Pre GE2025 Watanzania tunataka kura zetu zihesabiwe wazi wazi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kule Congo aliyekuwa Mkuu wa time ya uchaguzi iliyomuweka Tishekedi madarakani 2023 ndiyo huyo huyo Leo anaongoza M23
 
Maneno yako ni mazito.
Lakini yana dalili za kukata tamaa.
Wagombea ni Vyama.
Wapiga Kura ni sisi sote.
Tatizo letu Nchini, walioko Madarakani hawataki Tume Huru, hawataki Katiba Mpya, na hawaoni aibu kujinasibu na hali hiyo.
Sauti ya Wapiga Kura inao uwezo wa kufikisha madai haya mpaka Nje ya Nchi, na kwenye ulingo wa Kimataifa, shinikizo linaweza kuwarudia hawa Watawala wetu.
Kupaza kwetu sauti, kutaenda sambamba na jitihada za Vyama vinavyodai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.
Sauti za Wapiga Kura zitakuwa CHACHU kwenye jitihada zilizopo za kudai mabadiliko.
Kumbuka Mtawala aliyepo Madarakani haoni aibu kuwaengua Wagombea wa Vyama vingine na kubakiza wale wa Chama chake tu.
Kundi pekee ambalo haliwezi kuenguliwa ni sisi Wapiga Kura.
Tupaze sauti.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
Mimi sijakata tamaa bali nimepuuza huo uhuni uitwao uchaguzi. Usichanganye kukataa tamaa na kupuuza boss. Ndio maana nasema machafuko ni njia sahihi ya kurejesha heshima ya box la kura.
 
Njia pekee ya Watanzania kuheshimiwa na Wawakilishi wetu ni kuhakikisha kwamba Kura zetu zinahesabiwa katika mazingira ya uwazi kwenye kila Kituo cha Kupigia Kura, na matokeo hayo yawe rasmi.

Tabia ya kufukuza Wapiga Kura kwenye Vituo vya Kupiga Kura ikomeshwe ili Mshindi halali ajulikane.
Hili halihitaji Azimio la Bunge wala Mswada wowote wa Sheria.

Wananchi tukiamua na kushinikiza, hili linawezekana kufanyika kwenye Uchaguzi Mkuu Novemba mwaka huu 2025
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
Kuandamana huwezi ndio utaamua kulinda kura!? PUMBAVU!
 
Mimi sijakata tamaa bali nimepuuza huo uhuni uitwao uchaguzi. Usichanganye kukataa tamaa na kupuuza boss. Ndio maana nasema machafuko ni njia sahihi ya kurejesha heshima ya box la kura.
Na machafuko yakianza tunaanza na wewe na familia yako mnakuwa wiped out! Kenge wewe!!
 
Kule Congo aliyekuwa Mkuu wa time ya uchaguzi iliyomuweka Tishekedi madarakani 2023 ndiyo huyo huyo Leo anaongoza M23
Ndiyo sababu Wapiga Kura tunatakiwa kuamka na kudai heshima ya Kura zetu.
Kwa kipindi kirefu, Watanzania tumekaa pembeni na kuwaachia Wanasiasa mstakabali wa Nchi yetu.
Hili la Wanasiasa wa Kongo liwe fundisho juu ya ukomo wa kuwaamini Wanasiasa.
Tudai haki stahiki ya Mpiga Kura.
Tuanze na hili la Kura zetu kuhesabiwa kwa Uwazi.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Mimi sijakata tamaa bali nimepuuza huo uhuni uitwao uchaguzi. Usichanganye kukataa tamaa na kupuuza boss. Ndio maana nasema machafuko ni njia sahihi ya kurejesha heshima ya box la kura.
Ni vigumu kutenganisha kukata tamaa na kupuuza.
Kwa kuwa hii ni Nchi yetu sisi sote, tusipuuze hizi taratibu za Kisiasa zinazowapa nguvu za Kisheria, watu kututoza Kodi na kupanga matumizi ya Kodi zetu hizo.
Tule nao Sahani moja.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Kuandamana huwezi ndio utaamua kulinda kura!? PUMBAVU!
Usikate tamaa.
Watawala wanafurahia sana Watanzania wanapoandika matusi badala ya Hoja.
Wanaamini wanaotukana hawawezi kujipanga na kuweka shinikizo kwa Watawala.
Tusikubali.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Na machafuko yakianza tunaanza na wewe na familia yako mnakuwa wiped out! Kenge wewe!!
Njia sahihi ya Kuzuia machafuko ni Haki kuonekana imetekelezwa.
Mifano dhahiri ipo mingi duniani.
Kura zikihesabiwa kwa uwazi, anayeshindwa hawezi kuleta machafuko.
Machafuko yanatokea pale Kura zinapohesabiwa mafichoni bila uwazi.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Ukiwaachia ni sawa na kuacha Mlango wazi ili Mwizi aje KUIBA kiulaini.
Tufunge Milango kisawasawa, ili Mwizi akija, apambane kuuvunja.
Anaweza kukamatwa kabla hajatimiza azma yake ya kishetani.
Tupige Kura.
Na Kura zetu ZIHESHIMIKE.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
Tatizo ni kwamba wanaanza kuengua wagombea hilo nalo utalizuiaje na sababu ya kuengua wagombea nikuwakatisha tamaa wapiga kura kuwa hata mkienda kupiga kura sisi tayari tunawabunge au madiwani waliopita bila kupingwa zaidi ya nusu kisha wanakuja kuchakachua wagombea kiduchu waliopita sasa si ujinga huo afadhali tu uwaachie wote. Kisha wanakuja kukupa wabunge wa viti maalumu na fedha ili kukupoza kwasababu wanajua una njaa. Kwa mfumo huu wa uchaguzi wala sijisumbui. Wanaokwenda na waende tu.haya nimaamuzi yangu mwenyewe na viongozi watakao pita mimi nitawaheshimu tu kwani ndiyo mifumo yetu.
 
Na machafuko yakianza tunaanza na wewe na familia yako mnakuwa wiped out! Kenge wewe!!
Tena nitahakikisha mnaanza na mimi, maana hakutakuwa na mabadiliko bila hayo kutokea. Nina uhakika baada ya mimi kutoweka hiyo itakuwa damu iliyomwagwa kwa ajili ya mabadaliko.
 
Mbona kura kwenye vituo huwa zina hesabika kwa uwazi tatizo ni kukosa mawakala, CCM wakizidiwa wakati wa uchaguzi huenda maporini lejea taarifa ya mkuu wa wilaya aliye tumbuliwa
MAWAKALA huondolewa kwa nguvu kwa msaada wa polisi ili matendo ya wizi wa kura yafanyike.
Kura zihesabiwe kwa uwazi mbele ya wapiga kura wanaopenda kushuhudia zoezi hilo.
Hakuna haja ya kujificha chumbani, kura zipigwe wazi na zihesabiwe kwa uwazi tena nje katika eneo la wazi.
Watz wanapenda amani na wangependa zoezi la kupiga kura na kuhesabu vifanyike kwa uwazi mbele yao wakishuhudia.
 
Tatizo ni kwamba wanaanza kuengua wagombea hilo nalo utalizuiaje na sababu ya kuengua wagombea nikuwakatisha tamaa wapiga kura kuwa hata mkienda kupiga kura sisi tayari tunawabunge au madiwani waliopita bila kupingwa zaidi ya nusu kisha wanakuja kuchakachua wagombea kiduchu waliopita sasa si ujinga huo afadhali tu uwaachie wote. Kisha wanakuja kukupa wabunge wa viti maalumu na fedha ili kukupoza kwasababu wanajua una njaa. Kwa mfumo huu wa uchaguzi wala sijisumbui. Wanaokwenda na waende tu.haya nimaamuzi yangu mwenyewe na viongozi watakao pita mimi nitawaheshimu tu kwani ndiyo mifumo yetu.
Kwenye maelezo yako, kuna makosa mawili ya kiufundi.
Kosa la kwanza ni kuwaachia wafanye wanachopenda.
Tusiwaachie.
Tupaze sauti zetu na tuwaseme sana.
Kosa la pili kwenye andiko lako ni pale unaposema "utaheshimu atakayeletwa".
Mwizi akikuubia Baiskeli yako, hutakiwi kukubali.
Silaha yetu sisi Wapiga Kura ni moja tu: SAUTI ZETU kwenye SOCIAL MEDIA.
Hii Mitandao inao uwezo wa kufanya miujiza.
Mfano, wapo madhalimu ambao PRESHA huwa inawapanda wakimuona Maxence Mello wetu wa JF. Hii ndiyo nguvu ya Social Media.
Tutumie.
Tupaze sauti zetu.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Tena nitahakikisha mnaanza na mimi, maana hakutakuwa na mabadiliko bila hayo kutokea. Nina uhakika baada ya mimi kutoweka hiyo itakuwa damu iliyomwagwa kwa ajili ya mabadaliko.
Mabadiliko bila damu kumwagika yanawezekana.
Na hii ndiyo Historia ya Nchi yetu.
Mwaka 1961, Tanganyika ilipata Uhuru bila damu kumwagika.
Baadaye Vyama vingi vikarudi bila damu kumwagika.
Na Kura zetu zitahesabiwa kwa uwazi bila damu kumwagika.
Na hapo, mimi na wewe tutashikana mikono kusherehekea ushindi huo mkubwa wa Kura zetu kuheshimika.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
MAWAKALA huondolewa kwa nguvu kwa msaada wa polisi ili matendo ya wizi wa kura yafanyike.
Kura zihesabiwe kwa uwazi mbele ya wapiga kura wanaopenda kushuhudia zoezi hilo.
Hakuna haja ya kujificha chumbani, kura zipigwe wazi na zihesabiwe kwa uwazi tena nje katika eneo la wazi.
Watz wanapenda amani na wangependa zoezi la kupiga kura na kuhesabu vifanyike kwa uwazi mbele yao wakishuhudia.
Hiki ndicho kinachotakiwa.
Watanzania tukipaza Sauti zetu, na Jumuiya ya Kimataifa ikatuunga mkono, uwazi wa kuhesabu Kura unawezekana.
Nini maana ya kukaribisha "Election Observers" kama Kura hazihesabiwi kwa UWAZI?
Tupaze sauti.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
MAWAKALA huondolewa kwa nguvu kwa msaada wa polisi ili matendo ya wizi wa kura yafanyike.
Kura zihesabiwe kwa uwazi mbele ya wapiga kura wanaopenda kushuhudia zoezi hilo.
Hakuna haja ya kujificha chumbani, kura zipigwe wazi na zihesabiwe kwa uwazi tena nje katika eneo la wazi.
Watz wanapenda amani na wangependa zoezi la kupiga kura na kuhesabu vifanyike kwa uwazi mbele yao wakishuhudia.
Polisi hutoa matangazo watu wasikae karibu na vituo vya kupigia Kura eti kabla ya kupiga Kura unahitajika, lakini ukisha piga huhitajiki Tena, unakuwa siyo mzalendo, kikikiki
 
Kwenye maelezo yako, kuna makosa mawili ya kiufundi.
Kosa la kwanza ni kuwaachia wafanye wanachopenda.
Tusiwaachie.
Tupaze sauti zetu na tuwaseme sana.
Kosa la pili kwenye andiko lako ni pale unaposema "utaheshimu atakayeletwa".
Mwizi akikuubia Baiskeli yako, hutakiwi kukubali.
Silaha yetu sisi Wapiga Kura ni moja tu: SAUTI ZETU kwenye SOCIAL MEDIA.
Hii Mitandao inao uwezo wa kufanya miujiza.
Mfano, wapo madhalimu ambao PRESHA huwa inawapanda wakimuona Maxence Mello wetu wa JF. Hii ndiyo nguvu ya Social Media.
Tutumie.
Tupaze sauti zetu.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
Pressure Machine hakuna inayo mpanda kiongozi wa kiafrika akitafuta madaraka, wanaua adharani na kunyamaza kimya sembuse kuchakachua kura, mimi nitawaheshimu tu kama viongozi wangu kwa sababu imeshakuwa mila na tamaduni zetu nitajitaidi kujilimia viazi huku kwetu njombe niuze nisomeshe wanangu ila swala lakuwapigia kelele wala sifanyi wacha waibe tu.
 
Back
Top Bottom