Nimesoma kwa makini ilichoandika.
Bandiko lako limeegemea upande wa Mfumo wa hivi Vyama vyetu vya Kisiasa.
Na hicho ndicho wanachotamka Watawala.
Kwamba, Wananchi wa kawaida, ambao ndio Wapiga Kura, WAJITENGE NA MADAI YA VYAMA VYA SIASA, ili kesho na kesho kutwa Babu Wassira aende kwenye Majukwaa na kuwaambia watu kwamba hayo ni "mambo ya Waoinzani".
Hoja yangu mimi ni kuhusu SISI WAPIGA KURA, tena wengi wetu, (majority), tusio Wanachama wa Chama chochote cha Siasa.
Nimemskia Mchambuzi wa Siasa na Ujasusi, ndugu yetu Evarist Chahali, akisema kwamba Asilimia 80 ya Wapiga Kura, siyo Wanachama wa Chama chochote cha Siasa.
Kundi hilo ndilo tunaotakiwa kupaza sauti zetu.
Kwenye Vituo vya Kupiga Kura, CHADEMA wanakuwa na Wakala.
CCM wanakuwa na Wakala.
Sisi tusio na Wakala, tena ambao ndio MAJORITY, haki yetu inalindwa na nani?
Mlinzi pekee wa Haki yetu ni KURA ZETU KUHESABIWA KWA UWAZI, na zitangazwe kuwa rasmi.
Tupaze sauti zetu.
#KURA ZIHESABIWE KWA UWAZI UCHAGUZI MKUU