Idrissou02
JF-Expert Member
- Jul 31, 2018
- 354
- 656
Ishawahi kukukuta siku ambayo mpaka umefika mchana wa saa 9 hujaweka kitu tumboni, sio kwamba umefunga hapana bali huna hela ya kula? Ukaona kimbilio pekee ni kumtafuta mtu wako wa karibu akukopeshe angalau hela ya kula tu ili uondokane na zahma inayokukuta. Ukamtafuta wee kwenye simu bila mafanikio mpaka hatimae ukaja kumpata lakini jibu alilokupa likawa ni la kukatisha tamaa kabisaa. Akakuambia, "kulala na njaa siku moja sio jambo la ajabu ndugu yangu mbona kuna watu wengine kibao wanalala njaa".
Naam huu ni mfano mzuri wa kilichotukuta watanzania tuliokuwa tunamsubiria " mama" atoke kwenye ziara yake ya kutangaza utalii huko marekani aje kutukomboa na mfumuko mkubwa wa bei ambao hauendani na vipato tunavyoingiza watanzania. Cha ajabu mtu huyu tuliekua tunaeka matumaini kwake akasemaje alivyotua nchini?
Akasema kwamba ni lazima mfumuko wa bei utokee kutokana na hali ya vita uko ulaya. Naam akakwamia hapo, hakuja na suluhisho la aina yeyote la kuleta unafuu kwa wanaanchi, na tena isitoshe mafuta yakazidi kupanda bei baada ya yy kutua nchini.
Ziko wapi zile ziara za kutatua matatizo ya wananchi? Wizara ya nishati imekua ikiyumba sana kwa ukimya wao tokea jambo hili lianze, hatua gani imechukuliwa kwao? Wananchi tunalia shida jamani hali ni zaidi ya tete alafu bado tu kuna hela zinaendelea kupotezwa kuonesha filamu za "loyo tua" mikoa ya arusha na dar es salaam.
Sawa bana filamu hizo wataendelea kuangalia wadau wa utalii tu na makada wa "mama". Nasubiri nione wananchi wa hali ya nchini watavumilia hali ngumu mpaka itakapofika kiwango gani.
Shaabash