Watanzania tunazikuza sana timu za Kiarabu, hazina ubora wa kutisha kama tunavyoziongelea

Watanzania tunazikuza sana timu za Kiarabu, hazina ubora wa kutisha kama tunavyoziongelea

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Tukiweka ushabiki pembeni, kwa miaka ya hivi karibuni, club zetu za Simba na Yanga zimekuwa daraja moja na timu za kiarabu ambazo tunaziona kama ni daraja la juu sana kulinganisha na za kwetu.

Ukisikia wachambuzi wakidai Percy Tau analipwa millioni 250 kwa mwezi utadhani kuwa ni nchezaji wa class ya juu sana ila uhalisia wake tumeona

Ngoja nitaje mifano kadhaa inayothibitisha tunazikuza tu hizi timu kuliko
Mfano Yanga iliitoa club Africain kwa kuifunga nyumbani, pia iliongoza kundi kwenye Shirikisho iliyokuwa na US Monstir ya Tunisia, na Fainali dhidi ya USM Alger Yanga wangeweza kushinda sema tu ni ile presha ya kucheza fainali kwa mara ya kwanza na walitoka tu kwa kanuni ya goli la ugenini na sio aggregate

Simba pia tumeona ikicheza na Wydad, al Ahlly, JS Soura, na kuzifunga au kutoa sare, hata kama ikifungwa kunakuwa hakuna tofauti kubwa sana ya ubora ile useme kuwa imekuwa out classed, zinakuwa ni timu za viwango vinavyofanana.

Ni muda sasa kuanza kuona timu zetu sio za kinyonge tena kwa timu za Kaskazini, na Simba hatutakiwi kushangilia hii draw bali kusiikitika kwani uwezo wa kuwafunga Ahly tunao.
 
Ni muda sasa kuanza kuona timu zetu sio za kinyonge tena kwa timu za Kaskazini, na Simba hatutakiwi kushangilia hii draw bali kusiikitika kwani uwezo wa kuwafunga Ahly tunao
Uko sahihi kabisa, mfano kama game ya leo kocha angeanza na plani nzuri, tulikuwa tunawafunga kwao. Au ile game ya kwanza tungemaliza mchezo hapa hapa.
 
Simba huwa INA mashabiki wajinga sana....wanaona fahari kucheza kimataifa lakini kiuhalisia wanatumika kama ngazi kuzipatia timu zingine maujiko na mafanikio.
Mashabiki wa simba utasikia "tumetoka kiume" na blahblah nyingi.
In short mashabiki wa simba ni malofa.
Refer hata hapa jukwaani.
 
Al Ahly ni wabovu, wale Wydad walikuwa na matatizo ya bechi la ufundi. Kaka vilabu vikubwa kama hivi usifikiri ni kama Azam au Ihefu, jamaa mpira wanajua haswa.

Tanzania tunahitaji uwekezaji mkubwa ktk soka ili kufika hapo walipo, timu kama Mamelod wanaoipasua Al Ahly nje ndani usifikiri Mamelod ni kama Simba au Yanga, Mamelod wapo vizuri ktk uwekezaji.
 
Kwa ufupi tu, leo vibonde wawili walikutana.

Kwa sisi tulio neutral tunaotazama kwa ajili tu ya burudani ilikuwa kero tupu. Yaani Simba wanacheza ovyo, Al Ahly nao wanacheza ovyo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
]
Tukiweka ushabiki pembeni, kwa miaka ya hivi karibuni, club zetu za Simba na Yanga zimekuwa daraja moja na timu za kiarabu ambazo tunaziona kama ni daraja la juu sana kulinganisha na za kwetu
Ukisikia wachambuzi wakidai Percy Tau analipwa millioni 250 kwa mwezi utadhani kuwa ni nchezaji wa class ya juu sana ila uhalisia wake tumeona

Ngoja nitaje mifano kadhaa inayothibitisha tunazikuza tu hizi timu kuliko

Mfano Yanga iliitoa club Africain kwa kuifunga nyumbani, pia iliongoza kundi kwenye Shirikisho iliyokuwa na US Monstir ya Tunisia, na Fainali dhidi ya USM Alger Yanga wangeweza kushinda sema tu ni ile presha ya kucheza fainali kwa mara ya kwanza na walitoka tu kwa kanuni ya goli la ugenini na sio aggregate

Simba pia tumeona ikicheza na Wydad, al Ahlly, JS Soura, na kuzifunga au kutoa sare, hata kama ikifungwa kunakuwa hakuna tofauti kubwa sana ya ubora ile useme kuwa imekuwa out classed, zinakuwa ni timu za viwango vinavyofanana

Ni muda sasa kuanza kuona timu zetu sio za kinyonge tena kwa timu za Kaskazini, na Simba hatutakiwi kushangilia hii draw bali kusiikitika kwani uwezo wa kuwafunga Ahly tunao
Huo nao ni uwekezaji. Hatukuzi timu tu bali hata dini za kiarabu, waarabu na kila ujinga wao. Bado wazungu nao kutukuzwa hadi kuabudiwa. Ni hatari kwa waswahili wasipoamka na kujitambua. Mtaliwa mpaka mkome
 
Sisi bado sana matokeo yasituvimbishe vichwa, uwanjani tuna butua butua nyingi ilhali wenzetu wakipata mpira wanafungua vyumba zinagongwa pasi sambusa

Tuna safari ndefu kufikia soka la ufundi
 
Warabu wanajua wanachokifanya uwanjani.
Kama anatafuta goli atalipata kama ni droo ataipata.

Simba uwezo mdogo kwa timu kubwa.
Simba imejitahidi sana
Mnawaabudu tu hawa waarabu, hawana la kutisha, sema ndio hivyo ngozi nyeusi na inferiority
 
Sisi bado sana matokeo yasituvimbishe vichwa, uwanjani tuna butua butua nyingi ilhali wenzetu wakipata mpira wanafungua vyumba zinagongwa pasi sambusa

Tuna safari ndefu kufikia soka la ufundi
Hawana kiwango cha kutisha hivyo, wanawaZidi Simba ila kidogo tu, Wydad na Ahly ambazo ndio timu bora zaidi Afrika, hawakuweza kuwa outclass Simba
 
Al Ahly ni wabovu, wale Wydad walikuwa na matatizo ya bechi la ufundi. Kaka vilabu vikubwa kama hivi usifikiri ni kama Azam au Ihefu, jamaa mpira wanajua haswa.

Tanzania tunahitaji uwekezaji mkubwa ktk soka ili kufika hapo walipo, timu kama Mamelod wanaoipasua Al Ahly nje ndani usifikiri Mamelod ni kama Simba au Yanga, Mamelod wapo vizuri ktk uwekezaji.
Mamelodi hawana kombe lolote Afrika, n
 
Ivi unakuaje sawa na vilabu ambavyo mashindano ya Africa wakiingia wao wanafikiria ubingwa tu. Yaani wakati wewe plan yako na uwekezaji wako bado huwezi kuvuka robo unajilinganisha na wanao pambania ubingwa!!!

Waaarabu wamepiga hatua na wametuacha mbali, unatakiwa uwekezaji mkubwa na tuache ubabaishaji.
 
Back
Top Bottom