Watanzania tupige magoti kwa Mungu kumuombea Prof. Janabi ashinde Ukurugenzi WHO kanda ya Afrika

Piga magoti mwenyewe. Kwa sasa tunaombea mabadiliko kwenye nchi yetu.

#No reforms no election
Hili dubwasha huwa ni jinga sijawahi ona, ukisoma maandiko yake unaeleewa tu kwamba ni mtu ambae either dishi limeyumba au folder moja limiliwa na virusi
 
Kupitia ushindi wake itatusaidia watanzania kupata nafasi ya kufanya kazi katika shirika hili la Afya Duniani,tutapata fursa mbalimbali kama nchi na kama Taifa.
Kwani yule mtoto wa mzee Malecela hajawasaidieni kuwatengenezea njia ili mpewe fursa hadi awe huyo Janabi?
 
Tanzania atuwezi kushinda mara mbili.
Dr Janabi aendelee kuwa Kiongozi wa Muhimbili na mshauri wa afya kwa Wa TZ
 
Ushindi wa Janabi una tija gani kwa mtanzania wa vijijini huko?
Kwani lazima kumkimbiza awe kule si mpeni ubalazo kama mnataka awe mbali na nchi?
Eee Mwenyezi Mungu Mwenye haki na unayependa haki ya kuishi, ikiwa huyu mtu ni anget wa malaika Israel na aangukie pua asishinde kwa jina lako tukufu, amin amin.
 
Huyu na Elimu yake ya kuunga unga . Janabi kafika hapo kwa uchawa Ila kichwani mweupe .
 
Mtu alie shauri mpige upinzani na kupeana kesi za uhaini nahisi hakuangalia kesho. Nilianza msikitikia Prof Janabi kiukweli na mpenda ila kwa hali ilivyo duniani huku kuhusu Tz. Mim nafunga mdomo.
 
Kama vile mwenendo wa William Ruto ilivyosababisha Raila Odinga kukosa kiti cha Mwenyekiti wa Commission ya Africa, ndivyo ambayo Samia Suluhu anavyoenda kusababisha Prof.Janabi apigwe chini.
 
uchaguzi ni lini??
ila, tangu jamaa aanzishe utaratibu wa kulipia getini muhimbili unapoingia na gari, sijafurahishwa kabisa, maana watu wanakwenda muhimbili kwa sababu ya changamoto za afya, siyo shopping mall kama mlimani city, kwamba hata ukiambiwa kulipia, siyo neno. Waziri wa afya aangalia namna ya kurekeshisha hili, ni kero kwa ndugu wa wagonjwa. Mwanzoni tuliaminishwa kwamba kuna watu wanapaki magari na kwenda kufanya kazi posta, na ilikuwa bure ukiingia na kutoka ndani ya nusu saa. Wameondoa huo utaratobu, sasa hivi unalipia hata kama umeingia, ukamshusha mgonjwa na kuondoka ndani ya dakika 10, lazima ulipie. Sasa kama hii ndiyo njia ya kuonyesha ubunifu wa kuongeza mapato ya taasisi, amefeli sana.
 
Upige magoti ya nini we bwege nini.
Akiwa na vigezo anashinda hana hashindi hata ukalale juu ya bati la kanisa.
 
Mimi sitamani atoke pale Muhimbili. Amefanya kazi kubwa sana so far. Amepabadilisha mno. Pasafi, pameanza kunyooka.. imekuwa kama JKIC kipindi anaiongoza (ambayo sasa imeanza kuharibika tangu aondoke). Angebaki tu Muhimbili jamani.
 
Mnataka ashinde ili iwe rahisi kwenu kupitisha agenda zenu za kishetani na kichawa?, bahati mbaya huyo jamaa angekuwa na hicho cheo kipindi cha Covid-19 si ajabu angemshauri jiwe wananchi wapigwe lockdown na kufuata sera mbovu za kishetani.

Siwalaumu maana mna agenda zenu, bahati mbaya wananchi nao wana amka taratibu na kuanza kufahamu njama zenu ovu mnazotumia kuharibu taifa.
 
Mmeshamharibia! Sasa hivi kwa yanayoendelea nchini ya kuteka,kujeruhi na kuua watu,kumfungulia Lissu kesi yenye sura ya kisiasa kumeshaichafua nchi yetu machoni pa jumuia ya kimataifa!
Sidhani kama atatoboa.
 
Pelekeni polisi wakapige mabomu kwenye huo uchaguzi Janab atangazwe mshindi. Kama vipi wanaccm mumuombee ashinde. Sisi tunataka ashindwe tuanze sherehe.
 
Walimaliza kazi ambayo ilikuwa ya muhimu kwao wakaenda kuhiji Macca!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…