Pre GE2025 Watanzania tunataka kura zetu zihesabiwe wazi wazi

Pre GE2025 Watanzania tunataka kura zetu zihesabiwe wazi wazi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Njia pekee ya Watanzania kuheshimiwa na Wawakilishi wetu ni kuhakikisha kwamba Kura zetu zinahesabiwa katika mazingira ya uwazi kwenye kila Kituo cha Kupigia Kura, na matokeo hayo yawe rasmi.

Tabia ya kufukuza Wapiga Kura kwenye Vituo vya Kupiga Kura ikomeshwe ili Mshindi halali ajulikane.
Hili halihitaji Azimio la Bunge wala Mswada wowote wa Sheria.

Wananchi tukiamua na kushinikiza, hili linawezekana kufanyika kwenye Uchaguzi Mkuu Novemba mwaka huu 2025
CCM hawatoboi kwa njia hiyo
 
Kura za Samia,nyie angaikeni na ubunge
Tuanze naye huyu huyu Madame President SSH.
Fikiria Kura zikihesabiwa kwa uwazi, na akashinda kwa kishindo, heshima ya Taifa letu itapaa juu zaidi na zaidi.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Wazo zuri hao wasimamizi hawana mamlaka ya kutangaza matokeo kwasababu eti wana akili za kusimamia upigaji kura na kuzihesabu lakini za kutangaza matokeo huwa hawana
Kanuni zinasema Matokeo yabandikwe nje ya Kituo cha Kupigia Kura.
Tafsiri yake ni kwamba Wasimamizi wanayo Mamlaka ya kutangaza Matokeo.
Tukipaza Sauti zetu zetu, Haki itatendeka.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Angalia mkutano mkuu wa CCM ndiyo utajua hiyo haiwezekani.
Utaratibu wa CCM yenyewe unakiukwa huku Wajumbe wakipumbazwa na Wasanii.
Huu ni muda wa Wapiga Kura kuamka na kushikamana.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Hiyo nk kweli, hawa wanatufanya kama hatujitambui. Sasa ni wakati wa kupaza sauti kwa ajili sisi wenyewe wananchi. Ukiona mzee mzima anapiga kelele na kutoa matusi ujue hali si nzuri.
Wapiga Kura tumejisahau kwa kipindi kirefu sana.
Matokeo yake Wawakilishi wetu Bungeni wanajiwakilisha wao na familia zao, huku wakitupuuza sisi.
Fikiria wanajiongezea Posho wakati Watumishi wa Serikali hawapati nyongeza stahiki za Mishahara.
Sasa tupaze sauti tudai heshima yetu stahiki.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI MKUTANO MKUU
 
Hiyo nk kweli, hawa wanatufanya kama hatujitambui. Sasa ni wakati wa kupaza sauti kwa ajili sisi wenyewe wananchi. Ukiona mzee mzima anapiga kelele na kutoa matusi ujue hali si nzuri.
Ameliamsha dude, mimi nimekuwa nafuatilia kwa karibu kuhusu kuhoji tatizo la kuhoji linaanza kwenye ngazi ya familia kuna vitu ukivihoji utaambiwa kama umekuwa ondoka hii tabia ya kukata ama kuwaziba watu midomo inabebwa kwenye ngazi zote za maisha kumbuka Kuna wadau walihoji kuhusu tozo za kwenye simu waliambiwa kama hawataki kuzilipa waende burundi

Hitimisho mwenye mamlaka ya yote haya ni mwananchi, yaani jamii, namfahamu kwamba tunaishi kwenye jamii ya kanyaga twende yaani jamii ya bora liende jamii ambayo haiwezi kuchakata fikra chanya na hasi pia unaweza kuisafisha ubongo ikafikiri unavyotaka wewe, lakini mafuvu yakirudishiwa akili patakuwa hapatoshi
 
CCM hawatoboi kwa njia hiyo
Mkuu Benjamin Netanyahu, tusaidiane tupaze sauti.
Wawakilishi wanaongezeana Posho huku wakitupandishia Vifurushi vya DATA ili tushindwe kuwasiliana.
Inabidi wajue kuwa Wapiga Kura tumeshika Mpini, wao wameshika Makali.
Wakiendeleza mizaha, wakatike vidole.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Kanuni zinasema Matokeo yabandikwe nje ya Kituo cha Kupigia Kura.
Tafsiri yake ni kwamba Wasimamizi wanayo Mamlaka ya kutangaza Matokeo.
Tukipaza Sauti zetu zetu, Haki itatendeka.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
Ndiyo maana ya uchaguzi wa haki na huru lakini chaguzi zetu zinaendeshwa na wapumbavu, upumbavu ni kipaji, mpambu ni mtu aliyebobea kwenye jambo fulani lakini ana mapuuza hatekelezi majukumu yake kwa weledi, anajizima data
 
Uko sahihi Benny Haraba.
Sisi Wapiga Kura, kwa bahati mbaya kabisa, tumeendekeza upuuzi wa hawa wanaoendesha Chaguzi zetu.
Sasa tuseme imetosha.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Wakati nyie mnapiga kelele wana uzoefu wa kufanya vinginevyo, na wamesha jipanga, over
Ni kwa sababu wametuchukulia poa kwa muda mrefu.
Sasa tuseme imetosha.
[Because they have taken us for granted for so long.
It's time to say, 'enough is enough'.]
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Uko sahihi Benny Haraba.
Sisi Wapiga Kura, kwa bahati mbaya kabisa, tumeendekeza upuuzi wa hawa wanaoendesha Chaguzi zetu.
Sasa tuseme imetosha.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
Changamoto ipo hivi anayeruhusiwa kutangaza matokeo ni mkurugenzi hayo matokeo mliyo yapata huko mkurugenzi akitangaza tofauti mtamfanya nini sheria zinasemaje?, Vile vile mkurugenzi akijizima data, a.k.a kuahirisha kufikiri kizalendo utamfanya. nini
 
Changamoto ipo hivi anayeruhusiwa kutangaza matokeo ni mkurugenzi hayo matokeo mliyo yapata huko mkurugenzi akitangaza tofauti mtamfanya nini sheria zinasemaje?
Haya ndiyo tunayotakiwa kujadili katika kupaza sauti zetu.
Kura yako na yangu, na ya Watanzania wenzetu wote, inampeleka Mtawala Ikulu, au Mbunge Mjengoni.
Ni haki na wajibu kudai heshima stahiki kwa Kura zetu.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU
 
Back
Top Bottom