Watanzania tunaimba viwanda mdomoni, Kenya wanajenga viwanda

Aisee kama ni hivyo mimi sioni haja ya kuendelea na mjadala na wewe. Yaani Dangote Cement si FDI?? A private firm which came in the country with the capital to invest in cement industry!!?? Duu ngoja nikuache.
Inabidi kwanza ujue nini maana halisi ya "FDI",Dangonte ndio ni private firm which came to Tanzania with capital to invest,

Je sasa nikuulize kama kampuni imekuja na pesa kutaka ku invest Tanzania ndio kigezo cha "FDI"?? nafikiri fungua vitabu vyako usome ufahamu nini maana ya "foreign Direct investment"...

Matatizo yetu watazania ni wavivu wakusoma,wavivu wa kufanya utafiti,tunapenda kukukurupuka na kurukia mambo na kujifanya tunajua

kama unataka kujua nini maana halisi ya FDI sema nikufahamishe...!? waswahili wanasema "kuuliza sio ujinga"
 
Hicho ni kitu kizuri mkuu,lakini itategemea hao wachina wanataka kuwekeza vipi Tanzania,unajua mkuu matatizo yetu waafrika ni rahisi sana kuwa ""sell out,kwasababu uko china ndio unaona wachina ndio watakuwa waokozi wa Tanzania,..

Wachina ni wafanya biasahra kama wafanya biashara wengine,faida ndio kitu kikubwa anachokiangalia mfanya biashara,kama mikataba itakuwa mibovu wachina wanaweza kuchukua nchi yote na wakakuachieni jangwa..,nchi bila ya raslimali bila ya miti,bila ya maji..

Someni kwa warabu vipi wamewatajirisha raia wao,someni vipi wanafunga mikataba na kampuni za nje,huu sio wakati wa kujisifia uko china ni wakati wakujisifia umefunaga mikataba gani na kampuni za kichina kuinufaisha Tanzania,tafakari
 
Your stupid. Usitake kujiaibisha hapa fara wewe.
Huna hata cha maana. Ficha upumbavu wako hapa

Tanzania leads regional peers in foreign direct investment
 
Your stupid. Usitake kujiaibisha hapa fara wewe.
Huna hata cha maana. Ficha upumbavu wako hapa

Tanzania leads regional peers in foreign direct investment
wasahili wanasema "ukiona mtu anaanza kujibu hoja kwa matusi ujue kashindwa hoja",unakiwa kwanza uje nini maana ya FDI,kama umeshindwa kujua maana sema uambiwe maan, kuna msemo mwengine wa kiswahili unasema "kuuliza sio ujinga"..

Lakini bado nasisitie kuwa hicho kiwanda kimoja cha Dangonte mnachokisifia ndio FDI hakina sifa ya FDI,pili kiwanda chenyewe kinashindwa hata kuzalisha kutokana na urasimu wenu,Dangote mwenyewe kumuonya Magufuli kuhusu mbinu zake anazotumia kwa wawekezaji wa Tanzania..

Link yako uliyoweka "Tanzania leads regional peers in foreign direct investment" ni habari kama habari nyeingine yoyote ile,hii ni habari ya2017 mambo mengi yamebadilika katika macho ya wawekezaji kutoka nje....
 
Nimekueleza hujui chochote usitaka kujipendekeza. Wewe ni kichwa tupu.
 
Nimekueleza hujui chochote usitaka kujipendekeza. Wewe ni kichwa tupu.
😀😀😀😀 hahahaa mbavu zangu,Mkuu nipe mfano wa viwanda vya FDI vilivyoko Tanzania..😀
 
Matendo yamebaki Kitandani tu.
 
Mkuu, baadhi ya Comments zako nyingi humu sikubaliani nazo,
Jamaa wamekupa hadi evidence kuwa Tanzania is leading the region in FDI, Unatumia feelings zaidi ya facts,
Lakini kuna kitu umeongea kwa huyo jamaa aliyeko China kwa kutumia kodi zetu sijui kama atakuelewa,
Binafsi sifurahishwi na namna hii Sera ya Viwanda inatekelezwa, We are now opening the doors to everyone probably without any precautions, Kitu pekee watz wanatakiwa kuelewa ni Kuwa China is in Africa for China, and so are the Europeans and the Americans, We must decide wisely kwenye haya mambo,
Ukienda pale EPZ ya Ubungo External, au pale Dangote plant Mtwara kaongee na wale employees wazawa mzee utatamani ulie,
Wanasiasa wanatuingiza mkenge tena aisee,
Trust me, hii Sera ya Viwanda ingelenga zaidi kutoa ujuzi na kuwawezesha wazalishaji wadogowadogo wazawa ingekuwa na impact kubwa kuliko hivi sasa, Tuna raw materials kwa nini tunakurupuka namna hii, mtu anatumia pesa za poor taxpayers kuzurula China kuwaalika waje kutuprocessia mahindi na nyanya huu ni uzwazwa, can't we do this??
Ni gharama kiasi gani inahitajika kufungua kiwanda cha furniture au karatasi kule Mufindi au Kiwanda cha kutengeneza viatu na Kushona Matisheti na Mashati serikali inashindwa kufund hadi tukalete wachina?
For sure, Kuna baadhi ya Uwekezaji ambao tunahitaji wawekezaji wenye experience, technology na mitaji mikubwa probably toka nje, like Oil and Gas n.k lakini sio hivi vya matunda sijui nini jamaa wanazindua daily,this sucks kwa kweli.
 
Kitu kimoja cha kukuhakikishia Tanzania imeabdilika sana

Ni wachache tu watakaoamini ifikapo 2025 na nikuhakikishie tena next president ni Magufuli type

Sababu kubwa ni Kupiga hatua haraka za kimaendeleo

Tanzania Kwanza
 
Malibukeni Mnadhani Uwekezaji wa. viwanda vya magari Ndio Uwekezaji tu. FDI in tanzania is biggest in the region.
 
Sio lazima tukubaliane na kila kitu,Mkuu,kupingana ndio njia moja ya kuleta uelewano,ndio maana nchi za wenzetu wanatatua matatizo yao kwa makongamano(debate),kutokana na mawazo ya watu wengi wenye mawazo tafauti ndio unaweza kupata "solution" ya kudumu....

Anyway, Mkuu naona umenisoma na kunifahamu,.,nimefurahi sana kuwa umekuwa muelewa hiyo point(red) uliyoweka hapo ndio hasa serikali inabidi iangalie kwa umakini kwa wawekezaji wa kigeni.

Mkuu unajua katika mambo ya uchumi kuna "model" za aina nyingi serikali zinakuwa zainafata "methodologies" tafauti ili kuendeleza ucgumi wa nchi..

Model 1)Sereikali inaweza ikaleta sera ya uchumi ya kuwanifaisha wananchi,kutoka kwa wananchi ndio serikali itafaidiaka kwa kukushanya kodi,vile vile kodi inayokusanywa kwa wananchi inarudi tena kwa wananchi kwa kuwawezesha kwenye biashara zao au miradi yao,serikali inafungua miradi tafauti ile kuifanya pesa izunguke...

Model kama hii ni ya warabu,na naona Vietnam imeiga vile vile,na hizi nchi zote zimepaa kiuchumi,hii naweza kuita model ya "serikal ni wananchi",kama vile tulivyodundisha tukiwa darasa primary schoool

model 2)Model nyengine kuwa serikali inafanya kila kitu peke yake,inafungua miradi mikubwa mikubwa,kodi inakuwa kubwa sana kwa wananchi ili mwananchi asiwe juu ya serikali,..

Model hii ni yakuinufanisha serikali lakini kuwatia umasikini wananchi,model hii inakaribisha udikteta,"inakarisha "police state" hii Model naita Serikali ni baba wa wananchi ni watoto,kila kitu kinaamua serikali,hii ni Model ya Magufuli...,

Model hii ya Magufuli nchi itang'ara kwa miundo mbinu na mambo mengine lakini wananchi wako maskini,Model hii mwisho wa siku ita "collapse"..,haina mwisho mwema wananchi wata "revolt" baadae

Nchi kama Dubai na sasa Vietnam mwekezaji yoyote wa nje akitaka kuwekeza lazima ashirikiane na kampuni ya mzawa,kufanya hivyo wazawa ndio wanaudhibiti uchumi wao,Tanzania inabidi tuige mfumo wa Dubai ili kuwawezesha watanzania wajitoe katika imasikini uliokithiri

Bila kuwasezehsa watanzania wazawa Tanzania haiwezi kufika popote,wawekezaji watachukua chao nakuondoka,nchi itakuwa shamba la bibi,tumeona mifano ya mikataba iliyowekwa kwenye madini na mambo mengine vipi imeiflisi Tanzania

Turudi kwenye FDI(Foreign Direct Investment),huu ni mfumo wa uwekezaji wa kampuni za nchi kwa kutumia rasilimali zao wenyewe,mfano kampuni ya Toyota imefungua "assemble Plant" Kenya,Toyota inakuja na kila kitu chake Kenya inachohitajia ni "Labor" tu,..

Kwa maana hiyo Toyota itafanya kila njia katika mikataba yake na serikal ipatiwe "cheap labor",moja katika kasoro za FDI ni kuwalipa mishahara midogo wafanya kazi ili wafanye biashara zao..

Kiwanda cha saruji cha Dangote hakina sifa za "FDI",kwasababu Dangote anategeme rasilimali zote kutoka Tanzania,kuanzia gesi,lime stone nk,huu ni uwekezeshaji wa kawaida tu sio FDI..

Unakaribishwa kutoa maoni yako kwani naamini kuwa "Discussion is the only way of solving problem permanently"😉
 


BREAKING DOWN 'Foreign Direct Investment - FDI'

Foreign direct investments are commonly made in open economies that offer a skilled workforce and above-average growth prospects for the investor, as opposed to tightly regulated economies. Foreign direct investment frequently involves more than just a capital investment. It may include provisions of management or technology as well. The key feature of foreign direct investment is that it is an investment made that establishes either effective control of, or at least substantial influence over, the decision-making of a foreign business.

The Bureau of Economic Analysis (BEA), which tracks expenditures by foreign direct investors into U.S. businesses, reported total FDI into U.S. businesses of $373.4 billion in 2016, marking a 15% decrease from the prior year. As per usual, acquisitions made up the overwhelming majority of new foreign direct investments into the U.S., totaling $365.7 billion. Meanwhile, greenfield investments, a type of FDI defined by the BEA as investments to either establish a new business or to expand an existing foreign-owned business, comprised a much lighter $7.7 billion.


Read more: Foreign Direct Investment (FDI) Foreign Direct Investment - FDI
Follow us: Investopedia on Facebook
Foreign Direct Investment - FDI
 
 
Umefahamu kilichoandikwa hapo...,au ume google copy and paste...,bado hii "article" yako haijaeleza nini "FDI",imeleza "financial aspect ya "FDI" tu"...

Kuna post humu nimemjibu "Game over" kwa makini nini "FDI" na vipi inafanya kazi katika nchi husika...
 
Aisee dah, una akili nyingi sana bro, wenzako hawakuelewi kabisaa..st kayumbazz taaabu!!![emoji382]
 
You're writing nonsense

No any Empiricism in you're argument rather than toilet words
Teh teh! Did I hurt your feelings? Write that again without crying.
 
Ongea facts sio maneno ya mtaani ,tatizo unachanga siasa na Policy ya Tanzania ya viwanda?
Kwa hiyo kwa akili timamu (sidhani kama ni timamu), vitu hivyo viwili vinaweza kutengeneshwa? No wonder mna maniac of a president ambaye anasema yeye siyo mwanasiasa. Na fools like you mnapiga vigelelege.
 
Mkuu nimeona kama una matatizo ya kufahamu kingereza hii link uliyoweka ->"Foreign Direct Investment - FDI" inaeleza habari zote kuhusu "FDI",..

Inaeleza Mbinu za kuwekeza kwenye FDI (Methods of Foreign Direct Investment),
Aina za FDI (Types of Foreign Direct Investment),
mifano ya FDI(Examples of Foreign Direct Investment's Impact)..

Sasa kwanini umekwenda ku copy and paste habari ya "economical beneficiary" ya FDI?! halafu unaniambia ndio maana ya FDI!??😀

Ingia kwenye hiyo link utafaidika sana kama unataka kujua nini hasa maana ya FDI,kuna aina ngapi za FDI na mbinu gani zinatumika kwa kampuni katika kuwekeza kwenye FDI...

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…