya CCM
  3. Kumekuwepo na tetesi za kumshinikiza ajiuzulu ili kumpa amani ya moyo nduli aliye juu yake
  4. Mpasuko huu unapelekea kuongezeka kwa nyufa za Muungano na utawala ngazi ya juu kama nchi
  5. Kuna mpasuko mkubwa ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama kupitia huu mtifuano wa Nchimbi na Samia
  6. Watanzania. Hii ndiyo nafasi pekee Mungu ametupatia ya ukombozi wetu. Tumuombee Nchimbi kwa sababu ameamaua kusikiliza sauti ya HAKI kutamalaki

Mwenye kuni mbichi au kavu shime yuwachochee hawa CCM warndelee kupasuana, kutifuana na kugawanyika ili nchi ipone
So tumuombee sote na akigombea Urais 2030 sote tuungane kumpa kura awe Rais CCM iendelee kutawala
 
Hata Polepole tuliambiwa ni watu wa system tu, kwamba anacheza mchezo na sanaa ya siasa ila ni CCM mtupu.

Je Leo Yuko wapi na kilimtokea kitu gani.
Kwa Sasa hakuna mwana mtandao atajitoa mhanga eti ni mwana mtandao.
 
Aliyemteua Nchimbi kuwa Katibu Mkuu ni Mh.SAMIA,na aliyempitisha Mh. SAMIA kuwa mgombea wa CCM ni Nchimbi-na aliyemteua Nchimbi kuwa Mgombea mwenza ni SAMIA na atakeyemteua Mgombea ajaye wa CCM ni SAMIA.
Siasa ni mchezo,tulia watu wasukume kete.
 
Hiyo mitifuano ni kichwani kwako tu,kwa Tanzania Rais ajeye ateteuliwa na SAMIA.akitaka nchimbi awe basi atakuwa na akitaka mwingine yoyote awe basi atakuwa maana yeye ndio mwenyekiti wa chama na anakadi zote mezani.
 
  1. Nchimbi amekuwa akitoa kauli zinazojitenga na mambo ya aibu na ukatili yanayotendwa na Samia pamoja genge lake
  2. Kikao cha Kamati Kuu CCM kilichofanyika Unguja kimevuja kuwa Nchimbi atapelekwa Kamati ya Maadili ya CCM
  3. Kumekuwepo na tetesi za kumshinikiza ajiuzulu ili kumpa amani ya moyo nduli aliye juu yake
  4. Mpasuko huu unapelekea kuongezeka kwa nyufa za Muungano na utawala ngazi ya juu kama nchi
  5. Kuna mpasuko mkubwa ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama kupitia huu mtifuano wa Nchimbi na Samia
  6. Watanzania. Hii ndiyo nafasi pekee Mungu ametupatia ya ukombozi wetu. Tumuombee Nchimbi kwa sababu ameamaua kusikiliza sauti ya HAKI kutamalaki

Mwenye kuni mbichi au kavu shime yuwachochee hawa CCM warndelee kupasuana, kutifuana na kugawanyika ili nchi ipone
Mbona kama tunapangwa?
 
First time met the guy in 2012 nilikuwa meintenant sun plaza tower floo7

Alikuwa na macho makubwa.! Ya uaminifu.!

Wakati wanaruhusu UMOJA wa vijana ya zamani ivunjwe. 🤗

Wakawa hawana pa kufikia mjini 🤭

Leo wanaita ewura.!?🤔

Sema ni mvivu
 
Sinema zetu tu hizi. Hakuna lolote kwani wao ni wamoja. Tangu lini na wapi ulisikia makamu wa rais akipelekwa kamati ya maadili ya chama au bunge au Serikali? Shitukeni, mnaibiwa pesa za viongilio vyenu!
 
Kama kweli nae anania na anachozungumza kina ukweli bas atoke uko alipo nje na apo ccm haina mtu mwema
Kutoka hapana tunahitaji mpambanaji aliye ndani ya Ccm humohumo ili watibuane hasa. Akitoka yaani inakuwa haina maana inakuwa tu kama Msigwa alivyotoka Ccm kuja Chadema.

Hapa ndo Chadema na nyinyi huwa mnakuwa hamna akili yaani mnaamini eti mtu mpaka awe chamani kwenu ndipo aaminike badilisheni mindset zenu. Maana hata Mbowe mmekuja kumgundua mida mingi sana imepita kuna wakati ni muhimu sana kuwa na mpambanaji aliyepo ndani ya kundi hasimu siyo wote wawe ndani huwa nashangaa sana hata mnapoanza kumnanga HP wakati uwepo wake ndani ya Ccm ulisaidia sana halafu mtu akitubu hata kama alikuwa mbogamboga asamehewa tuungane kwenye mapambano.
 
  1. Nchimbi amekuwa akitoa kauli zinazojitenga na mambo ya aibu na ukatili yanayotendwa na Samia pamoja genge lake
  2. Kikao cha Kamati Kuu CCM kilichofanyika Unguja kimevuja kuwa Nchimbi atapelekwa Kamati ya Maadili ya CCM
  3. Kumekuwepo na tetesi za kumshinikiza ajiuzulu ili kumpa amani ya moyo nduli aliye juu yake
  4. Mpasuko huu unapelekea kuongezeka kwa nyufa za Muungano na utawala ngazi ya juu kama nchi
  5. Kuna mpasuko mkubwa ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama kupitia huu mtifuano wa Nchimbi na Samia
  6. Watanzania. Hii ndiyo nafasi pekee Mungu ametupatia ya ukombozi wetu. Tumuombee Nchimbi kwa sababu ameamaua kusikiliza sauti ya HAKI kutamalaki

Mwenye kuni mbichi au kavu shime yuwachochee hawa CCM warndelee kupasuana, kutifuana na kugawanyika ili nchi ipone
Kwa fursa hii, unaonaje wewe ukawa wa kwanza kuwahamasisha vijana kitaa kudai mabadiliko? Achana na kutamba na JF, ingia kitaa!
 
Fanyeni maigizo yote ila damu za watanganyika October 29th zimeshawatia najisi ya milele hamtasafishika wala kuwa na ridhaa ya raia tena kubabake zenu.
 
Watanzania. Hii ndiyo nafasi pekee Mungu ametupatia ya ukombozi wetu. Tumuombee Nchimbi kwa sababu ameamaua kusikiliza sauti ya HAKI kutamalaki
Ninakubaliana na wewe kuhusu nafasi ya kipekee na adimu sana hii tunayopewa ya "ukombozi wetu"; ila suala la "kuombea" haitoshi bila ya kusimama naye bega kwa bega katika mapambano haya ya ukombozi.

Maombezi tu kwake, hayatakuwa na tofauti kubwa na yaliyotokea Oktoba 29.
Watammaliza haraka sana, na hizo ndoto za ukombozi zitabaki hivyo hivyo.

Naomba sana tuachane na lugha za aina hii.
 
Back
Top Bottom