Watanzania tupaze sauti zetu kunusuru uhai wa maelfu ya vifaranga visivyo na hatia vinavyoenda kuangamia

Watanzania tupaze sauti zetu kunusuru uhai wa maelfu ya vifaranga visivyo na hatia vinavyoenda kuangamia

THE BROKER

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2014
Posts
743
Reaction score
915
Leo katika taarifa ya habari ya ITV saa 08:00pm wametoa taarifa ya mfanyabiashara huko Morogoro kukamatwa na mabox 200 yenye vifaranga vyenye thamani ya TZS 40M vilivyoingizwa nchini kinyemela kutoka Kenya.

Mwandishi amemhoji mtaalam husika wa Serikali Ni nini kitafuata baada ya ukamataji huu, mtaalam akawa na jibu moja tu "Tutaviteketeza kwa mujibu wa sheria"

Ningekuwa mimi ndio nmeulizwa hilo swali ningejibu "Tutachukua hatua mbalimbali ikiwemo kuvipima kuangalia Kama vimebeba vimelea vya magonjwa then mamlaka husika itaona Ni hatua gani zaidi zichukuliwe baada ya kushauriana.

Hii ni kwa sababu, endapo vitachomwa na ikaja kuthibitika havina magonjwa, kwanza ni kukiuka haki ya ya kuishi kwa viumbe hai, pili kupotezea nchi mapato ambayo yangeweza kupatikana endapo muingizaji angetozwa faini, tatu kupoteza Kodi ya mapato kutoka kwa muingizaji na mwisho wa siku kuua uchumi wa wafanyabiashara.

Kuliko vichomwe Kama itathibitika havina ugonjwa bora vigawiwe bure hata kwenye majeshi yetu kuongeza tija.

Kwa sababu tajwa hapo juu, nawaomba wanaJF wote na watanzania kwa ujumla tuungane kwa pamoja kupinga kitendo hichi kisitekelezwa kwa Hawa viumbe hai wenye Tina kubwa kiuchumi.

Pia soma > Tanzania kuchoma tena vifaranga kutoka Kenya?

Roho inaniuma Sana kwa kweli!
 
Wawapime na kama hawana magonjwa wapige mnada kama mwenye mali hana hela ya Kodi, tuache kutumia nguvu kila siku wakati tunahitaji pesa. Hii hata tukiwachoma haitusaidii kitu. Halafu najiuliza kuna nini Kenya mbona watu wanapenda mbegu ya vifaranga vya huko?
Sheria ndio inasema hivyo?
 
Ni kwamba hizi nchi zetu hatuwezi kuweka utaratibu wa kuuziana bidhaa kama hizi, na vipimo vikafanyika kuthibitisha ubora?
 
Umeongea pointi kabisa, jamaa hao wanasema wanateketeza huku wanatia ndani vifaranga 400 vikue viuzwe.
 
Ndo huyo huyo mkuu wangu ..huyo huyoo...mie nilienda 2015 nikabak kupiga selfie tu na kuku zake...bwana kuna watu wako serious jamani
Kabisa mkuu! Mimi nilienda mwaka jana.yule mtu ni noma sana kwenye ufugaji wa kuku,kama ndiye mwenye mzigo watamuumiza sana wakiteketeza hivyo vifaranga.
 
Ni mambo ya ajabu kabisa sijui nani katuloga, mpigeni faini jamaa pima hivyo vifaranga vikifaa viuzwe vikiwa na Corona ndo mteketeze.
Sasa mnatupa hadithi ya kuvichoma vyote Uongo mtupu mnapeleka kwenu kila kitu.
Tutaona hapa badae.
 
Kwani Sheria inasemaje kuhusu Hilo ,kwann hawataki kufuata Sheria ?
Kwa maswala ya Kodi unaweza ukafata Sheria zooote , ukafeli kipengele kimoja tu , ukawa msala mkubwa
Mambo kama haya yanatokea sana kimya kimya na kuna watu Hadi hupoteza maisha
 
hui NI mara ya pili sasa.mara ya Kwanza alikuwa marehemu aliwachoma Moto vifaranga kule Arusha.ngoja tuone mama nae kama ataanza kuua NAFSI ZISIZO NA HATIA
 
Back
Top Bottom