Watanzania tunapitia kipindi kigumu kiuchumi kuwahi kutokea

Acha kulalamikia kitu kisicho na uhalisia,umeandika mengi lakini ni Nonesense [emoji57]
 
Kama unaona wanaolalamika kuhusu hizi tozo wanaigiza basi chukua Mali zako zote uuze kitakachopatikana ipe serikali ili ijulikane wewe ndo mzalendo Mana unachokitete ni ujinga na utoto.
Sijasema kuwa KIWANGO CHA TOZO kiko sahihi....

Ndio maana mh.Rais Msikivu amekisikia kilio chetu kwa kuunda kamati....majibu yakipatikana tutakuwa na nafasi nzuri kudadavua.....

Ila.....

Serikali Ni lazima ibuni vyanzo vya mapato....

Ingekuwa ni hiyari...hakuna mtumishi wa UMMA angekubali kukatwa.....

#KaziIendelee
#SiempreSSH
 
Wanufaika wa mikopo ni sehemu ndogo sana ya watanzania. Sasa Samia kaondoa hiyo TOZO ya 6% halafu kapandisha makato apo ndo kafanya nini sasa.?
 
Ulikuwa huna muajiriwa hata mmoja kwa miaka 6....ndani ya siku 100 una waajiriwa 8000....

ENDELEA KUUFUKUZA UPEPO
So nafasi za ajira za walimu zaidi ya 35000 je? Au ndo mpaka ajisikie wakati vijana wako mitaani hawana ajira? Mm nakwambia ukweli, nenda mtaa wowote sasaiv conduct survey ya jinsi gani raisi anakubalika, alaf nijibu
 
Tanzania hata akija Mungu kuwa rais wetu watu watalalamika na kusema bora hata yule rais aliepita kuliko huyu Mungu wa sasa.
 
Hajaajiri ndugu, ametupoza!! Uhitaji 40,000 ualimu tu alaf katoa kibalicha 7k-8k ili iweje? Kwahiyo sehemu zenye uhitaji na walimu hawakupelekwa wasubirimpaka lini au wao hawana umuhimu? Unataka tushukuru kwa lipi tozo za miamala, bei ya mafuta kuongezeka na hela kuzidi kuwa ngumu kitaa?
 
Ndo ibuni vyanzo vya kodi na mapato! Ila tozo ni kukosa ubunifu na kuaminisha watz kuwa raisi haelewi na hawezi kazi! Alowaajiri wote wizara ya fedha na wizara nyengine pia wameshindwa kufikiri mpaka wakatafuta njia nyepesi ya kuibia na kunyonya kipato kidogo cha mtanzania mnyonge!!!🤮🤮🤮🤮

Imagine kitu linasimama na majivuno;
ETI MIMI NI DR. WA UCHUMI!! sasa ulishindwa vipi kutafakari vyanzo vya mapato!!
 
Kodi si lazima? Wachukue ilala Tozo kwanini iwe lazima? Sa si bora watuambie yote ni kodi tuelewe kama ni lazima?
 
Awamu ya 5 haikutoa ajira kwa miaka 6....wewe ulikuwa usingizini kutoziona hizi ajira 8000 za TAMISEMI na WIZARA YA AFYA?!!!

#KaziIendelee
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Jiwe nae aliajiri Walimu kama mara mbili hivi. 2017 aliajiri walimu wa sayansi na 2019 kipindi cha uchaguzi aliajiri walimu 8000.
 
So nafasi za ajira za walimu zaidi ya 35000 je? Au ndo mpaka ajisikie wakati vijana wako mitaani hawana ajira? Mm nakwambia ukweli, nenda mtaa wowote sasaiv conduct survey ya jinsi gani raisi anakubalika, alaf nijibu
Mkuu usemalo ni kweli....ajira ni tatizo....ila mh.Rais ameanza kuajiri 8000 tena kufidia nafasi za wastaafu na waliofariki dunia....mwakani kabla ya bajeti ataajiri tena....
Ni zoezi endelevu.....

Tumpe muda mama....
Hili la tozo ataliangalia kwa macho 3......

#KaziIendelee
#SiempreSSH
 
😍
 
Kujenga upya mfumo wa uchumi aliouacha Mwendazake inaweza chukua hata muongo au miongo.........

Ilichukua awamu tatu (miongo mitatu) kuusimamisha uchumi uliobomolewa na Siasa na Sera za kijamaa pamoja na Vita ya Kagera.

Ukweli mama Samia ana wakati mgumu, kuliko JPM alivyochukua nchi. Ni kama Rais Mwinyi alivyochukua nchi. Nchi ikiongozwa na watu wenye mentality ya ujamaa/ socialism inakuwa haifanyi vizuri kiuchumi, kidemokrasia na kidoplomasia, bali inafanya vizuri kwenye propaganda za kuwa-win maskini,wasio na elimu nk
 
Magu mpaka anafariki ameacha makusanyo TRA hapo Trilion 1.6 wakati alikuta billion 800, Magu hakupandasha bei za bidhaa kama maguta zaidi alirahisisha upatiakanaji mafuta kwa kusini baada ya kusafirisha kwa gari toka Dar mpaka Mtwara ila Meli ilikuwa inaenda kushushia kulekule, JPM hakutuachia matozo ya uzalendo haya! Kila mtu abebe msalaba wake kama JPM alibebeshwa msalaba wake na huyu Jumong abebeshwe msalaba wake pia.
 
Braza.. trillion 1.6 kwa takwimu za Mwendazake? Zimeenda wapi kwa siku 120+?

Kumbuka wengi tulidhulumiwa...

Bei ya sasa ya mafuta ndio iliyokuwepo kipindi kile Cha marehemu kabla ya janga la korona ( wimbi la kwanza Covid-1) baadae yakashuka mpaka kufikia Tsh. 1600 kipindi Cha covid-19.
 
Suala la tozo dizaini kama mnamkwepesha mithiri kama hakuwa anajua chochotr vile!! Sasa nakuletea kifungu cha katiba hapa kinachosema issue yoyote inayohusu masuala ya kodi hakitawasilishwa Bungeni bila kupata idhini ya Mh Rais! Kwa maana wazo linakuwa kwa Rais ila kwa niaba ya Rais ndiyo linawasilishwa Bungeni na Waziri husika.

Kwaiyo issue ya Tozo anaijua kinagaubaga sio yakusingizia.
 
Sikusema mh.Rais HAIJUI HIYO TOZO....

Anaijua....

Kilichowakera wananchi ni kiwango kikubwa....na ndio maana mh.Rais ameyapokea malalamiko na ameagiza KAMATI iangalie viwango na ije na mapendekezo.....

Hoja ni kiwango cha TOZO....hoja si kutokuwepo kwa hiyo TOZO....

#KaziIendelee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…