Watanzania tunapaswa kuambiwa na kujua ukweli kwamba Gesi inayochimbwa Mtwara si yetu

Kwamba angalau kidogo sio?
 
Hata gas ingekuwa yako hakuna cha maana ungepata,mfano ni madini tuambie serikali inafaidika na nini kikubwa kuwasogelea wawekezaji?
 
Mungu ndio kafanyaje? Gas atafiti mzungu,teknolojia yeye, wataalamu yeye,soko analijua yeye wewe umekalisha battacks zako eti unasubilia 50/50 ,,mjinga ndio atakupa..

By the way madini yoyote hata leo wakisema tunaweka vikwazo hatununui si mtaishia kuchezea BAO tuu maana hakuna cha kufanyia..

So tukipata kodi,ajira na utaalamu inatosha Sana.
 
Contract ni ya muda gani kwa hao wawekezaji kurudisha gharama na kupata faida? hisa za serikali ni asilimia ngapi? ndo maana magu hakuwa na mzuka nako hadi kuangukia kwenye bwawa la stiglaz.......
Hisa za nini kwenye gas?
 
Upumbavu,eti subiria kwani teknolojia inakusubiria wewe? Mahitaji yanakusubiria wewe? Ni wewe pekee ndio una hayo madini au gas Duniani?

Usubirie Ili uvumbue nini? Kwani kila nchi ina madini? Na ambako hakuna maisha hayaendi?
 
Mambo ya kikwete na madam mwenye macho Kama kinyonga
 
Kwani hata bandari inayo taka kujengwa bagamoyo kwani itakuwa ya kwetu?

Sent using Jamii Forums mobile app
itakua ya mchina , na mkataba ni miaka mia , hivi ndivyo tulivyorogwa na mabeberu, bado kuuza mlima Kilimanjaro tu na serengeti maana huko hoteli zao washajenga na wana hati miliyi ya miaka zaidi ya 200
 
Wameghakamia utafiti,uchimbaji na uchakataji wa hyo gesi yan wabongo tunataka gesi iwe mali yetu kwa zaidi ya 30% kwa kutochangia chochote turidhike tu na hyo 16%
Pamoja na makelele meeengi na mikwara ya kina mwendazake kwenye makinikia tumeishia kupata kiinimacho cha 16% 😄😄..
 
Kwani JPM alivyosema kwenye gesi hatuna chetu hukumuelewa? Unazani kwanini aliamua kuingia kwenye umeme wa Hydro? RIP Jembe
Hiyo Jembe hakuwepo miaka hiyo? Hakuwa anagonga meza? 😄😄..

Kwa taarifa yako India wanazalisha zaidi ya mgwt 5,000 za umeme wa jua kwa pesa isiyozidi til.4 wakati wewe na tuumeme twako tena twa maji utazalisha mg 2000 tuu kwa til.7..

Huu kama sio WEhu wa huyo Jembe wako ni nini? Stupid wajinga nyie
 
Kuelimisha wale wajinga waliojaa mihemko na propaganda za Jiwe kichwani ni sawa na kujaza maji kwenye net mkuu..

Haya majinga ni kuyaacha afu yaone matokeo,ndio yamelishwa upumbavu Sana na yule jizi mkuu Jiwe.
 
Ok, hao wageni walitupa nini hadi tukawapa hiyo gesi wachimbe? Bila shaka kuna makubaliano na sisi tumefaidika.
Napendekeza zile account za uswiss zichunguzwe. Huko Ndio wanakozichimbia.
 
That’s impossible kwa sababu mwekezaji hajui kama atakuta reserve ya kutosha anaweza fanya exploration akakuta kiwango chenyewe gharama za kutoa mafuta ni kubwa kuliko hela inayopatika.

Let’s say for example gharama ya Kujenga infrastructure ya kutoa mafuta ni $30 billion, commercial reserve estimate ya mafuta/gas iliyopo ni $10 billion; sasa si ni bora kuyaacha huko huko yalipo kuliko kujiongezea hasara.

So ni lazima wajue kiwango cha reserve, amount of investment needed in upstream and mid stream; halafu baada ya hapo ndio waingie kwenye mkataba wa pili.

Zile sheria za dharura zililenga kuweka majedwali ya kiwango wanachoweza vuna in percentage of reserve amount baada ya kurudisha hela zao, na azikuwa popular kwao.

Tatizo wataalamu wakitaka kuwasaidia kama hakina Prof Muhongo mnaanza kupotoshana na kuwatukana inabidi waache.

Ni sawa na Dr Gwajima akiamua kuibadilisha afya iwe na huduma bora ashindwi, kufanya ivyo atapigwa vita na wazembe huko kwenye vituo vya afya, huku hana support ya jamii wala serikali. Sasa si bora ale neema za kuwa waziri tu kuliko kununua ugomvi ambao hana backup.
 
Impossible kwa vipi? Ni suala la kuweka "IF you get oil...", the rest inabakia jinsi inavyotakiwa kuwa kwenye mkataba wa pili. Kwani huwezi kutengeneza mkataba wenye options kuwa kitu kimoja kikitimilika, then mkataba unafuata option hiyo? Huoni kuwa tunakuwa kwenye disadvantage position unapo negotiate na mgundua mafuta baada ya yeye kuyagundua na technically ni yake yote kwani hakuna mkataba ?
 
Una mali sawa lkn huna pesa ya kuutumia hyo mali ipasavyo au gesi nayo tuwape wachimbaji wadogowadogo wachimbe
Kwa hiyo kwa maoni yako, kwa viule machinga wetu hawawezi kuichimba hiyo gesi, basi ni bora wachukue wenye uwezo wa kuichimba hata kama manufaa ya uchimbaji huo hayatupi manufaa ya kutosha!

Hizi ndio akili tulizobaki nazo huko serikalini?
 
Wapi nimesema wanachukua kila kitu wanachokikuta huko chini? Hata hivyo wachangiaji wengi wameeleza tena wengine wameeleza kiundani zaidi kuhusu hizo biashara katika maeneo mbalimbali huko duniani.
Mimi sijaona maelezo hayo kwenye mada hii, hebu nipe mfano uliouona wewe kwenye jukwaa hili.
 
Kwa kuujua ukweli huu ndio maana Hayati Jiwe aliwahi kusema,"...Kwenye gesi, huko tumepigwa..."!
 
Hakuna dhahma yeyote. Kama unataka gesi iwe yako by 100% ulipaswa uwekeze mwenyewe kwa fedha zako kwenye Exploration na R & D.

Ile kujuwa tu kuwa kwenye shores za Indian ocean kuna gesi tulikuwa hatujui. Amekuja mzungu amewekeza kwa mkataba na TPDC akaikuta gesi na akatupa hisa bado tunalalamika.!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…