Pre GE2025 Watanzania tunataka kura zetu zihesabiwe wazi wazi

Pre GE2025 Watanzania tunataka kura zetu zihesabiwe wazi wazi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tindo, uko sahihi sana.
Uwakilishi unaopatikana kwa mbinu badala ya Kura halali, ni uporaji na ni kinyume cha Katiba iliyopo na Kanuni za Uchaguzi zilizopo.
Kwa kuwa Kura zinatakiwa ziwe halali, Wapiga Kura tumechangia sana kuleta tabia hizi mbaya za Chama Tawala kwa kukaa kimya.
Kila wanachofaa, sisi tumekuwa kimya.
Mwishowe wanajiona wako sahihi.
Hatuhitaji Silaha za moto.
Tunahitaji kupaza sauti, tusikike.
Wanaotumia Silaha za moto, Kwa watu ambao hawana hata mawe mikononi wana lengo la kututisha.
Wanalenga kututisha ili tutishike, tuogope kusema.
Kimsingi, wanajijua kuwa wana hatia.
Sisi tupaze sauti.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
Mkuu huenda hufuatilii vizuri, ukipiga kelele hakuna lolote la maana litatekelezwa na wanasema hayo ni maumivu ya kushindwa. Na wala wanaosimama kidete kupinga wizi huo hupewa kesi za kuharibu uchaguzi. Kibaya zaidi mahakama zinakuwa zimepewa maelekezo ya kuwafunga watu waliokuwa wanapinga uhuni huo.

Haya yanayoitwa maridhiano ni pamoja na watu waliofungwa kwa kupinga kura za wananchi kuchezewa, lakini hakuna hatua za kisheria walizochukuliwa wanaoharibu chaguzi. Machafuko pekee ndio lugha itakayoeleweka kwa wanaonajisi chaguzi zetu. Lakini kupaaza sauti ni kuongopeana mchana kweupe.
 
Naunga mikono hoja,
Watanzania ikibidi katika kituo cha kupiga kura tujigawe,wa ccm upande wao na upinzani upande wao,ijulikane kabla hata ya kura kupigwa
 
Mifumo inaweza kusaidia kuimarisha imani ya umma katika mchakato wa uchaguzi na kuleta uwazi zaidi kwenye upigajinna kuhesabu kura:

1. Uchaguzi wa Kidijitali: Kutumia mifumo ya kidijitali kwa ajili ya kuhesabu kura inaweza kuongeza uwazi. Hata hivyo, ni muhimu kuhakikisha mfumo huo unakuwa salama na unapatikana kwa umma.

2. Vituo vya Uhesabuji Kura vya Hadhara: Kuweka vituo vya kuhesabu kura ambavyo vinapatikana kwa umma, ambapo waangalizi na wawakilishi wa vyama wanaweza kushuhudia mchakato mzima.

3. Vidokezo vya Kura (Ballot Tracking): Kutoa mfumo wa kufuatilia kura zinazopigwa, ambapo wapiga kura wanaweza kufuatilia kura zao hadi mwisho wa mchakato wa kuhesabu.

4. Ushirikishwaji wa Waangalizi wa Tatu: Kuleta waangalizi wa kimataifa au wa ndani ambao wanaweza kushiriki katika mchakato wa uchaguzi na kuangalia uhalali wa mchakato wa kuhesabu kura.

5. Ripoti za Mara kwa Mara: Kutolewa kwa ripoti za mara kwa mara kuhusu mchakato wa kuhesabu kura ili kuweka umma informed na kuimarisha uwazi.

6. Kurekodi na Kutangaza Matokeo kwa Haraka: Matokeo ya awali yanaweza kutangazwa haraka ili kupunguza nafasi za udanganyifu na kuweka uwazi.
 
Tukiamua, kwa wingi wetu sisi Wapiga Kura, asiyetaka atalazimika kutaka.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
Na kwanini mtu asitake uwazi,yeye ni nani?
Mimi nasemaje ikibidi kila chama wakati wa kura kiwe na upande wake tuone hawa ni ccm na hawa ni Chadema ama Act
 
Mkuu huenda hufuatilii vizuri, ukipiga kelele hakuna lolote la maana litatekelezwa na wanasema hayo ni maumivu ya kushindwa. Na wala wanaosimama kidete kupinga wizi huo hupewa kesi za kuharibu uchaguzi. Kibaya zaidi mahakama zinakuwa zimepewa maelekezo ya kuwafunga watu waliokuwa wanapinga uhuni huo.

Haya yanayoitwa maridhiano ni pamoja na watu waliofungwa kwa kupinga kura za wananchi kuchezewa, lakini hakuna hatua za kisheria walizochukuliwa wanaoharibu chaguzi. Machafuko pekee ndio lugha itakayoeleweka kwa wanaonajisi chaguzi zetu. Lakini kupaaza sauti ni kuongopeana mchana kweupe.
Nimesoma kwa makini ilichoandika.
Bandiko lako limeegemea upande wa Mfumo wa hivi Vyama vyetu vya Kisiasa.
Na hicho ndicho wanachotamka Watawala.
Kwamba, Wananchi wa kawaida, ambao ndio Wapiga Kura, WAJITENGE NA MADAI YA VYAMA VYA SIASA, ili kesho na kesho kutwa Babu Wassira aende kwenye Majukwaa na kuwaambia watu kwamba hayo ni "mambo ya Waoinzani".
Hoja yangu mimi ni kuhusu SISI WAPIGA KURA, tena wengi wetu, (majority), tusio Wanachama wa Chama chochote cha Siasa.
Nimemskia Mchambuzi wa Siasa na Ujasusi, ndugu yetu Evarist Chahali, akisema kwamba Asilimia 80 ya Wapiga Kura, siyo Wanachama wa Chama chochote cha Siasa.
Kundi hilo ndilo tunaotakiwa kupaza sauti zetu.
Kwenye Vituo vya Kupiga Kura, CHADEMA wanakuwa na Wakala.
CCM wanakuwa na Wakala.
Sisi tusio na Wakala, tena ambao ndio MAJORITY, haki yetu inalindwa na nani?
Mlinzi pekee wa Haki yetu ni KURA ZETU KUHESABIWA KWA UWAZI, na zitangazwe kuwa rasmi.
Tupaze sauti zetu.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Cha kwanza kabisa issue ya UCHAWA ife
Hubble Telescope, (Astrophysicist),
Majority ya Wapiga Kura tumekuwa kimya sana.
Basically, kwa sababu walio wengi hawafungamani na Watawala au Waoinzani.
Matokeo yake, sauti zinazosikika ni za MACHAWA.
Sasa tuseme imetosha.
Tupaze sauti zetu.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Wao ndiyo wanaamua nani wametangaze kama mshindi...

Cc: Mahondaw
Mkuu Smart911,
Wametuchukulia powa kwa muda mrefu sana mpaka wamejisahau.
Tukiamua kupaza sauti zetu, zikaenea Tanzania nzima, mpaka zikavuka Mipaka ya Nchi yetu, watasikiliza.
Zama hizi za Social Media, ndiyo wakati wa wasio na sauti.
Tupaze sauti zetu.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Naunga mikono hoja,
Watanzania ikibidi katika kituo cha kupiga kura tujigawe,wa ccm upande wao na upinzani upande wao,ijulikane kabla hata ya kura kupigwa
Nakubaliana na wewe.
Wapiga Kura tuhimize thamani ya Kura zetu.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Mifumo inaweza kusaidia kuimarisha imani ya umma katika mchakato wa uchaguzi na kuleta uwazi zaidi kwenye upigajinna kuhesabu kura:

1. Uchaguzi wa Kidijitali: Kutumia mifumo ya kidijitali kwa ajili ya kuhesabu kura inaweza kuongeza uwazi. Hata hivyo, ni muhimu kuhakikisha mfumo huo unakuwa salama na unapatikana kwa umma.

2. Vituo vya Uhesabuji Kura vya Hadhara: Kuweka vituo vya kuhesabu kura ambavyo vinapatikana kwa umma, ambapo waangalizi na wawakilishi wa vyama wanaweza kushuhudia mchakato mzima.

3. Vidokezo vya Kura (Ballot Tracking): Kutoa mfumo wa kufuatilia kura zinazopigwa, ambapo wapiga kura wanaweza kufuatilia kura zao hadi mwisho wa mchakato wa kuhesabu.

4. Ushirikishwaji wa Waangalizi wa Tatu: Kuleta waangalizi wa kimataifa au wa ndani ambao wanaweza kushiriki katika mchakato wa uchaguzi na kuangalia uhalali wa mchakato wa kuhesabu kura.

5. Ripoti za Mara kwa Mara: Kutolewa kwa ripoti za mara kwa mara kuhusu mchakato wa kuhesabu kura ili kuweka umma informed na kuimarisha uwazi.

6. Kurekodi na Kutangaza Matokeo kwa Haraka: Matokeo ya awali yanaweza kutangazwa haraka ili kupunguza nafasi za udanganyifu na kuweka uwazi.
Mkuu "milele Amina"
Kwa yote uliyoandika, naomba niseme, "Iwe hivyo MILELE DAIMA".
Tupaze sauti zetu.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Njia pekee ya Watanzania kuheshimiwa na Wawakilishi wetu ni kuhakikisha kwamba Kura zetu zinahesabiwa katika mazingira ya uwazi kwenye kila Kituo cha Kupigia Kura, na matokeo hayo yawe rasmi.

Tabia ya kufukuza Wapiga Kura kwenye Vituo vya Kupiga Kura ikomeshwe ili Mshindi halali ajulikane.
Hili halihitaji Azimio la Bunge wala Mswada wowote wa Sheria.

Wananchi tukiamua na kushinikiza, hili linawezekana kufanyika kwenye Uchaguzi Mkuu Novemba mwaka huu 2025
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
We ndio watanzania? Watanzania wana wawakilishi wao wa kuwasemea, tafuta fursa ya kwenda kuwawakilisha hao watanzania kwanza
 
Back
Top Bottom