Pre GE2025 Watanzania tunataka kura zetu zihesabiwe wazi wazi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Njia pekee ya Watanzania kuheshimiwa na Wawakilishi wetu ni kuhakikisha kwamba Kura zetu zinahesabiwa katika mazingira ya uwazi kwenye kila Kituo cha Kupigia Kura, na matokeo hayo yawe rasmi.

Tabia ya kufukuza Wapiga Kura kwenye Vituo vya Kupiga Kura ikomeshwe ili Mshindi halali ajulikane.
Hili halihitaji Azimio la Bunge wala Mswada wowote wa Sheria.

Wananchi tukiamua na kushinikiza, hili linawezekana kufanyika kwenye Uchaguzi Mkuu Novemba mwaka huu 2025
Mbona kura kwenye vituo huwa zina hesabika kwa uwazi tatizo ni kukosa mawakala, CCM wakizidiwa wakati wa uchaguzi huenda maporini lejea taarifa ya mkuu wa wilaya aliye tumbuliwa
 
Kazi ya mawakala wa vyama nini? Huwaamini mawakala wako au?
 
Huwa wanakuja na kauli za uchawa zisizo na mashiko, kama hii hapa...
👇
Wassira tumueleze kwamba Watanzania walikimbia Nchi kwa sababu ya Kura zao kutohesabiwa kwa uwazi.
Anayeshinda kwa haki baada ya Kura kuhesabiwa kwa uwazi, kamwe hawezi kuwarisha Wapiga Kura
 
Samia hakubali hata kwa mikwaju.

Yani mnataka kumuumbua na kura za familia yake tu atakazopata.
 
Mbona kura kwenye vituo huwa zina hesabika kwa uwazi tatizo ni kukosa mawakala, CCM wakizidiwa wakati wa uchaguzi huenda maporini lejea taarifa ya mkuu wa wilaya aliye tumbuliwa
Kura zikihesabiwa mbele ya macho ya waliopiga Kura kwenye kila Kituo, uharamia wa kwenda porini hautakuwepo.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI
 
Kunapokuwa na mawakala mbona Kura huhesabiwa kwa uwazi lakini hawaruhusiwi kutangaza matokeo, kwa maana eti wasimamizi wana akili za kusimamia upigaji kura na kuzihesabu
lakini za kutangaza matokeo zina hama, yaani zina hamia kwa mgurugenzi wa halmashauri
Hata mkilinda kura anayetangaza matokeo ni mkurugenzi wa halmashauri
 
Kazi ya mawakala wa vyama nini? Huwaamini mawakala wako au?
Mawakala ni wa Wagombea.
Wapiga Kura hatuna Mawakala.
Tunataka Kura zetu ZIHESHIMIKE.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Kunapokuwa na mawakala mbona Kura huhesabiwa kwa uwazi lakini hawaruhusiwi kutangaza matokeo, kwa maana eti wasimamizi wana akili za kusimamia upigaji kura na kuzihesabu
lakini za kutangaza matokeo zina hama, yaani zina hamia kwa mgurugenzi wa halmashauri
Hata mkilinda kura anayetangaza matokeo ni mkurugenzi wa halmashauri
Wapiga Kura hatuna Mawakala.
Tunataka Kura zihesabiwe kwa uwazi ili Wagombea wa Vyama Vyote, pamoja na Mawakala wao watuheshimu sisi Wapiga Kura.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Wapiga Kura hatuna Mawakala.
Tunataka Kura zihesabiwe kwa uwazi ili Wagombea wa Vyama Vyote, pamoja na Mawakala wao watuheshimu sisi Wapiga Kura.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
Wazo zuri hao wasimamizi hawana mamlaka ya kutangaza matokeo kwasababu eti wana akili za kusimamia upigaji kura na kuzihesabu lakini za kutangaza matokeo huwa hawana
 
Full Blood Picture, tupaze sauti ili Wassira na wenzake wote waone umuhimu wa kutuheshimu sisi Wapiga Kura.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
Hiyo nk kweli, hawa wanatufanya kama hatujitambui. Sasa ni wakati wa kupaza sauti kwa ajili sisi wenyewe wananchi. Ukiona mzee mzima anapiga kelele na kutoa matusi ujue hali si nzuri.
 
Back
Top Bottom