Pre GE2025 Watanzania tunataka kura zetu zihesabiwe wazi wazi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Haya ndiyo tunayotakiwa kujadili katika kupaza sauti zetu.
Kura yako na yangu, na ya Watanzania wenzetu wote, inampeleka Mtawala Ikulu, au Mbunge Mjengoni.
Ni haki na wajibu kudai heshima stahiki kwa Kura zetu.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
Mimi siyo yule mzee wa mikaka 80 ambaye betri lake liko full charged, (fulu mzuka)
 
Mimi siyo yule mzee wa mikaka 80 ambayo betri liko full charged
Ukitaja miaka 80, naanza kujiuliza kilichojiri kwenye Chama Tawala chetu.
Aliyeachia, akisema amezeeka, na anahitaji kupumzika, ana umri wa miaka 73.
Aliyepokea Kijiti ana miaka 80!
Hakika, kama Wapiga Kura ndani ya CCM wangeheshimika, hili lisingetokea.
Nani hajui kwamba ndani ya CCM hiyo hiyo, wapo wengi wenye uwezo, lakini wanapuuzwa?
Huu Utamaduni wa kupuuza Kura ya Mpiga Kura umeota mizizi hata ndani ya Vyama vya Siasa.
Sasa tuseme imetosha.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
miss kizimkazi hawezi kulukubali hili
Tushikilie na tukaze Uzi.
Mpiga Kura ni mimi na wewe.
Kura yako, yangu, na ya Watanzania wenzetu inampa Madaraka Mtawala anayeingia Ikulu kuanzisha au Kuzuia Vita.
Kura yako na yangu na ya Watanzania wenzetu inamfanya Mtanzania mwenzetu, mmoja, kuwa Amiri Jeshi Mkuu.
Kura zetu hizi ni kitu kikubwa sana.
Tuhakikishie zinaheshimiwa ipasavyo.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Unafikiri babu Wassira na aliyemteua wako tayari kwa kuhesabu kura kwa wazi?
Ndiyo sababu ni lazima tupaze sauti.
Wanapokubali kwenda Ikulu na Bungeni kwa Kura zetu, lazima pia wakubali kuziheshimu Kura zetu hizo.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Ukitaja miaka 80, naanza kujiuliza kilichojiri kwenye Chama Tawala chetu.
Aliyeachia, akisema amezeeka, na anahitaji kupumzika, ana umri wa miaka 73.
Aliyepokea Kijiti ana miaka 80!
Hakika, kama Wapiga Kura ndani ya CCM wangeheshimika, hili lisingetokea.
Nani hajui kwamba ndani ya CCM hiyo hiyo, wapo wengi wenye uwezo, lakini wanapuuzwa?
Huu Utamaduni wa kupuuza Kura ya Mpiga Kura umeota mizizi hata ndani ya Vyama vya Siasa.
Sasa tuseme imetosha.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
Nini kifanyike CCM ikiendelea kukataa, (chama dola), je tuwachalaze mijeledi?

Hivi watu wabishi kwenye jambo lenye fikra chanya la kitaifa dawa yao ni ipi yaani wanao jizima data, a.k.a kuahirisha kufikiri kizalendo
 
Tushikilie na tukaze Uzi.
Mpiga Kura ni mimi na wewe.
Kura yako, yangu, na ya Watanzania wenzetu inampa Madaraka Mtawala anayeingia Ikulu kuanzisha au Kuzuia Vita.
Kura yako na yangu na ya Watanzania wenzetu inamfanya Mtanzania mwenzetu, mmoja, kuwa Amiri Jeshi Mkuu.
Kura zetu hizi ni kitu kikubwa sana.
Tuhakikishie zinaheshimiwa ipasavyo.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
Watatuua mkuu na mabunduki tunayoyanunua wenyewe kwa kodi zetu
 
Binadamu akipata changamoto huamsha ubongo na kubuni mbinu za kukabiliana nazo, mimi nimegundua ukiwa unatafuta suluhisho,(solution) unajilaza ndani ya dk chache unapata suluhisho (solution)

Hebu hili jambo tulichukulie kama joka kubwa lomeingia nyumbani kwako inatakiwa upambane nalo kwa kuliua ili lisirudi tena
 
Nini kifanyike CCM ikiendelea kukataa, (chama dola), je tuwachalaze mijeledi?

Hivi watu wabishi kwenye jambo lenye fikra chanya la kitaifa dawa yao ni ipi yaani wanao jizima data, a.k.a kuahirisha kufikiri kizalendo
Hii ndiyo Hoja yenyewe.
Wanajizima Data, kwa sababu tumejitoa ufahamu tukawaaminisha kwamba wanachotamka katika midomo yao, sisi tutapongeza na kucheza Mdundiko.
Sasa tuseme imetosha.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Watatuua mkuu na mabunduki tunayoyanunua wenyewe kwa kodi zetu
Kabla hawajatuua, kabla ya siku ya Uchaguzi Mkuu, tupaze sauti zetu.
Watatusikia, na kwa kuwa wao pia wana Mioyo ya Nyama, kama sisi, na kwa kuwa Mungu wetu ni Mungu wa Haki, muujiza utatokea.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Binadamu akipata changamoto huamsha ubongo na kubuni mbinu za kukabiliana nazo, mimi nimegundua ukiwa unatafuta suluhisho,(solution) unajilaza ndani ya dk chache unapata suluhisho (solution)

Hebu hili jambo tulichukulie kama joka kubwa lomeingia nyumbani kwako inatakiwa upambane nalo kwa kuliua ili lisirudi tena
Benny Haraba, maneno yako yawe CHACHU ya mwanga katika Mioyo ya Watanzania wote.
Naungana na wewe nikisema, tunaweza kulitoa majumbani mwetu, hilo Joka Kubwa lililotuvamia.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Uko sahihi Vessel.
Ndiyo sababu ni muhimu sana kuoaza sauti, ndani na nje ya mipaka yetu kwamba TUNATAKA KURA ZETU ZIHESHIMIKE.
Ili Kura zetu ZIHESHIMIKE, tunataka zihesabiwe kwa Haki na kwa Uwazi.
Kwa Sheria hizi hizi na Kanuni za Uchaguzi hizi hizi.
Sheria hizi hazina na hazirihusu uwazi uteuzi wa tume unafanywa na mwajiri ili waganye kazi ya mwajiri kwa kanuni na taratibu zake ukishindwa uwezo wa kukufuta ajira anao na kuzifuta haki na stahiki zao,itawezekanaje tume kama hiyo kuwa huru.Ni bora tume iundwe kutoka wazalendo wa taifa hili ambao wako tayari hata kujitolea kuona uwazi,uhuru na haki ya kuchagua na kuchaguliwa kwa haki ikitendeka,katika vigezo na viwango vinavyokubalika na sii uhunu wa misuli,vifua na mitutu na maji washawasha.
 
Kura zetu Wapiga Kura kuhesabiwa kwa Uwazi, kwenye Kituo cha Kupiga Kura, ni utaratibu unaoweza kufanyika katika mazingira ya Sheria na Kanuni za Uchaguzi zilizopo.
Ukianza kutaja Tume ya Uchaguzi, utatakiwa utaje Bunge na Ratiba zake pamoja na mlolongo mwingine ambao ni mahususi kwa Vyama vya Siasa.
Tusiende huko.
Sisi tupaze sauti zetu kama Wapiga Kura.
Wapiga Kura wasio Wanachama wa Chama chochote, nasikia ni Asilimia takriban 75 ya Wapiga Kura wote Nchini.
Hili ni Jeshi Kubwa sana.
Rais akaaye Ikulu, anapelekwa Ikulu na Kura za Watanzania ambao siyo Wanachama wa CCM, wala CHADEMA, wala ACT wala wa kile Chama cha Mzee wa Ubwabwa.
Hii Asilimia 75 haina Mawakala kwenye Chumba cha Kupigia Kura.
Namna pekee ya Wapiga Kura hawa kutendewa Haki, ni Kura zao kuhesabiwa kwa UWAZI.
Tupaze sauti zetu.
Hili linawezekana.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Mkuu Benjamin Netanyahu, tusaidiane tupaze sauti.
Wawakilishi wanaongezeana Posho huku wakitupandishia Vifurushi vya DATA ili tushindwe kuwasiliana.
Inabidi wajue kuwa Wapiga Kura tumeshika Mpini, wao wameshika Makali.
Wakiendeleza mizaha, wakatike vidole.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
Sahihi kabisa mkuu ndiyo maana pamoja na vitisho tunapitia lakini hatunyamazi, lazima mwaka huu tuwanyooshe vizuri hawa majangili.
 
Ndio maana Trump amesema viongozi wa kiafrika wapumbavu wananunua silaha kuja kuua raia wao
Kitu cha msingi hapa ni kwamba tusikubali kufa kibubu.

Back
Top Bottom