Unaweza isvyo sahihi,
Kwamba kura fake zihesabiwe Kwa uwazi?
Hukujifunza uchaguzi wa Serikali za mitaa?
Rudi andika UPYA kwamba,
Tunataka Tume huru na Katiba mpya kabla ya Uchaguzi wa October,
Tupate Sanduku la kura lisilonajisiwa.
Ndipo tupige kura na zihesabiwe Kwa uwazi.
Na bila Tume huru ya Uchaguzi, uchaguzi utayeyuka.
Sijui umeelewa?
Rabbon, mimi na wewe, yaani sisi wote, tuko sahihi.
Kupaza sauti ni njia sahihi.
Tena njia ambayo Babu Wassira hawezi kuwadanganya Wapiga Kura waipuuze, kama alivyowaambia Watanzania wenzetu kule Musoma, siku walipompokea.
Aliwaambia kuwa Watanzania wanataka MAENDELEO, siyo Katiba Mpya na Wasanii wa CCM wakamshangilia.
Je, anaweza kusimama hadharani na kutamka kwamba Watanzania hawataki KURA ZAO ZIHESABIWE KWA UWAZI?
Katiba Mpya na Tume Huru ndiyo suluhisho Kuu.
Ili kulifikia, kwa hawa Watawala ambao wanajua kwamba Wapiga Kura hawawataki, upo umuhimu wa kutumia kila nyenzo tuliyonayo.
Nyenzo ambayo hawawezi kutunyang'anya ni SAUTI ZETU.
Tupaze sauti.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU