THE BROKER
JF-Expert Member
- Sep 10, 2014
- 743
- 915
Leo katika taarifa ya habari ya ITV saa 08:00pm wametoa taarifa ya mfanyabiashara huko Morogoro kukamatwa na mabox 200 yenye vifaranga vyenye thamani ya TZS 40M vilivyoingizwa nchini kinyemela kutoka Kenya.
Mwandishi amemhoji mtaalam husika wa Serikali Ni nini kitafuata baada ya ukamataji huu, mtaalam akawa na jibu moja tu "Tutaviteketeza kwa mujibu wa sheria"
Ningekuwa mimi ndio nmeulizwa hilo swali ningejibu "Tutachukua hatua mbalimbali ikiwemo kuvipima kuangalia Kama vimebeba vimelea vya magonjwa then mamlaka husika itaona Ni hatua gani zaidi zichukuliwe baada ya kushauriana.
Hii ni kwa sababu, endapo vitachomwa na ikaja kuthibitika havina magonjwa, kwanza ni kukiuka haki ya ya kuishi kwa viumbe hai, pili kupotezea nchi mapato ambayo yangeweza kupatikana endapo muingizaji angetozwa faini, tatu kupoteza Kodi ya mapato kutoka kwa muingizaji na mwisho wa siku kuua uchumi wa wafanyabiashara.
Kuliko vichomwe Kama itathibitika havina ugonjwa bora vigawiwe bure hata kwenye majeshi yetu kuongeza tija.
Kwa sababu tajwa hapo juu, nawaomba wanaJF wote na watanzania kwa ujumla tuungane kwa pamoja kupinga kitendo hichi kisitekelezwa kwa Hawa viumbe hai wenye Tina kubwa kiuchumi.
Pia soma > Tanzania kuchoma tena vifaranga kutoka Kenya?
Roho inaniuma Sana kwa kweli!