Watanzania tupige magoti kwa Mungu kumuombea Prof. Janabi ashinde Ukurugenzi WHO kanda ya Afrika

Watanzania tupige magoti kwa Mungu kumuombea Prof. Janabi ashinde Ukurugenzi WHO kanda ya Afrika

Sisi tumezoea kujinyenyekeza kwa Mama, Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.

Ni matumaini yetu atambariki Dr. Janabi hicho cheo.
Tayari Mama yetu alishafanya kazi ya kitume. Mpaka sasa kwa Uweza wa Mwenyezi Mungu tunakwenda kushinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima.
 
Lucas Mwashambwa unaona jinsi watu wamechoka na hizi propaganda za awamu hii?
Ila sio mbaya maana kila mtu anawasilisha hisia zake.

#MamaMitanoTena💪
Watu waache roho za wivu na chuki binafsi zisizo na msingi. Umaskini wako hauwezi kuondoka kwa kumuonea wivu mwenzako. Ni kazi pekee na kujituma kwako ndiko kutakuinua kimaisha.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nawaombeni kwa unyenyekevu na heshima kubwa sana kila mmoja kwa imani yake tupige Magoti na kujinyenyekeza mbele za Mwenyezi Mungu kumuombea Mtanzania Mwenzetu Profesa Mohammedi Janabi,mzalendo wa kweli aliyejitolea na kujitoa Maisha yake katika kulitumikia Taifa letu katika secta ya Afya.

Aweze kushinda uchaguzi wa Kujaza nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa WHO kanda ya Afrika. Nafasi iliyoachwa wazi na kubakia wazi kufuatia kifo cha Dkt Faustine Ndugulile aliyetangulia mbele za haki miezi michache kabla ya kushika rasmi na kukalia kiti hicho.

Soma Pia: Prof. Mohamed Janabi Miongoni mwa Wagombea wa Ukurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika

Uchaguzi huo unakwenda kufanyikia Geneva Uswiswi siku ya kesho kutwa yaani Tarehe 18-5-2025. Ushindi wa Profesa Janabi utakuwa ni ushindi wetu sote watanzania,itakuwa ni heshima kwetu watanzania, itakuwa ni ushindi kwa Taifa na itaendelea kututengenezea njia watanzania wengine kushika nafasi mbalimbali kimataifa. Kupitia ushindi wake itatusaidia watanzania kupata nafasi ya kufanya kazi katika shirika hili la Afya Duniani,tutapata fursa mbalimbali kama nchi na kama Taifa.

Itatuongezea Sauti katika maamuzi ,mipango , mikakati,mijadala na maazimio ya kimataifa. kila fursa itakayojitokeza tutakuwa na nafasi kubwa ya kuiona na kuipata . Vijana wetu na wataalamu wetu mbalimbali watapata fursa ya kukuza ujuzi na uzoefu wao kwa kufanya kazi na shirika hili la kimataifa .

Ndio Maana nawaombeni sana na kwa moyo wa unyenyekevu tuunganisheni Maombi yetu kumuombea heri na ushindi Mtanzania Mwenzetu ambaye anakwenda kuipeperusha Bendera yetu kimataifa. Tujue kuwa Profesa kalibeba Taifa letu mabegani mwake na sisi watanzania tunapaswa kuwa nyuma yake kumuombea kila la heri na ushindi mnono.

Mpaka sasa kama Taifa kupitia viongozi wetu mbalimbali wakiongozwa na Rais wetu Mstaafu na Mwana diplomasia mbobevu na mwenye uzoefu na ushawishi barani Afrika na Duniani kwote Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete amefanya kazi kubwa ya kuzunguka Bara zima la Afrika kuwasilisha ujumbe wa Rais wetu Mpendwa na kipenzi chetu watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan juu ya kuomba uungwaji mkono kwa mgombea wetu.

Lakini pia Mheshimiwa Rais wetu kipenzi alizungumza na Bara la Afrika kwa video yenye kueleza kwa kina juu ya Profesa Mohammedi Janabi na ni mtu wa namna gani na amefanya nini katika secta ya Afya na watarajie nini endapo atachaguliwa kushika nafasi hiyo. Ambapo mpaka sasa tunaendelea kumshukuru Mungu kwa kuwa ushindi upo Mikononi Mwetu na mataifa mbalimbali yanaendelea kutuunga mkono na kumuunga mkono mgombea wetu.

Kila nchi ina imani na Tanzania na watanzania. Hasa kwa kuzingatia historia ya Tanzania katika kulitetea Bara la Afrika na wa Afrika tangia wakati wa ukoloni,hali iliyosaidia nchi nyingi kujipatia uhuru wao kwa jasho na Damu ya watanzania. Kwa hiyo heshima hii ambayo tulijijengea kwamoyo wa upendo ,uaminifu ,huruma , unyenyekevu na kujitolea kwetu imeendelea kutupatia heshima sana mpaka leo hii na kupelekea kuungwa mkono kila tunapoomba nafasi za kimataifa.

Tumekuwa washindi wakati wote kwa sababu tunaaminika sana machoni pa wa Afrika wenzetu na Duniani kwote kwa ujumla wake. Hatujawahi kuwa wasaliti wala ubaguzi. kwetu sisi Binadamu wote ni sawa na wanastahili heshima na kuheshimiwa utu wao pasipo ubaguzi wa aina yoyote ile na kwa misingi ya aina yoyote ile.View attachment 3336400

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Sisi tunawapmbea Wazazi wako wapate walau hela ya kuburudika na CHIMPUMU 😁
 
Kwani huko CCM hamuwezi kuiba kura hadi uwaombe watu wapige sijui magoti na kujinyenyekeza?

Itapendeza sana akishindwa maana hizo taasisi za nje zikiwa zinawakemea kuhusu uvunjanji wa haki za binadamu mnasema wasiwapangie na wanaleta agenda za ushoga .

Pia hatuwezi kuwa na muwakilishi katika nchi inayomwaga damu za watu wanaotofautiana mawazo na watawala.

Na zaidi ya yote nchi isiyoheshimu demokrasia na mfumo kandamizi wa uchaguzi unaopendelea chama kimoja haistahili kupata hiyo docket.
CHADEMA wangeweza vipi kufanya mikutano yao ya hadhara kwa uhuru kabisa kama hakuna demokrasia? Au kwako demokrasia ni nini?
 
CHADEMA wangeweza vipi kufanya mikutano yao ya hadhara kwa uhuru kabisa kama hakuna demokrasia? Au kwako demokrasia ni nini?
Viongozi wa CCM wamekamtwa mara ngapi bila sababu yoyote au kuzuiliwa kwa kunyimwa uwanja wa kufanya mikutano mwaka huu?

Jibu hilo swali tuendelee.
 
Tupunguze kumsumbua Mungu,
Ombea mzazi na watoto zako, unaombea mtu ambae hatumuelewi.
 
Viongozi wa CCM wamekamtwa mara ngapi bila sababu yoyote au kuzuiliwa kwa kunyimwa uwanja wa kufanya mikutano mwaka huu?

Jibu hilo swali tuendelee.
Kwa hiyo unataka wakamatwe pasipo kosa? Kama unaona unaonewa nenda mahakamani akafungue shauri
 
Tanzania tu imemshinda ndio sembuse huko Bora waachiwe watu makini kama Rwanda kidogo Leo unakosea dawa hospitali unaambiwa ununue kwa nurse wakati dawa zinaingia hospital lakini hakuna usimamizi futa kabisa hiyo
 
Tanzania tu imemshinda ndio sembuse huko Bora waachiwe watu makini kama Rwanda kidogo Leo unakosea dawa hospitali unaambiwa ununue kwa nurse wakati dawa zinaingia hospital lakini hakuna usimamizi futa kabisa hiyo
Mchango wa profesa Janabi ni mkubwa sana hapa Nchini katika secta ya Afya
 
Back
Top Bottom