Pre GE2025 Watanzania tunataka kura zetu zihesabiwe wazi wazi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kura zetu Wapiga Kura kuhesabiwa kwa Uwazi, kwenye Kituo cha Kupiga Kura, ni utaratibu unaoweza kufanyika katika mazingira ya Sheria na Kanuni za Uchaguzi zilizopo.
Ukianza kutaja Tume ya Uchaguzi, utatakiwa utaje Bunge na Ratiba zake pamoja na mlolongo mwingine ambao ni mahususi kwa Vyama vya Siasa.
Tusiende huko.
Sisi tupaze sauti zetu kama Wapiga Kura.
Wapiga Kura wasio Wanachama wa Chama chochote, nasikia ni Asilimia takriban 75 ya Wapiga Kura wote Nchini.
Hili ni Jeshi Kubwa sana.
Rais akaaye Ikulu, anapelekwa Ikulu na Kura za Watanzania ambao siyo Wanachama wa CCM, wala CHADEMA, wala ACT wala wa kile Chama cha Mzee wa Ubwabwa.
Hii Asilimia 75 haina Mawakala kwenye Chumba cha Kupigia Kura.
Namna pekee ya Wapiga Kura hawa kutendewa Haki, ni Kura zao kuhesabiwa kwa UWAZI.
Tupaze sauti zetu.
Hili linawezekana.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
Changamoto Iko hivi hizo kura hesabuni na kuzilinda lakini nitakaye zitangaza ni mimi mgurugenzi wa halmashauri husika nikitangaza matokeo tofauti mtanifanya nini , inamaana mmesahau kinacho fanyika?
 
Umeeleza kitu ambacho ndicho Huwa kinatokea. Umeelezea uhalisia.
Tutoke kidogo kwenye MADA, nitoe mfano, nikitumia Uchaguzi Mkuu uliopita wa CHADEMA.
Baada ya Kura kuhesabiwa kwa Uwazi, wafuatiliaji walikuwa wameshajua Mwenyekiti atakuwa yupi kati ya Wagombea watatu waliokuwa kwenye kinyang'aniro.
Sasa, mathalani, (kwa kinadharia tu), ingetokea Msimamizi wa Uchaguzi akamtangaza Mgombea ambaye, mbele ya macho ya Wapiga Kura, hakuwa ameshinda!!!!
Hivi sasa CHADEMA kingekuwa MAREHEMU!
Sasa tuje kwenye CHAMA Tawala.
Mkurugenzi, ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi, (na Mteule wa Mgombea Urais), amtangaze Mshindi tofauti na uhalisia, hali itakuwaje?
Mimi naamini kwamba, siku zote Mwizi ni mwoga.
The guilty are always afraid!
Ndiyo sababu Mabomu ya Machozi Huwa yanapigwa, ili Wapiga Kura wasambaratike, Kura ziibiwe.
Wezi wa Kura ni waoga siku zote.
Tukishinikiza, Kura zikahesabiwa kwa Uwazi, Wezi wataogopa KUIBA wazi wazi.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Polisi wamenunuliwa magari mapya kuja kuumiza watanzania wakati wa uchaguzi mkuu
Hii yote ni uthibitisho uli wazi kwamba Watawala wanawaogopa Wapiga Kura.
Kama Wapiga Kura tungekuwa hatuogopwi, Chama Tawala kingetumia Kodi zetu kuimarisha Huduma kama Elimu, Afya na Miundombinu.
Badala yake, tunaimarisha Jeshi la Polisi wakati Walimu Mashuleni hawatoshi.
Na wachache waliopo wana maslahi duni.
Wakati huo huo, kwa pesa za Walipa Kodi ambao ndio Wapiga Kura, watoto wa Watawala wanasoma Shule Binafsi.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Anasema wakishapiga kura watapatwa na njaa gafla wawahi home wakale
Wassira anyimwe visingizio vyake vya kizee.
Hivi hakuna umri wa kustaafu Siasa?
Wanasiasa wanaochipukia watapata nafasi za kuongoza mwaka gani?
Tupaze sauti zetu.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Wassira anyimwe visingizio vyake vya kizee.
Hivi hakuna umri wa kustaafu Siasa?
Wanasiasa wanaochipukia watapata nafasi za kuongoza mwaka gani?
Tupaze sauti zetu.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
Kweli kabisaaa jitu zee bado linapewa nafasii
 
Umeeleza kitu ambacho ndicho Huwa kinatokea. Umeelezea uhalisia.
Tutoke kidogo kwenye MADA, nitoe mfano, nikitumia Uchaguzi Mkuu uliopita wa CHADEMA.
Baada ya Kura kuhesabiwa kwa Uwazi, wafuatiliaji walikuwa wameshajua Mwenyekiti atakuwa yupi kati ya Wagombea watatu waliokuwa kwenye kinyang'aniro.
Sasa, mathalani, (kwa kinadharia tu), ingetokea Msimamizi wa Uchaguzi akamtangaza Mgombea ambaye, mbele ya macho ya Wapiga Kura, hakuwa ameshinda!!!!
Hivi sasa CHADEMA kingekuwa MAREHEMU!
Sasa tuje kwenye CHAMA Tawala.
Mkurugenzi, ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi, (na Mteule wa Mgombea Urais), amtangaze Mshindi tofauti na uhalisia, hali itakuwaje?
Mimi naamini kwamba, siku zote Mwizi ni mwoga.
The guilty are always afraid!
Ndiyo sababu Mabomu ya Machozi Huwa yanapigwa, ili Wapiga Kura wasambaratike, Kura ziibiwe.
Wezi wa Kura ni waoga siku zote.
Tukishinikiza, Kura zikahesabiwa kwa Uwazi, Wezi wataogopa KUIBA wazi wazi.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
Hata mimi nakubaliana na wewe, tunapigwa wakati wa kutangaziwa kura na mkurugenzi kura haziibiwi kwenye vituo vya kupigia Kura nilishawahi kushiriki kama wakala, kwanini kura zinaibwa na zinaibwaje, tujadiliane, pia kwanini mkurugenzi hupotea kwa muda mrefu wakati huku wadau wa uchaguzi wanahitaji taarifa za uchaguzi, je huugua kaugonjwa ka uchaguzi? Kikikiki

Zitakuwa zinafaulishwa swali fikirishi nani hufaulisha hapa Ndiyo patamu labda tujadili pia
 
Kweli kabisaaa jitu zee bado linapewa nafasii
Kama Kanuni za Uchaguzi, ndani ya Chama Tawala zingekuwa zinafuatwa, wanaCCM wangetangaziwa ili wachukue Fomu.
Kilichotokea Dodoma ni mwendelezo wa kudharau kauli ya Wapiga Kura ndani ya CCM.
Tupaze sauti.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Hata mimi nakubaliana na wewe, tunapigwa wakati wa kutangaziwa kura na mkurugenzi kura haziibiwi kwenye vituo vya kupigia Kura nilishawahi kushiriki kama wakala, kwanini kura zinaibwa na zinaibwaje, tujadiliane, pia kwanini mkurugenzi hupotea kwa muda mrefu wakati huku wadau wa uchaguzi wanahitaji taarifa za uchaguzi, je huugua kaugonjwa ka uchaguzi? Kikikiki

Zitakuwa zinafaulishwa swali fikirishi nani hufaulisha hapa Ndiyo patamu labda tujadili pia
Hapa ndipo Hoja hii inapata mashiko.
Matokeo kwenye Kituo cha Kupiga Kura yakihesabiwa kwa uwazi, Fomu zikajazwa na kusainiwa, zikawa rasmi, Mkurugenzi atapata shida sana KUBATILISHA MATOKEO.
Nchi na Dunia itakuwa imeshuhudia idadi sahihi kwenye kila Kituo cha Kupiga Kura.
Kazi ya Mkurugenzi ni kujumlisha kinachojulikana tayari.
Hakika, kama ataamua KUIBA, itakuwa rahisi kuthibitisha WIZI wake.

Hapo Ndiyo patamu wewe unaongea kirahisi je ikija mijitu iliyoshiba na silaha tena nzito za moto unafanyaje?

Do not take things for granted
 
Njia pekee ya Watanzania kuheshimiwa na Wawakilishi wetu ni kuhakikisha kwamba Kura zetu zinahesabiwa katika mazingira ya uwazi kwenye kila Kituo cha Kupigia Kura, na matokeo hayo yawe rasmi.

Tabia ya kufukuza Wapiga Kura kwenye Vituo vya Kupiga Kura ikomeshwe ili Mshindi halali ajulikane.
Hili halihitaji Azimio la Bunge wala Mswada wowote wa Sheria.

Wananchi tukiamua na kushinikiza, hili linawezekana kufanyika kwenye Uchaguzi Mkuu Novemba mwaka huu 2025

Asante!zipigwe hadharani,zitumbukizwe kwenye maboksi yanayoonyesha ndani,zihesabiwe hadharani,zitangazwe hadharani na mshindi atangazwe mbele ya kadamnazi ya walipiga kura,tuachane na mabungutu soksini.
 
Mkuu, CCM wamezoea kula vibudu, kwa uzoefu huo vya kuchinja kamwe hawataviweza. Kuokoteza mizoga ndiyo ibada na jadi yao.
 
Asante!zipigwe hadharani,zitumbukizwe kwenye maboksi yanayoonyesha ndani,zihesabiwe hadharani,zitangazwe hadharani na mshindi atangazwe mbele ya kadamnazi ya walipiga kura,tuachane na mabungutu soksini.
Atangazwe hapohapo nakubaliana na hilo wapiga kura hatuhitaji mawakala
 
Asante!zipigwe hadharani,zitumbukizwe kwenye maboksi yanayoonyesha ndani,zihesabiwe hadharani,zitangazwe hadharani na mshindi atangazwe mbele ya kadamnazi ya walipiga kura,tuachane na mabungutu soksini.
Kura zihesabiwe hadharani pia matokeo yatangazwe hadharani baada ya kupata mgombea aruhusu kura zichomwe hakuna kuondoka nazo kuondoka nazo Ndiyo kuziiba kwenyewe, kikikiki nilisema tutapata suluhisho tu na suluhisho Ndilo hilo

Zoezi hili litapunguza kesi za wagombea kwenda mahakamani

Sikuhizi taarifa zinaingizwa kwenye mfumo wa kidigitali hakuna mbamba, yaani mfumo utaona matokeo yote ya siku hiyo
 
Hapo Ndiyo patamu wewe unaongea kirahisi je ikija mijitu iliyoshiba na silaha tena nzito za moto unafanyaje?

Do not take things for granted
I fully agree.
We can not take things for granted!
That's why we need to raise our voices before "hiyo mijitu iliyoshiba na silaha, tena nzito, haijafika"
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Asante!zipigwe hadharani,zitumbukizwe kwenye maboksi yanayoonyesha ndani,zihesabiwe hadharani,zitangazwe hadharani na mshindi atangazwe mbele ya kadamnazi ya walipiga kura,tuachane na mabungutu soksini.
Hakuna kuingia kwenye kichumba peke yako utakuwa mpweke, hahaha 😂
 
Back
Top Bottom